Napinga fainali ya FA kufanyika Zanzibar, Kisoka Zanzibar ni Nchi nyingine wala haina timu kwenye michuano hiyo

Napinga fainali ya FA kufanyika Zanzibar, Kisoka Zanzibar ni Nchi nyingine wala haina timu kwenye michuano hiyo

Shida mijitu inajipendekeza mdogomdogo utasikia baadhi ya mechi za ligi kuu kupelekwa Zenji hapa wanatest tu ikikubali utasikia kikao cha TFF kimepitisha sheria ya ligi kuchezwa huko
Hatutakubali Asilani!
 
hebu acheni mambo yakipuuzi tukiwa namawazo kama yako kuja kupata umoja wakitaifa na kuinga Africa itakuja kuwa tabu sana!.

if the option failed to the mainland let it be Zanzibar!.
Muhimu kuzingatia kanuni. Kama unakumbuka kuna timu ilitaka kwenda Zanzibar TFF wakasema kanuni haziruhusu hii ni ligi ya bara.

Sasa haya mashindano ni ya Tanzania?

Haina shida kuweka kanuni za mashindano mbona ulaya nadhan spain walihamisha baadhi ya mechi kupigwa nje ya spain.
 
Umeangalia labda suala la Mapato ? Kama faranga ni nyinzi zaidi zitapatikana huko hata Mwezini watu watakwenda....
 
Muhimu kuzingatia kanuni. Kama unakumbuka kuna timu ilitaka kwenda Zanzibar TFF wakasema kanuni haziruhusu hii ni ligi ya bara.

Sasa haya mashindano ni ya Tanzania?

Haina shida kuweka kanuni za mashindano mbona ulaya nadhan spain walihamisha baadhi ya mechi kupigwa nje ya spain.
Umeniwahi mkuu nilitakuuliza hili, Watanganyika tunajipendekeza sana. Ivi ulishawahi kusikia fainali ya mapinduzi kuchezwa bara.
 
Kwa akili yako ndogo unadhani ni sahihi kwa ligi ya Tanganyika fainali kufanyika Zanzibar, au utuambie lini Uliona Kipanga na KMKM wakicheza Kwa Mkapa fainali ya Karume Cup?

acha kutia siasa kwenye mambo ya football
 

Kuipeleka fainali ya FA Zanzibar ni sawa na kuipeleka fainali hiyo Kenya, Somalia ama Uganda, hakuna timu yoyote kwenye Nchi ya Zanzibar inayosimamiwa na TFF kama zilivyo Nchi nilizozitaja

Wala hakuna sababu yoyote ile iwe ya kijinga au ya maana ya kupeleka fainali hiyo Zanzibar

Sisi wapenda soka wa Tanganyika tuliojiandaa kwenda viwanja vya Tanganyika kuangalia fainali hiyo hatutakubali na kuna mpango wa kwenda Mahakamani kuzuia jambo hilo haramu.

Rais wa TFF hana Mamlaka yoyote ile ya kuamua kuliendesha soka la Tanzania atakavyo yeye kwa sheria za mfukoni mwake

Ni kweli kwamba sisi ni Wajinga lakini siyo Wajinga kiasi hicho.

PIA SOMA
- Kwanini TFF mnaipeleka fainali Zanzibar?
Ni zile zile siasa za kinafiki tu, na hayo yote ni kutaka kupoza sumu aliyoitema Lisu juu ya muungano!! Subiria uone mabango yatakayokuwa uwanjani!!
 
Naona Ligi ya Tanganyika nayo wamehamishia Zanzibar
 
Back
Top Bottom