Napendekeza iundwe Tume Huru ya kuchunguza kifo cha Hayati Magufuli

Fanya kazi wewe, acha kubwabwana mtandaoni. Haya unayoandika yatakugharimu muda si mrefu. Hatuwezi kuwafumbia macho wapumbavu wachache wanaotaka kuichonganisha serikali na wananchi wake, HATUWEZI.
Well Noted Mkuu..
 
weye naona umekaririshwa. Ongea mengine. Hilo la Nyerere ulishalisemea. Kifo cha Nyerere siyo msingi wa kifo cha Magufuli kutochunguzwa. Kila jambo lina mwisho wake.
Nyerere ndio rais wa kwanza wa nchi hii, JPM ni watano. Huwezi kuiongelea Tanzania bila ya kuwaongelea waasisi wake.

Ni sawa umpe umuhimu mtoto wa tano wakati wa kwanza mpaka wanne wapo.

Inaelekea wewe ni bwana mdogo wa miaka hii ya Hayati Magufuli, huna uzoefu wa Tanzania pana.
 
Vifo vya Nyerere na Mkapa havikuchunguzwa huyo JPM alikuwa na utakatifu upi wa kipekee?.

Nyerere alifia hospitalini Uingereza kama kuuwawa yeye angekuwa wa kwanza.

Narudia kukwambia, ondokana na dhana nyingi kichwani mwako hazikusaidii.
Wafuasi wengi wa magufuli, ni zaidi ya misukule! Inashangaza sana. Na kama angeendelea kutawala, huenda kuna watu wangemgeuza kabisa kuwa mungu.
 
Wafuasi wengi wa magufuli, ni zaidi ya misukule! Inashangaza sana. Na kama angeendelea kutawala, huenda kuna watu wangemgeuza kabisa kuwa mungu.
Ni kweli kabisa. Kisichunguzwe kifo cha Sokoine, kisichunguzwe cha Nyerere, kisichunguzwe cha Omar Ali Juma kije kichunguzwe cha Magufuli?.

Hao wengine waliotangulia hawakuwa na umuhimu kwa taifa!!.
 
Haijalishi sijaja hapa kwa story za Nyerere, Naunga mkono hoja iliyotolewa kuwa iundwe tume Huru kuchunguza kifo cha Magufuli.
Na hoja ni kuunda tume basi. hayo ya Nyerere kuwa nayo mwenyewe.
 
Haijalishi sijaja hapa kwa story za Nyerere, Naunga mkono hoja iliyotolewa kuwa iundwe tume Huru kuchunguza kifo cha Magufuli.
Na hoja ni kuunda tume basi. hayo ya Nyerere kuwa nayo mwenyewe.
Hiyo tume usitegemee kusikia imeundwa. Haina sababu wala msingi.
 
Huyu boys tumchngeze kwa lipi kama ni hivyo tuanze na Mkapa
Tatizo la wafuasi na wanufaika wa utawala wa magufuli, hawakuwahi kumchukulia mtukufu wao kama mwanadamu ambaye anaweza kufariki muda wowote ule!

Waliamini angeishi miaka mingi! Lakini ndiyo hivyo tena. Mwenyezi Mungu alimtwaa kabla ya muda walio utarajia. Na sasa hawataki kuukubali ukweli. Sijui wanataka uchunguzi wa aina gani! Na kwa akili zao fupi, wanatarajia kupata majibu wanayo yataka!! Hopeless kabisa!
 
Ni hawa wanaopinga kila kinachofanyika leo hii wakisema mama hafai wakati hayati alimtegemea kama msaidizi wake kwa muda wote wa urais wake.
 
Anza kutoa mapendekezo, unataka huo uchunguzi ufanyike vipi na uwahusishe watu gani, unaweza kusaidia kupatikana kwa ule moshi wa ruangwa ili nao ufanyiwe uchunguzi...maana na wenyewe umeutaja hapa.
 
Yaaah na ndo wapiga kura halisi, pia wahudhuriaji kampeni, safari hii 2025 huyu mama atapiga kampeni sijui wapi na chama chake.

Ni heri aanze kusafisha kwa kutembelea wananchi.
Yatakapo mkuta asijekusema hakuambiwa
 
Itabidi hata cha Mzee wetu Mkapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…