FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 38,920
- 44,970
- Thread starter
-
- #41
Miezi kadhaa kabla ya uchaguzi, kila mtu mwenye NIDA atapaswa kuainisha NEC ni namba ipi kati ya zile alizosajili ndio atapigia kura, hivyo ikifika uchaguzi, namba hiyo tu ambayo wewe ndio unayo physically, ndio itakuwa na option ya kupiga kura. Fingerprint ni kwa mawakala tu kwa wale wasio na simu.Labda tutumie fingerprint. Unakuta namba zingine umemsajilia mtoto, nyingine ya simu ya kubaki nyumbani nk. Vile vimashine vya fingerprint vitafaa sana kurahisisha mambo na itaupdate database ya fingerprint pia
Unadhani sijasoma comrade? Sijaona tu uchambuzi wa maana kwa wasio na simu mkuu, ni kama umeubadili rangi tu utaratibu wa sasa, ambao unatoa mianya ambayo ndiyo kelele kuu.Mbona kwenye uzi nimeeleza nini kifanyike kwa wale wasio na simu? Unafaidika nini kukurupuka kucomment bila kusoma thread?
Umesoma na hujaona, kwahiyo niliposema wasio na simu watapiga kura kwa mawakala wa Tigopesa kwa kutumia mashine za bank za fingerprint nayo hukuiona?Unadhani sijasoma comrade? Sijaona tu uchambuzi wa maana kwa wasio na simu mkuu, uko kwenye utaratibu wa sasa unaotoa mianya ambayo ndiyo kelele kuu.
Ova
Kwa utaratibu wako, unaweza kuwa msaada kwa mwenye simu tu, ila kwa wasio na simu, utaratibu wako unawabakiza kwenye utaratibu wa sasa unaotoa mianya.Umesoma na hujaona, kwahiyo niliposema wasio na simu watapiga kura kwa mawakala wa Tigopesa kwa kutumia mashine za bank za fingerprint nayo hukuiona?
Upigaji kura kwa mawakala wa Sim banking ni biometric, hivyo si sawa na ilivyo sasa, alama ya kidole ni unique, ukipiga kura ni kura moja tu.., mianya inakuwa imezibwa.., au hao mawakala watachongesha fingerprint ambazo hazipo NIDA, ofcourse not..Kwa utaratibu wako, unaweza kuwa msaada kwa mwenye simu tu, ila kwa wasio na simu, utaratibu wako unawabakiza kwenye utaratibu wa sasa unaotoa mianya.
Hata sasa wanapiga kura kwa hao mawakala, ambao ni wanaCCM wanaovaa tshirt's za NEC tu, na wanasimamia watu kupiga kura za udanganyifu.
Ova
Nadhani ungejielekeza kujua kura zinaibwaje? Nadhani utapata njia nzuri. Bila shaka hujui kama hadi sasa matapeli wanasajili namba za simu, na bado kuna fingerprint.Upigaji kura kwa mawakala wa Sim banking ni biometric, hivyo si sawa na ilivyo sasa, alama ya kidole ni unique, ukipiga kura ni kura moja tu.., mianya inakuwa imezibwa.., au hao mawakala watachongesha fingerprint ambazo hazipo NIDA, ofcourse not..
Mbona unahoji ambacho nimeshakijibu, hata kama mtu kasajilishwa laini 100 za simu, bado NIDA namba ni moja tu kwa laini zote hizo, na laini yoyote kati ya hizo 100 ikipiga kura, hizo zingine zote hazitaweza kupiga tena kura. Pia kama kuna laini za simu za ziada ambazo mtu alisajilishwa bila yeye kujua, kuna utaratibu upo tayari wa mtu kukagua namba zote za simu zilizosajiliwa kwa NIDA yake na kufuta zile zote ambazo hazitambui, NIDA namba ikishatumika kupiga kura, haitaweza tena kurudia kupiga kura, finger print ni unique. Na pia miezi kadhaa kabla ya uchaguzi, lazima mtu aainishe NEC kwamba ni namba ipi kati ya zile alizonazo atatumia kupigia kura, na hiyo tu ndio itakuwa na access ya kupiga kura, sasa kipi huelewi?Nadhani ungejielekeza kujua kura zinaibwaje? Nadhani utapata njia nzuri. Bila shaka hujui kama hadi sasa matapeli wanasajili namba za simu, na bado kuna fingerprint.
