Napinga Ramadhani Kailima kuteuliwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, ni Kada wa CCM

Nakuhakikishia kwamba Kailima hatofanya kazi NEC hadi anang'olewa
Ukimya uliopo CHADEMA kuhusu haya yanayoshuhudiwa wakati huu unanipa tafsiri moja katika ya hizi mbili:

Kwamba wanaelewa kinachoendelea na wao wanajiandaa kimya kimya na mipango yao kuyakabili kwa wakati mahsusi; au kwamba wanayaona na hayawapendezi, lakini hawajui lipi la kufanya, kwa hiyo pengine ni bora kuyanyamazia na kuendelea na mipango ya ahadi zinazotokana na maridhiano.

Kama ni hilo la pili, historia ya nchi hii itawahukumu kuwa matapeli na wahujumu wa nchi ambao hawajawahi kutokea tokea nchi ipate uhuru wake.

Nisome vyema unielewe vizuri, na usije ukabadili sura huko mbele ya safari.
 
Najua kwa uwezo wako ulionao, hapa unajisikia kuwa umetoa hoja nzito na mhimu sana ambayo haina mbadala wa jibu juu yake. Hiyo ndiyo ngazi ya juu uliyofikia katika fikra zako.

CCM wapo madarakani miaka yote, utawafananisha vipi na CHADEMA wanaotafuta kila aina ya mbinu kuwaondoa hawa wanaohodhi, tena kwa mabavu kubaki madarakani, kama huoni upungufu wa fikra zako?

Ngoja nikuache na hilo, lakini nina mashaka kama utakuwa na uwezo wa kuelewa kinacholengwa hapa.
Tumieni njia za halali kuingia ikulu. Msihalalishe njia ovu kuonekana nzuri ili mradi tu muingie Ikulu
 
Inakuwaje anachaguliwa mtu duni hivi kwenye ulimwengu wa demorasia?
 
Wakati umefika kuwauliza mabaka mabaka, hivi haya hayawahusu? Maumivu ya wajomba na shangazi zao wanaona ni mziki wa bongo Flava? Yaani hizo free ration za mchele na cooking oil zinawafanya wanajisahau kiasi cha kuona ukweli?
Jee hakuna wenye fikra na maamuzi ya vijana kama Thomas Sankara au Jerry Rawlings wa wakati ule kule West Africa?

Tunajua hata kwetu walikuwepo kina Hans Poppe, McGhee, Kamando, Lt Maganga, Col Msami, na wengineo. Lakini hawakuleta mabadiliko waliyokusudia ila early 80 walisababisha displin ya aina fulani.

Hatusemi wafanye coup bali na wao waonyeshe wanakwazika na yanayo endelea, hizi yes sir yes sir watakuta familia zao zimesha kwa kifafaduro na kipindupindu kwa umasikini.

Au siku hizi wamekwisha wanaojitafakari huko waliko?

Mkuu hata mimi nashangaa hao mabakax2, nao wanaowwlaogopa wana siasa wa CCM vibaya. Na nadhani wanafumbwa macho na upendeleo wa msosi na hiyo mikopo wanayopewa. Ile siku Magufuli alipokea wanaccm kwenye hafla ya jeshi huko Arusha ndio nilijua hamna watu hapo.
 
Tumieni njia za halali kuingia ikulu. Msihalalishe njia ovu kuonekana nzuri ili mradi tu muingie Ikulu

Njia za halali ndio hizi mnazinajisi, kila muda unavyosonga ndio box la kura mnalivyochezea, lazima machafuko yatokee ndio mtatoka madarakani.
 
Chadema hairuhusiwi kushinda uchaguzi iwe kwa njia halali au haramu. Ukweli mchungu uchukue huo

Hakuna mwenye akili timamu ataruhusu chadema ishinde
 
Kurejeshwa kwa Kailima kuwa Mkurugenzi wa NEC akichukua nafasi ya Dr. Mahera, ni sawa na kejeli na dharau kubwa sana kwa Watanzania, Jambo hili ni sawa na matusi ya nguoni kwa Watanzania.

Huyu ni miongoni mwa Makada wakubwa kabisa wa CCM wa tangu enzi na enzi.

Ushahidi huu hapa akiwa na Mwigulu enzi zao UVCCM.

