Napinga Ramadhani Kailima kuteuliwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, ni Kada wa CCM

Nakuhakikishia kwamba Kailima hatofanya kazi NEC hadi anang'olewa
Ukimya uliopo CHADEMA kuhusu haya yanayoshuhudiwa wakati huu unanipa tafsiri moja katika ya hizi mbili:

Kwamba wanaelewa kinachoendelea na wao wanajiandaa kimya kimya na mipango yao kuyakabili kwa wakati mahsusi; au kwamba wanayaona na hayawapendezi, lakini hawajui lipi la kufanya, kwa hiyo pengine ni bora kuyanyamazia na kuendelea na mipango ya ahadi zinazotokana na maridhiano.

Kama ni hilo la pili, historia ya nchi hii itawahukumu kuwa matapeli na wahujumu wa nchi ambao hawajawahi kutokea tokea nchi ipate uhuru wake.

Nisome vyema unielewe vizuri, na usije ukabadili sura huko mbele ya safari.
 
Tumieni njia za halali kuingia ikulu. Msihalalishe njia ovu kuonekana nzuri ili mradi tu muingie Ikulu
 
Inakuwaje anachaguliwa mtu duni hivi kwenye ulimwengu wa demorasia?
 
Mkuu hata mimi nashangaa hao mabakax2, nao wanaowwlaogopa wana siasa wa CCM vibaya. Na nadhani wanafumbwa macho na upendeleo wa msosi na hiyo mikopo wanayopewa. Ile siku Magufuli alipokea wanaccm kwenye hafla ya jeshi huko Arusha ndio nilijua hamna watu hapo.
 
Tumieni njia za halali kuingia ikulu. Msihalalishe njia ovu kuonekana nzuri ili mradi tu muingie Ikulu

Njia za halali ndio hizi mnazinajisi, kila muda unavyosonga ndio box la kura mnalivyochezea, lazima machafuko yatokee ndio mtatoka madarakani.
 
Njia za halali ndio hizi mnazinajisi, kila muda unavyosonga ndio box la kura mnalivyochezea, lazima machafuko yatokee ndio mtatoka madarakani.
Chadema hairuhusiwi kushinda uchaguzi iwe kwa njia halali au haramu. Ukweli mchungu uchukue huo

Hakuna mwenye akili timamu ataruhusu chadema ishinde
 
I agree with you. Sasa tumpe nani? Tick 1 (zingatia gender na pande 2 za Miungano):

A: FATMAKARUME
B: ASKOFUBAGONZA
C: MARIATSEHAYI
D: PROF LWAITAMA

Majibu yatumwe kwa Dr Mahera Charles, Dodoma
 
Nafikiri afikishwe MAHAKAMANI
 
Tumieni njia za halali kuingia ikulu. Msihalalishe njia ovu kuonekana nzuri ili mradi tu muingie Ikulu
Hivi CCM wanatumia "njia za halali" kuendelea kuwepo ikulu?

Utahimiza vipi upande mmoja utumie halali, na kushangilia upande unaotumia haramu ukiwa mtu mwenye fikra nzuri?
 
Chadema hairuhusiwi kushinda uchaguzi iwe kwa njia halali au haramu. Ukweli mchungu uchukue huo

Hakuna mwenye akili timamu ataruhusu chadema ishinde
Nothing lasts longer
 
Nadhani ametegwa ili adakwe
Kuna mambo badala ya kusikitika inalazimu tu kucheka ukiyawaza vizuri.

Hivi Samia anapofanya teuzi kama hizi wakati huu, akilini mwake anajihisi vipi?

Nchi anayoiongoza anaiona ikiwa yenye raha na mafanikio ya uteuzi wa namna hii?

Au basi tuseme kashauriwa afanye hivi kwa maksudi ili kuonyesha nguvu alizo nazo endapo kama uteuzi wake utapingwa? Kama ni hivyo, hizi hadithi za "maelewano na maridhiano" ni za nini?

Lakini haishangazi kwa tabia za huyu mama aliyewahi kusema mbele za watu wenye akili kwamba "Mbowe ni gaidi kweli, kwa sababu hata wenzake alioshirikiana nao kwenye uharifu huo tayari wanatumikia vifungo vyao magerezani!"
Na baadae kuja kusahau yote hayo na kufuta kesi nzima.

Huyu atakuwa analo tatizo kichwani; hata kama ni tofauti na matendo ya yule aliye mrithi.
 
Hivi CCM wanatumia "njia za halali" kuendelea kuwepo ikulu?

Utahimiza vipi upande mmoja utumie halali, na kushangilia upande unaotumia haramu ukiwa mtu mwenye fikra nzuri?
CCM huwa inashinda kihalali. Wale watu wanaodharaulika na CHADEMA ndo huipigia kura CCM. Upinzani unawathamini vijana wa twitter na kuwadharau watu wengine. Kwa mfano yule mzee kule Mara aliyedhalilishwa na mdogo wake Heche kisa kavaa shati la CCM unadhani ataipigia kura CHADEMA? Vijana wa Bajaj Sumbawanga waliodhulumiwa malipo yao wataipigia kura CHADEMA?
 
Mimi nilidhani unatofauti na baadhi ya watu humu ambao michango yao kila mara inajulikana kuwa ya hovyo, kumbe ni kundi lilelile?

Basi, imetosha kujibishana na wewe.
 
Noma sana
 
Mimi nilidhani unatofauti na baadhi ya watu humu ambao michango yao kila mara inajulikana kuwa ya hovyo, kumbe ni kundi lilelile?

Basi, imetosha kujibishana na wewe.
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Nchi yetu Ina mambo ya hovyo sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…