Napendekeza kazi za kuhesabu idadi ya watu (Sensa 2022) ifanywe na wajumbe wa nyumba 10 , pesa zitakazookolewa zikajenge flyover TAZARA

Napendekeza kazi za kuhesabu idadi ya watu (Sensa 2022) ifanywe na wajumbe wa nyumba 10 , pesa zitakazookolewa zikajenge flyover TAZARA

Wazo lako ni kwa nia njema lakini naamini rahisi ni ghali. Nnavyoelewa sensa hutakiwa kufanywa kwa siku moja tu. Hawa wajumbe zetu wa nyumba kumi (siku hizi, nasikia bwana yule,alizifanya za nyumba 50, siyo 10 tena) watayaweza hayo?

Halafu kwanini zikajenge flyover palepale ambapo lipo halijamaliza hata miaka 10? Au bwana yule aliona ile design iliyotolewa wakati wa Kikwete haifai na yake na engineer wake imebuma?

Rahisi ni ghali.
shida design ya kikwete inataka anaepita atoe hela kama Kigamboni.
 
Mzee kiufupi ni wengine tunazisubiria hizo kazi za muda ili tupate hata vimtaji.
Hasa national cake tutashare vp na sisi.
Wakati mwingine mbn huwa wanajibana matumizi lakini matokeo kwa. Wananchi huwa 0.

Hiyo hela watu wapewe wapige kazi.
Kama uko ofisini na unaandika uzi huu jua mtaani vijana hali siyo nzuri.
Uko sahihi lakini angalia upande wa ajira zilivyo ngumu. Ila kwa kuwa ni ajira tu ya muda basic ilete ahueni kiduchu.
 
Kwa kupitia serikali za mitaa / vijiji (local government) , wajumbe wa nyumba 10 wapewe fomu za sensa na wapite kwenye nyumba zilizochini yao, wapewe wiki moja tu wawe wameshazitembelea nyumba zote zilizochini yao na kuzijaza fomu zote kwa kila nyumba, wakazikabidhi fomu hizo kwenye ofisi za serikali ya mtaa/kijiji, ofcourse wapewe na posho kidogo.

Afisa mtendaji akusanye zote na kuziwasilisha ofisi ya wilaya/mkoa ya sensa kwa ajili ya majumuisho na uchakataji wa taarifa.

Pesa zitakazookolewa ziende zikajenge flyover pale TAZARA, foleni ya malorry pale imesababisha hali kuwa mbaya sana.
Wajumbe wengi hawajui kutumia kishkwambi
 
Basi nisameheni nimeteleza, zikatumike kila wilaya kuboresha huduma ya afya [emoji23][emoji23]. Ila foleni za malorry yanayoenda mikoa mbali mbali ikipungua, hata gharama za usafirishaji kwenda mikoa na wilaya husika inapungua.
Nashangaa kwann TAZARA Hawakujenga kama UBUNGO badala yake wakaeka daraja...
Bora wangelieka kinyume basi wa Mandela Road wapite juu ila wa Goms ndio wanapita juu
 
Kwa kupitia serikali za mitaa / vijiji (local government) , wajumbe wa nyumba 10 wapewe fomu za sensa na wapite kwenye nyumba zilizochini yao, wapewe wiki moja tu wawe wameshazitembelea nyumba zote zilizochini yao na kuzijaza fomu zote kwa kila nyumba, wakazikabidhi fomu hizo kwenye ofisi za serikali ya mtaa/kijiji, ofcourse wapewe na posho kidogo.

Afisa mtendaji akusanye zote na kuziwasilisha ofisi ya wilaya/mkoa ya sensa kwa ajili ya majumuisho na uchakataji wa taarifa.

Pesa zitakazookolewa ziende zikajenge flyover pale TAZARA, foleni ya malorry pale imesababisha hali kuwa mbaya sana.
La saba wale wanajua hata kutumia kishkwambai?

Kiujumla sensa itatumia bil.629 ,,Aisee pesa nyingi sana hii Serikali iangalie nna ya kupunguza gharama.
 
Dogo huna hoja ya maana hapo, hoja haina mashiko na haiwezi chukuliwa na kufanyiwa kazi.

Ni hoja ambayo ikichukuliwa itawekwa pending kwanza.
Wewe hapa ndio huna hoja, kwamba wajumbe wa nyumba 10 watashindwa kujaza hizo fomu?
 
