Napendekeza Serikali ya Tanzania ichapishe Noti za Shilingi Elfu (50,000) na Laki moja (100,000)

Najaribu kuwaza tu kuwa dunia inaelea kwenye cashless, hili wazo lako bado litafaa miaka 20 ijayo? Pia nchi kama Zimbabwe wana noti kubwa, ina maanisha uchumi wao kuwa imara?
 
Mzunguko unaruhusu hilo? Yaani gap ya mzunguko wa malipo ya chini ukilinganisha na malipo ya juu. Una noti ya elfu hamsini umepanda dalalala, mzunguko unaruhusu mbadilishano wa huo muamala kiwepesi? Kuna maeneo chenji ya elfu kumi tu ni shughuli.
 
Kutokana na nyuzi za nyuma za mtoa mada, nadhani atakuwa ni mhandisi (engineer).
Kama ndivyo, atakuwa amedandia fani asiyoijua, Tena bila kufanya utafiti.

Mfano, wakati ule Zimbabwe ilipokuwa na inflation ya kutisha wali print noti ya trillion Mia moja !
Sasa linganisha hiyo na USA yenye uchumi mkubwa ambayo noti yake ya denomination kubwa zaidi ina sifuri mbili tu (yaani $100).

 
 
Unayajua madhara ya kufanya hivyo kiuchumi?,...usiombe itokee
 
Hawakuwa serious kabisa hawa 😄🍺
 
Ulichokuwa unazungumzia hapa ni tofauti kabisa na hoja nilizojenga. Tukiwa na noti ya elfu 50 (TSH 50,000) na laki moja (100,000 TSH), pengine si kila mtu ataweza kuishika kwa urahisi, itakuwa kama vile Dola za Marekani 100 (USD 100). Watu watakaoweza kumiliki noti hizo ni wale ambao vipato na miamala yao inaanzia elfu 50 na kuendelea. Kuhusu Zimbabwe, mfumuko wa bei uliwalazimu kuchapisha noti zenye thamani kubwa, kwani noti ndogo zilikuwa na thamani ndogo ikilinganishwa na bei za bidhaa sokoni. Hivyo Case ya Zimbwabwe haiwezi kuingizwa kwenye hii mada.
 
Haya ndio majibu ya kisomi sasa.
 
Ni matumaini yangu pendekezo hili litazingatiwa na Serikali ya Tanzania na Benki Kuu ya Tanzania kwa umakini na kufanyiwa tathmini ya kina.
Mimi nina swali tu, kwa yeyote mwenye ufahamu juu yake.
1. Je, inawezekana Tanzania, ikabadili fedha yake yenye thamani tofauti na hizi tunazotumia sasa?
Kwa mfano, iache kutumia shlingi, iamue kwa mfano mbovu kuiita hiyo pesa "madafu", ambayo itapangiwa thamani tofauti na hii tuliyonayo sasa hivi. Dafu moja kwa mfano liwe na thamani yenye mlingano wa hiyo Tsh100,000/ anayopendekeza mleta mada.
Dafu la juu kabisa, kwa mfano liwe 'madafu 100', ambayo ina thamani kubwa kulingana haya mapesa ya wakubwa wa dunia
Patakuwepo pia na pesa za sarafu; kwa mfano Dafu 1, Dafu 5 Dafu 10, n.k.

Lengo hapa ni kufanya kinyume na anachopendekeza mkuu 'Meneja Wa Makampuni.

Kwa kujitetea mbele ya safari, nitoe mfano mwingine: Shilingi ya Kenya, pamoja na kuporomoka kunakotokea kwa sasa, bado inayo thamani kubwa. Ksh 140, bado inakupatia dola moja ya kimarekani; hapa kwetu tunahitaji Tsh 2300/
Uchumi wa Kenya, pamoja na kuwa mkubwa (kidogo), kuliko wetu, hauna tofauti sana na sisi; kwa hiyo hatuwezi kutumia sababu ya uchumi hafifu kuwa sababu ya kuwa na pesa yenye thamani kubwa sokoni (hii ni kwa uelewa wangu mdogo nilio nao kwenye maswala haya. Lakini ukinifundisha ninao uwezo wa kujua ulichonieleza, kwani najua hakuna 'roketi sayansi hapa).

Mkuu 'Meneja', eti unasemaje wewe kuhusu hili.
 
Hakuna kitu kinachoboa kama kulazimika kutembea na mabulungutu ya fedha mpaka mfukoni hazienei

Just imagine ukiwa na laki tano tu za elfu kumi kumi wallet inajaa mpaka kutembea ni tabu sasa laki tano pekee ndio ya kukufanyia hivyo???

Tukirudi nyuma malipo ya kidijitali bado sio sawia hasa pembezoni mwa nchi na hivyo kupelekea kutembea na fedha taslimu kubaki kuwa suluhisho kuu kwa sasa

Mwisho kabisa dola 100 ukiicheji kwa madafu yetu ni sawa na laki 2 na ushee

Sio ubaya tukiwa na noti ya elfu 20 ama 50k kwani kwa usawa wa sasa pesa yetu ni ya madafu sana
 
Mkuu 'Covax', huitendei haki hiyo elimu yako unayodhani unayo kwa majibu kama haya uliyoweka hapa.
Nadiriki kusema wewe siyo msomi hata kidogo.
Lakini najua watu wengi hapa Tanzania wanaojiita wasomi wa aina yako ndio walioenea kila mahali.

Hakuna jambo la kutisha sana katika hayo uliyoyataja hapo kwa mikogo mingi, kiasi kwamba ni watu kama wewe tu, msioweza hata kuyaelezea kwa wengine ndio pekee yenu mlio na uwezo wa kuyafahamu.

Ninakusihi, chukua muda, andika makala mbalimbali za mambo hayo kwa lugha rahisi na zitume zichapishwe magazetini watu wazisome, na nyingine weka humu, tutakusoma na kukusifu kwa elimu yako uliyopata. Sote tutajivunia kuwa na waTanzania wasomi kama wewe.

Ni matumaini yangu kwamba utanielewa vizuri tu na siyo kwa kinyongo kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…