Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sawa mwalimu,somesha watoto wako wote ualimu,mnyororo wa umaskini utakuwa nawe daima, nakutakia umaskini mwema aminaKuna harakati nimezikuta toka najiunga jamii forum na bado zinaendelea kwa baadhi ya member kuwadharau na kuwakejeli walimu wa nchi hii
Napinga kwa nguvu zote za kuwafanya walimu kama marginal group kwa kigezo cha mshahara na maisha kiujumla
Nakataa unyanyasaji huu wa kifikra kwa walimu eti kisa some of them walienda kwa olevel certificate
Hata kama imefika wakati walimu wakawa wengi mtaani kwa sababu ya kimfumo bado haiwafanyi walimu wadharauliwe kwani kada nyingi bado zinasota kwenye suala la ajira
Nchi hii hakuna mwenye afadhali tukija suala la maslahi hasa walio halmashauri na tukija kwenye mishahara bado utakuta mfumo unaotumika kulipa watumishi ni kulingana na kiwango chao cha elimu kwa kada zote
Kuhusu hali ya kimaisha ngazi ya halmashauri wote ni wagaa gaa na upwa wanakula wali bila mchuzi dharau zinatoka wapi?
Tukija superiority ya kada michepuo ya kada zingine na ualimu mtiririko ni uleule either mtu aende olevel certificate, advance certificate au chuo moja kwa moja
Kwanini walimu wadharauliwe? Kwanini tuwakejeli? Nchi hii tunategemeana hii ni ecosystem bila mwalimu bila dactari na kada zingine hakuna mtiririko wa uendeshaji nchi tuheshimiane
We nawe mnazi mnazi hivi. Utajiri na umasikini tofauti yake nini. Je ambao sio walimu wote ni matajiri?Ukitaka ujichimbie kaburi la umasikini kuwa mwalimu.
Swali zuri sana....We nawe mnazi mnazi hivi. Utajiri na umasikini tofauti yake nini. Je ambao sio walimu wote ni matajiri?
Una akili sana.Kazi zote huwa ziko hivi,ama ikupe fedha nyingi lakini itakunyima muda wa kupumuzika,au ikupe fedha za kawaida tu,lakini itakupa pia muda wa ziada wa kupumuzika.Ukiwa unakasirika na kila maoni yanayotolewa humu JF utawehuka bure... Hili ni jukwaa la fikra huru, humu kuna kila aina ya watu...
Kimsingi maoni yote yana mantiki ukiona kilichoandikwa na mwenzako hukielewi maana yake hujakomaa kifikra...
Sasa unakuta kuna Mwl anapokea million 1 kwa mwezi halafu kuna mimi nipo private sector napokea laki3 ila kilasiku nawatukana walimu humu, unadhan nani mgonjwa wa akili?
Walimu wanatucheka sana tunavyo waona cheap, nilichogundua Mwl anapokea mshahara ila kwa siku anafanya kazi masaa yasiyozidi 4, hapo kama akiwa ana vipindi kama hana wengi hawaendi kazini wanafanya mambo yao binafsi...🙄
WaTz wengi tuna kufa mapema kwasababu ya chuki wivu makasiriko husda vinyongo na roho mbaya...
Wana ahueni hawali mihogo asubuhi kama kifungua kinywa wala kula ugali wa wanafunzi.We nawe mnazi mnazi hivi. Utajiri na umasikini tofauti yake nini. Je ambao sio walimu wote ni matajiri?