Hii ni Tanzania, unajua kwanini namba za magari za 3D zilitolewa kwa nguvu? Ndiyo maana nimeelewa mpiga kura mwenye simu yake, lakini sijaelewa wa kwenda kupigia kura kwa mtu.
Kwa Tanzania kupiga kura usiyoweza kuiwekea kumbukumbu kwenye kifaa chako, ni kama utaratibu wa sasa tu. Upige kura halafu ukae mbali na kituo umbali wa mita ngapi sijui.
Fingerprint haijawa dawa Tanzania, maana simu za udanganyifu bado zinasajiliwa, na zinatumia kutuma meseji za majaribio ya kututapeli.
Ova
Sijui umeelewaje hoja yangu? Lakini, ulichofafanua sicho nilichomaanisha, ila nilikupa huo mfano wa matumizi yenye udhibiti wa fingerprint ambayo yameendelea kuwa holela.Mbona unahoji ambacho nimeshakijibu, hata kama mtu kasajilishwa laini 100 za simu, bado NIDA namba ni moja tu kwa laini zote hizo, na laini yoyote kati ya hizo 100 ikipiga kura, hizo zingine zote hazitaweza kupiga tena kura. Pia kama kuna laini za simu za ziada ambazo mtu alisajilishwa bila yeye kujua, kuna utaratibu upo tayari wa mtu kukagua namba zote za simu zilizosajiliwa kwa NIDA yake na kufuta zile zote ambazo hazitambui, NIDA namba ikishatumika kupiga kura, haitaweza tena kurudia kupiga kura, finger print ni unique. Na pia miezi kadhaa kabla ya uchaguzi, lazima mtu aainishe NEC kwamba ni namba ipi kati ya zile alizonazo atatumia kupigia kura, na hiyo tu ndio itakuwa na access ya kupiga kura, sasa kipi huelewi?
Kama mtu anaweka pesa kwenye simu na anaondoka, na kisha baade akiangalia salio lake anaikuta pesa yake, basi hata kura yako utaikuta tu..
Bank servers huwa ni ngumu kuchezea kwa sababu hazipo independent, zinahuishwa na servers nyingine nyingi kote duniani, ukichezea server yako itakuwa rejected na server zingine zote.. (Self auditing system). Ni kama technology inayotumika kutunza ledgers za ‘Cryptocurrency’ za Bitcoin nk., aisee huibi wala kugenerate fake currency hata moja, maana users ndio wana act kama servers, sasa server yako moja uichezee iseme CCM wana kura milioni 5, wakati kuna servers zingine elfu moja zinasema CCM wanakura milioni 1 tu, automatically server yako inakuwa blocked na kufungwa..
Kumbuka, kura itakuwa treated kama Currency
Unachosema nilikielewa. Kwamba kuna watu wanasajili laini za ziada kwa kutumia fingerprint za watu wengine na kuzitumia kufanya utapeli hiyo inawezekana kwa sababu tuSijui umeelewaje hoja yangu? Lakini, ulichofafanua sicho nilichomaanisha, ila nilikupa huo mfano wa matumizi yenye udhibiti wa fingerprint ambayo yameendelea kuwa holela.
Kwamba tuna usajili wa namba za simu kwa fingerprint, lakini bado zipo namba za simu zinasajiliwa na kuwa zikitumika kutapeli, zikiwa ni namba za wasiojulikana ila zinatumika.
