Napendekeza kazi za kuhesabu idadi ya watu (Sensa 2022) ifanywe na wajumbe wa nyumba 10 , pesa zitakazookolewa zikajenge flyover TAZARA

Wewe unafikiri kwenye sensa kinachofanyika ni kuhesabu watu tu. Huwa kuna dodoso refu na fupi! Dokezo refu huangazia pia mambo mbalimbali. Ndiyo maana kwa tangazo lilotoka wamesema awe form four ambaye angalau akierekezwa anaweza elewa cha kufanya.
Kwahiyo mtu anaeweza kufanya majukumu ya mjumbe atashindwa kufanya hayo madodoso? Au we unaposikia dodoso unaona ni kitu cha ajabu sana, si ndio?
 
Nakuhakikishia ni 10% ya wajumbe wanaofahamu wananchi wao na makazi yao.

Ila 90% ya wajumbe hawajui hilo, wao kazi yao ni kusaini barua tu.

Utapata 20% ya taarifa sahihi.

Hizo nyingine ni uongo.
Hata kama hawajui, si ndio atapewa taarifa akienda kuwatembelea, au hao watakaoajiriwa ndio wanawajua wenye nyumba?
 
Kuna namna zoezi litafeli,,, Wajumbe wote ni sisiemu na utendaji wa watu wa sisiemu ni wa hovyo sana....

Mashaka yangu tu
Hamna hoja hapa, kwani hii sensa inaendeshwa na serikali ya Chadema?
 
Wazo zuri, ila tatizo wajumbe wa nyumba 10 wengie hawana elimu ya kutosha, alaf matumizi ya smartphone yamewapita kushoto.

Zoezi litakuwa gumu kwao.
 
Wazo zuri, ila tatizo wajumbe wa nyumba 10 wengie hawana elimu ya kutosha, alaf matumizi ya smartphone yamewapita kushoto.

Zoezi litakuwa gumu kwao.
Kwani kigezo cha kuweza kuhesabu watu ni kujua kutumia smartphone? Wao watakusanya data kwa analog, then itakuwa ni jukumu la afisa mtendaji ku-digitize na kutuma taarifa kwa mamlaka husika...
 
Dogo sensa sio kama unavyofikiria kwa nchi hizi maskini.

Kulikuwepo na kitu kinaitwa EPR ( village electronic population register) wakapewa baadhi ya hao unaosema kwa baadhi ya wilaya hela nyingi zikatumika ,ulizia matokea yake..

Alafu ujue sensa sio kuhesabu watu like 1,2,3,...n hapana,sensa inajumuisha demographic variable nyingi, economic variable nyingi, social variable nyingi.

Na sasa kuna variable za majengo na anwani za makazi na huwezi mpa tablates mjumbe akaanze kuhesabu watu.

Sensa kwa afrika ni very cost fully

Wenzetu wazungu wameendelea kijitali ndio maana kwao hutasikia sensa period .Coz wanatumia de facto method of sensa.
 
Mtu asiyejua kusoma wala kuandika hawezi kupewa ujumbe, hii kali sasa. Kama hii ni kweli, afisa mtendaji na mwenyekiti watawajibika kumjazia fomu zake, maana wao ndio walifanya uhuni wa kumpa ujumbe.
Mkuu unashangaa!? Sasa si kwa mjumbe tu.

Kuna wenyeviti wengi tu wa kupita bila kupingwa hawajui kusoma na kuandika. Unakuta Halmashauri nzima ya Kijiji ukimtoa mtendaji wenyeviti wa vitongoji tu ndio wanaojua kusoma na kuandika japo kwa kubabaisha, hao ni kwakuwa wanafanya shughuli za uandishi mara kwa mara! The rest ni tabu tupu. 2019 & 2020kulikuwa na chafuzi badala ya chaguzi
 
Hakuna kitu kama hicho, kujua kusoma na kuandika ni pre-requisite
 
Sasa hapo ndio umeongea nini, kwani nani hajui hayo, wewe sema ni kitu gani kitawashinda wajumbe wa nyumba 10?
 
Nani kakwambia dunia inazungukia dar tu?
 
Huwa najiuliza kwani kuna ulazima wa kufanya sensa wakati tunaweza kuwa tunarekodi taarifa ya vifo na kuzaliwa kila mwaka kwa mfumo wa kielectronik ili kumbukumbu zinakua zinajipunguza na kujiongeza kwa muda sahihi
Wengine wanazaliwa nyumbani vifaa..hawaendi hospital..na wengine wanakufa taarifa zao haziendi popote..wengine wanachama nchi pia
 
wajumbe wengi hata kusoma hawajui,

wacha pesa iingie mtaani pato la mmoja mmoja liongezeke
Mtoa mada hafahamu kwamba mwaka huu vitatumika vishikwambi (tablets) kukusanyia taarifa, sio wajumbe wote wanaweza kufanya hizo kazi.
 
Sio kweli, Mi sijawahi kuona mjumbe hajui kusoma, anatekelezaje majukumu yake ya kushuhudia kuandikishana kama hajui kusoma?
Tanzania ni kubwa, tembea uone usijifiche mtaa moja ukahitimisha ndio Tz nzima iko hivyo.
 
We dogo wajumbe wa ccm hawajui kusoma Wala kuandika u know it?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…