GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Baadhi ya wasomi wa Biblia na viongozi wa dini wameshauri kitengenezwe chombo kitakachofuatilia mienendo ya wahubiri na wachungaji pamoja na kuwapima afya ya akili kabla ya kuruhusiwa kuhubiri.
Ushauri huo umetolewa leo Alhamisi Novemba 14, 2024 kwenye kongamano la kiukemene kujadili imani moja na mafundisho sahihi kwa ustawi wa binadamu lililoandaliwa na Chuo cha Biblia cha Kilutheri Nyakato kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (Saut) vyote vya mkoani Mwanza.
Akitoa mada kwenye kongamano hilo, Mkuu wa Idara ya Falsafa na Maadili chuo cha Saut Mwanza, Padri Innocent Sanga amesema Biblia haina tena utamu wa kuhubiri na hata umisionari umepoteza ladha kwa sababu umeingiliwa na wanyang’anyi wanaotumia vifungu vyake kutapeli waumini wao.
“Tutengeneze chombo…Tunapaswa kuwapima wachungaji vichwa vyao, afya ya akili, kuna wengine ni wagonjwa, wanadanganya watu kumbe hapa kichwani pameshaharibika…miaka na miaka pameshaharibika,”amesema Padri Sanga.
Chanzo: mwananchi_official
Mimi nionavyo Wahubiri pamoja na Waumini wao wote kwa 100% wana Changamoto Kubwa sana tu ya Afya ya Akili.