Hata mfumo wa sasa wa upigaji kura wa Tanzania ni mzuri na umelindwa sana, lakini, vile kuwa unapiga kura kwa wakala ndipo penye shida, kwani kura yako iko kwa wakala.
Ni tofauti na mwenye simu yake kwa mujibu wa mfumo wako, yake iko salama.
Na umesema vizuri kuwa bank severs ni ngumu kuchezewa kwa sababu zinatumia microsoft security software, ila japo ni ngumu, ila zinachezewa na hela zinaibwa.
Mfano, kuna kesi ya CRDB ina miezi nane sasa, ilianzia pale Kituo cha Selander Bridge, watuhumiwa ni Wakenya, wako Keko, wameingilia mfumo wakachota hela nyingi.
Wengine wamejenga maghorofa Mbezi ya Kimara ili wayauze na kutakatisha. Kama una nafasi nenda pale kituoni wanaweza kukueleza.
Hata kesi ya Tabora ya CRDB, watu wa ndani ya CRDB kwa kushirikiana na watu wa nje, wamedanganya mfumo na wakachota hela.
Hivyo, bado mimi nauelewa mfumo wako kwa minajili ya kutatua tatizo, ni kwa upande wa wamiliki simu tu. Huko kwa wasio na simu, I'm sorry, No!
Ova
Labda useme Yas PesaItakapofika uchaguzi mkuu 2025, mtu aruhusiwe kupiga kura kwa kutumia simu yake ya mkononi kwa kutumia mifumo ya mobile money.
Pawekwe kipengele cha kupiga kura kwenye menu, ambapo atachagua Rais, Mbunge, Diwani, kisha atatuma kura yake.
Kwa wasio na simu wataenda kwa mawakala kwa kutumia alama za vidole zilizosajiliwa na Nida, atatumia tu mashine zile zile za bank au smartphone za mawakala zilizoongezwa kipengele cha kupiga kura.
Kwa kuwa pesa za kwenye Tigopesa ni ngumu kuiba, hata hizi kura zitakuwa salama.
===========================
KURA kuwa treated kama CURRENCY
“Kura ikitumwa inahuishwa kwenye servers zote instantly hadi zile zilizopo kwenye bank za nje ya nchi.
Sasa ukibadili taarifa kwa kufoji kwenye server moja, server zingine zote zitakataa kureconcile na server yako iliyochezewa.
Ni kama unavyotuma oesa toka Airtelcmoney kwenda kadi ya bank ya Visa au Mastercard inayofanya malipo marekani, taarifa zote zinahuishwa kote, lazima pawe na reconciliation, huwezi kufoji chochote!
Kimsingi hapa, tunachukulia kura kama ‘Currency’, na inakuwa treated just like currency, yaani kuiba kura inakuwa kama umeiba pesa!! Na ukituma kura ni sawa na umetuma pesa!!”
Na kama jinsi unavyoangalia salio lako la bank au simu kwa uhakika kabisa, basi hata NEC wataweza kupata matokeo ya Urais, Ubunge na Madiwani kwa kuangalia tu salio lao kama mtu anavyoangalia salio lake kwa simu.
Mabank na mitandao ya simu itaingiza pia kipato kwa kuruhusu mifumo yao kutumika, wanaweza wakalipwa Lumpsum watakayokubaliana na NEC.
==========================
Update: 29/06/2023
Prof. Assad: Sitapiga tena kura labda mfumo uwe wa kidigitali
Aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad amesema hatojisumbua tena kushiriki zoezi la kupiga kura. Amesema hayo kwa hoja ya kwamba Watanzania huwa wanashiriki kupiga kura lakini hawashiriki uchaguzi. Kwa maana ya kwamba kura haina maana katika uchaguzi. Aidha amesema...www.jamiiforums.com
===========================
Rais Samia afanya uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali kama ifuatavvo: Amemteua Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya...www.jamiiforums.com
Sio Yas pesa ni mixx by yasLabda useme Yas Pesa