Napendekeza mfumo wa ‘Randomizer’ kwenye usajili wa ‘plate number’ za magari nchini

Huoni kuna mikoa gari zisingezidi 10 kusajiliwa?
 
Yaan unataka tusiwavhuje wenye mikangafu na wenye vitu vipyaaa
 
Gari kuwa namba plate za usajili wa no mpya haimanishi kuwa gari hilo ni zima au, hiyo itategemeana , mfano Kuna magari yanauzwa kwa mnada wa serikali au mashirika na mengine yanakua yamechoka Sana . Sasa unapolinunua lazima ulisajili na usajili huo ni wa namba plate mpya.

Sent from my Redmi Note 6 Pro using JamiiForums mobile app
 
Good idea, ila pia namba ziwe ‘randomized’ , zisionyeshe mtiririko wa kujua ipi imesajiliwa zamani na ipi imesajiliwa recently.
 
mfumo wenyewe hujaweka bayana.
 
Hiyo watu hawajui, anaweza akanunua gari bovu akaacha zima kisa usajili wa namba ni mpya zaidi
 
Mkuu wazo lako ni too personal...

Kama haliingizii kipato taifa basi kwao hali make sense.
Watu wengi hununua gari toka Japan ili tu aweze kupata usajili mpya kwenye gari lake, na hivyo tunatumia pesa nyingi mno za kigeni kuagiza magari kama taifa, wakati huo huo kuna gari nyingi nchini zina hali nzuri kuliko hata hizo za kutoka japan (imefungwa engine mpya, gearbox mpya, matairi mapya, body halina accident damage, low mileage); ila linakosa soko kisa ni namba C, au B au D, ila kuna watu wanaagiza mikangafu toka Japan kisa tu itapata usajili mpya.

Hii itatoa fursa ya kuanzishwa kwa ‘Car restoration facilities’ ambazo zinalorudisha gari katika hali ya upya kama ilivyokuwa kiwandani, hata hao Japan ndivyo wanavofanya koasi wakituuzia mkangafu sisi tunaona kama jipya, hii itatengeneza ajira nyingi sana!!!!

Pia itaokoa fedha nyingi tunazotumia kuagiza magari toka Japan, maana mtu ataona anunue hapa hapa nchini restored car ambayo haitamwaibisha barabarani kwa kuwa na plate number ya zamani...
 


Nimependa idea ya car restoration facilities.
 
Nimependa idea ya car restoration facilities.
Hata kule Japan ndicho wanachofanya, gari inakuja huku utasema mpya; kinachokwamisha ‘Car restoration facilities Tz ni plate number, unatumia gharama kurestore gari halafu ukienda sokoni unaambiwa hiyo namba B chukua milini 2, inatukwamisha sana kama taifa na kuexport ajira kwenda Japan, maana gari za Japan tu ndio zinapewa usajili mpya, tunawatajirisha wao na kujifukarisha wenyewe
 
una zungumziaje katika kodi pia?
 
Nchi zilizoendelea hufanya hv hata South Africa

Ni wazo zuri sana hili lakini pia inakuwa rahisi kuyatambua magari katika mkoa husika.
 
una zungumziaje katika kodi pia?
Gari hata ikiuzwa ndani nchini, kuna pesa unalipa kabla huja-transfer ownership, kwahiyo bado kodi itapatikana, tutazalisha ajira za ndani kupitia ‘Car restoration facilities’ ambazo nazo zitalipa kodi, na kikibwa zaidi, pesa za kuagiza magari Japan tutazitumia kuagiza matrekta toka India ili kukuza uchumi wetu wa kilimo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…