Kiongozi wa 'malaika' alishajenga flyover TAZARA. Au unataka kufuta 'legacy' kwa kujenga nyingine?

Unawachokoza sukumagengi
 
Mtoa mada hafahamu kwamba mwaka huu vitatumika vishikwambi (tablets) kukusanyia taarifa, sio wajumbe wote wanaweza kufanya hizo kazi.
Wewe unasema watatumia tablets, as if internet ipo kila mahali nchini na as if hiyo tablet inauzwa buku5, mimi napendekeza hao wajumbe wajaze fomu kwa peni na karatasi, kisha afisa mtendaji azifanyie digitization kwa ajili ya uchakataji na kuzituma taarifa mahala husika
 
Wewe unasema watatumia tablets, as if internet ipo kila mahalai nchini, mimi napendekeza hao wajumbe wajaze fomu kwa peni na karatasi, kisha afisa mtendaji azifanyie digitization kwa ajili ya uchakataji
Tumeshavuka huko kwenye peni na karatasi.
 
Kwa kupitia serikali za mitaa / vijiji (local government) , wajumbe wa nyumba 10 wapewe fomu za sensa na wapite kwenye nyumba zilizochini yao, wapewe wiki moja tu wawe wameshazitembelea nyumba zote zilizochini yao na kuzijaza fomu zote kwa kila nyumba, wakazikabidhi fomu hizo kwenye ofisi za serikali ya mtaa/kijiji, ofcourse wapewe na posho kidogo.

Afisa mtendaji akusanye zote na kuziwasilisha ofisi ya wilaya/mkoa ya sensa kwa ajili ya majumuisho na uchakataji wa taarifa.

Pesa zitakazookolewa ziende zikajenge flyover pale TAZARA, foleni ya malorry pale imesababisha hali kuwa mbaya sana.
Hii ni zama ya kulamba asali babu kama unauchungu na hii mali ya uma utachelewa Sana.
 
Wewe hapa ndio huna hoja, kwamba wajumbe wa nyumba 10 watashindwa kujaza hizo fomu?
Kijana uko nyuma sanaa ya wakati, sensa ya mwaka huu inatumia technology ya kishikwambi ,madodoso yamewekwa huko.

Naona bado uko kipindi cha nyerere cha makarani kutembea na makaratasi na kuanza kupika data wakiwa chini ya mti.

Nchi nyingi duniani kwa sasa zimehama kwenye mafumo yako zinaenda kutumia technology ya kishikwambi kwenye kufanya tafiti.

Wewe unataka kuturudisha nyuma.

Nchi inapambana kusambaza umeme kila kona ya nchi ili tuweze kutumia technology kufanya mambo mengi wewe una discourage haya mambo.

Dogo nenda na wakati. Tulishatoka huko
 
Mtu asiyejua kusoma wala kuandika hawezi kupewa ujumbe, hii kali sasa. Kama hii ni kweli, afisa mtendaji na mwenyekiti watawajibika kumjazia fomu zake, maana wao ndio walifanya uhuni wa kumpa ujumbe.
Umesahau kuna madiwani walishawai shindwa kusoma kiapo nadhani ilikuwa morogoro au ww ni mgeni hapa galilaya(Tanzania)
 
Wazo lako ni kwa nia njema lakini naamini rahisi ni ghali. Nnavyoelewa sensa hutakiwa kufanywa kwa siku moja tu. Hawa wajumbe zetu wa nyumba kumi (siku hizi, nasikia bwana yule,alizifanya za nyumba 50, siyo 10 tena) watayaweza hayo?

Halafu kwanini zikajenge flyover palepale ambapo lipo halijamaliza hata miaka 10? Au bwana yule aliona ile design iliyotolewa wakati wa Kikwete haifai na yake na engineer wake imebuma?

Rahisi ni ghali.
Kwani Bibi umesaliti chama au na wew umeanza kulamba asali.
 
We dogo wajumbe wa ccm hawajui kusoma Wala kuandika u know it?
Sio kweli, wajumbe wote wanajua kusoma na kuandika, na kama walimpa ujumbe asiejua kusoma na kuandika, basi mwenyekiti na mtendaji wake watawajibika kumjazia hizo fomu, maana wao ndio wamefanya huo uhuni
 
Back
Top Bottom