Napinga kwa nguvu zote baadhi ya member humu kuwaona walimu kama "special group"

Sawa mwalimu,somesha watoto wako wote ualimu,mnyororo wa umaskini utakuwa nawe daima, nakutakia umaskini mwema amina
 
Kwani moderators wa JF uwa wanafurahia mada za kila siku za kuwakejeli walimu ndiyo maana uwa hawazifuti? Wenyewe wakiguswa kidogo tu wanafutilia mbali nyuzi zake muda huo huo.
 
Una akili sana.Kazi zote huwa ziko hivi,ama ikupe fedha nyingi lakini itakunyima muda wa kupumuzika,au ikupe fedha za kawaida tu,lakini itakupa pia muda wa ziada wa kupumuzika.
Think about this.Mwalimu ana muda mwimgi wakutokuwepo kazini(wanafunzi wakifunga).Pia muda wake wakuwa kazini ni mfupi.Mwalimu mwenye akili ataugeuza muda wote huo wa kuwa huru kuwa fedha.Advantage nyingine ni kuwa ni rahisi kwa mwalimu kupanda madaraja kiutumishi na kufikia kiwango cha juu cha mshahara,kuliko kada zingine.
Walimu wenye akili wameshaona hiyo fursa ya muda mwingi wa ziada,na sasa wanatafuta tu pesa.Off course hawakosi walimu wasioona fursa waliyonayo,kama ilivyo kwenye kada zingine pia.Sio wafanyakazi wote wa TRA kwa mfano wana maisha mazuri.Wengine wanaishi kawaida tu.
WALIMU POPOTE MLIPO,MSIFADHAISHWE NA KEJELI ZA WATU HUMU.WENGI WAO WANAOWAKEJELI HAWANA HATA NUSU YA MAISHA MNAYOISHI.


KWA MEMBERS WENGINE HUMU,UJUMBE WANGU KWENU NI KUWA,NI MTU MPUMBAVU TU ANAWEZA KUKEJELI KAZI YA UALIMU,PAMOJA NA WALIMU WETU.KEJELI ZOZOTE KWA WALIMU ZINAONYESHA JINSI GANI HAUJITAMBUI NA ULIVYO LIMBUKENI TU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…