Napinga hoja ya kuwaombea wafu, maombi hayo hayafanyiwi kazi

Hello!

Naomba nieleweke wazi kuwa, mimi binafsi nalaani vikali kitendo cha kuua watu Kwa risasi za moto Kwa sababu za kijinga kwamba unalinda mali za unaowaua,ambapo ilikuwa inawezekana kuzuia hayo yasitokee Kwa kusikiliza hoja zao na kuzifanyia kazi.

Sasa twende kwenye mada, wafu hawaombewi, kuombea wafu ni ibada ya shetani Kwa sababu Mungu ni Mungu wa walio hai na si wa wafu, hivyo usiende kuombea wafu.

Ikitokea umehudhuria ibada hiyo, badili maombi, wewe omba mwenyezi Mungu airehemu Tanzania, asikie sauti ya damu iliyomwagika bila hatia na kulipa kisasi Kwa wahusika Kwa maana imeandikwa, auaye Kwa upanga, naye atauwawa Kwa huo.

Ikumbukwe pia kuwa kanisa Hilo Lina mtandao mpana wenye matawi mengi kuliko chama tawala hivyo maombi haya yatajibiwa haraka ikiwa wataomba Kwa usahihi.

Aamen
Ibrahimu ni mfu, Musa ni mfu, Isaka ni mfu?, Yakobo ni Mfu?, Daudi ni Mfu? Mtume Stefano ni Mfu? Bikira Maria ni Mfu? Naomba unijibu hili Swali ndipo tuendelee na mada.
 
Wote ni hai hao, sababu ni watakatifu wako mbinguni,

Ila hatuwaombei,

Na hatujaruhusiwi kuwaombea,wao ndio huombea na kuwatia moyo walio duniani
 
Hello!

Naomba nieleweke wazi kuwa, mimi binafsi nalaani vikali kitendo cha kuua watu Kwa risasi za moto Kwa sababu za kijinga kwamba unalinda mali za unaowaua,ambapo ilikuwa inawezekana kuzuia hayo yasitokee Kwa kusikiliza hoja zao na kuzifanyia kazi.

Sasa twende kwenye mada, wafu hawaombewi, kuombea wafu ni ibada ya shetani Kwa sababu Mungu ni Mungu wa walio hai na si wa wafu, hivyo usiende kuombea wafu.

Ikitokea umehudhuria ibada hiyo, badili maombi, wewe omba mwenyezi Mungu airehemu Tanzania, asikie sauti ya damu iliyomwagika bila hatia na kulipa kisasi Kwa wahusika Kwa maana imeandikwa, auaye Kwa upanga, naye atauwawa Kwa huo.

Ikumbukwe pia kuwa kanisa Hilo Lina mtandao mpana wenye matawi mengi kuliko chama tawala hivyo maombi haya yatajibiwa haraka ikiwa wataomba Kwa usahihi.

Aamen
Ni kweli, Biblia haina fundisho la kuombea marehemu waliokufa kwa risasi au namna yoyote.

Pamoja na hayo, ni kutukumbusha tu tukio chafu, baya na chungu la kuwaangamiza Watanganyika hata waliokuwa wamelala majumbani bila hatia na vitoto vichanga.
 
Back
Top Bottom