Napinga kwa nguvu zote baadhi ya member humu kuwaona walimu kama "special group"

Walimu mbona wana maisha standard nipo nao Apa Nachingwea Bar moja inaitwa Zurich naona wanajitutumua kula Safari lager.
Sijui wamebahatisha wapi posho
 
Umenena vyema mkuu. Kuna watu Kwa dharau tu wanalala na kuamka na wazo lao juu ya walimu. Tuheshimiane aise
 
Walimu ni watu muhimu sana, sema wameamua kutumika Kwa maslahi ya watawala
 
Kwanza idadi yao ni kubwa kuliko kada nyingine zote alafu pia imeshajengeka mentality ya kuwa wale watu walioshindwa kimasomo (ufaulu mdogo) ndo huenda kwenye hiyo kada alafu pia ni kada inayoongoza Kwa maslahi kiduchu lakini pamoja na yote wanatumika mno na serikali hii inawafanya waonekane kama vile ni cheap labour
List ni ndefu but why walimu?

Mbona sector ya ulinzi na usalama haidharauliwi unaweza ukaleta hoja
 
Ungesoma vizuri hoja zangu sijui kama ungerudia kuandika haya

Hebu niambie afsa maendeleo mwenye diploma analipwa shingapi?

Je hakuna mtendaji mwenye certificate (ufaulu mdogo)?
 
Unalinganisha vitu visivyofanana hata kidogo. Uwekezaji na risk za coaster ni sawa na degree?
Je, kwenye hiyo coaster kwa mwezi unapata net profit kiasi gani?
N.B usije ukachanganya pato na faida.
aise nilishangaa kusikia daktari analipwa 900k. pesa ambayo naingiza kwa coaster special hire moja ndani ya siku 3.

sio mwalimu sio daktari kwa mishara ya Tanzania mtu smart kichwani unaona ni upuuzi
i
 
Walipoanza kuchukua vilaza tu kwenda kuwa walimu hasa shule za msingi waliharibu kila kitu
Hivi unajua asaivi mtoto wako akipata four au three ya mwisho anapelekwa wapi?

Swali ni why walimu pekee ndio huonekana vilaza wakati kada nyingi tu wanachukua certificate na diploma kwa waliomaliza form four?
 
Hakuna kada inayotumika nchi hii zaidi ya kada ya ulinzi na usalama hivyo hoja yako inakosa mashiko

Kwanini jeshi la police hawadharauliwi?

Unajua mshahara wa afisa maendeleo au mtendaji mwenye diploma ni shingapi? Mbona hadharauliwi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…