Ktk hili nakuunga mkono kwa %100 jukwaa la kiswahili tusitoke kwenye Lugha yetu adhimu
tukitoka wengi watakosa kuelimika kwa kile tunakiweka jukwaani !
wewe endelea kumjibu kwa kiswahili utaeleweka zaidi ✍️
Huyo mtu ni mpumbavu tu katika ligha yoyote.
Kwa sababu katika hoja hii, kabla ya Kiingereza nilimuandikia vizuri tu Kiswahili. Soma juu hapo.
Ujue watu wengine wana utapiamlo wa ubongo hata uwaeleweshe vipi, sio tu hawaelewi, hawataki kuelewa.
Kuna watu wanaweza kuwa na ujinga katika kitu fulani, halafu wepesi sana wa kujifunza kitu kipya ukiwafundisha, wana udadisi wa kuhoji kujua vitu vipya, wana adabu fulani inayokuja kutokana na udadisi huo, an intelligent humility.
Halafu kuna watu wana utapiamlo wa ubongo uliochanganyika na matatizo ya kisaikolojia ya miaka mingi kutoka walivyopigwapigwa ovyo na familia zao tangu walivyokiwa wadogo.
Wewe unaweza kuona unajadiliana na mtu kimangmtiki, kumbe mwenzako ana process trauma zake na social anxieties za miaka mingi.
Hakusikii wala kukuelewa katika lugha yoyote.
Anakuja kuoigana vita vya kidini Yesu hivi, Yesu vile, imani yangu mimi hivi, mpaka kwenye misa ya kuombea marehemu, jambo ambalo mtu yeyote mwenye ustaarabu mdogo tu anatakiwa ajue hapa naenda kuonesha heshima kwa waliofariki na kufariji wafiwa.
Mbona wakristo wanaingia misikitini na waislamu wanaingia makanisani kwenye hizi misa, ina maana wanapoingia hivyo wanakuwa wameacha imani zao na kuchukua imani tofauti?
Mpaka mimi Kiranga The Unorthodox nisiyeamini Mungu wala dini naelewa hilo.
Hjyu ana matatizo ya kisaikolojia inawezekana, halafu ukitaka kumueleza mambo kimantiki hataki kukuelewa, kwa lugha uoyote.
Lugha si tatizo hapa.