View attachment 2530740

Wakati Kagulumujuli akihujumu uchaguzi wa Kinondoni na kusababisha mauaji ya Akwilina , Kailima alikuwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi na akanyamaza , Kailima alihusika na kukamatwa kwa Salum Mwalimu aliyekuwa Mgombea wa Chadema kwenye vituo vya kupigia kura Magomeni akishirikiana na RC wa DSM wakati huo Paulo Makonda , Mtu kama huyu awezaje kuaminiwa na kurejeshwa tena Tume ya uchaguzi , kwa uteuzi huu Rais Samia ana malengo gani na Demokrasia ya Tanzania ?

Hata kama Watanzania ni Wajinga lakini si wajinga kwa kiwango ambacho mamlaka ya uteuzi inawaona , ni nani aliyesahau madudu ya Kailima hapo Tume ya Uchaguzi ?

Hakika kwa Uteuzi huu ninaamini Mungu hawezi kukubali na ATATENDA JAMBO , haliwezi kwisha hivi hivi tu .
I agree with you. Sasa tumpe nani? Tick 1 (zingatia gender na pande 2 za Miungano):

A: FATMAKARUME
B: ASKOFUBAGONZA
C: MARIATSEHAYI
D: PROF LWAITAMA

Majibu yatumwe kwa Dr Mahera Charles, Dodoma
 
Kurejeshwa kwa Kailima kuwa Mkurugenzi wa NEC akichukua nafasi ya Dr. Mahera, ni sawa na kejeli na dharau kubwa sana kwa Watanzania, Jambo hili ni sawa na matusi ya nguoni kwa Watanzania.

Huyu ni miongoni mwa Makada wakubwa kabisa wa CCM wa tangu enzi na enzi.

Ushahidi huu hapa akiwa na Mwigulu enzi zao UVCCM.

View attachment 2530740

Wakati Kagulumujuli akihujumu uchaguzi wa Kinondoni na kusababisha mauaji ya Akwilina , Kailima alikuwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi na akanyamaza , Kailima alihusika na kukamatwa kwa Salum Mwalimu aliyekuwa Mgombea wa Chadema kwenye vituo vya kupigia kura Magomeni akishirikiana na RC wa DSM wakati huo Paulo Makonda , Mtu kama huyu awezaje kuaminiwa na kurejeshwa tena Tume ya uchaguzi , kwa uteuzi huu Rais Samia ana malengo gani na Demokrasia ya Tanzania ?

Hata kama Watanzania ni Wajinga lakini si wajinga kwa kiwango ambacho mamlaka ya uteuzi inawaona , ni nani aliyesahau madudu ya Kailima hapo Tume ya Uchaguzi ?

Hakika kwa Uteuzi huu ninaamini Mungu hawezi kukubali na ATATENDA JAMBO , haliwezi kwisha hivi hivi tu .
Nafikiri afikishwe MAHAKAMANI
 
Tumieni njia za halali kuingia ikulu. Msihalalishe njia ovu kuonekana nzuri ili mradi tu muingie Ikulu
Hivi CCM wanatumia "njia za halali" kuendelea kuwepo ikulu?

Utahimiza vipi upande mmoja utumie halali, na kushangilia upande unaotumia haramu ukiwa mtu mwenye fikra nzuri?
 
Nadhani ametegwa ili adakwe
Kuna mambo badala ya kusikitika inalazimu tu kucheka ukiyawaza vizuri.

Hivi Samia anapofanya teuzi kama hizi wakati huu, akilini mwake anajihisi vipi?

Nchi anayoiongoza anaiona ikiwa yenye raha na mafanikio ya uteuzi wa namna hii?

Au basi tuseme kashauriwa afanye hivi kwa maksudi ili kuonyesha nguvu alizo nazo endapo kama uteuzi wake utapingwa? Kama ni hivyo, hizi hadithi za "maelewano na maridhiano" ni za nini?

Lakini haishangazi kwa tabia za huyu mama aliyewahi kusema mbele za watu wenye akili kwamba "Mbowe ni gaidi kweli, kwa sababu hata wenzake alioshirikiana nao kwenye uharifu huo tayari wanatumikia vifungo vyao magerezani!"
Na baadae kuja kusahau yote hayo na kufuta kesi nzima.

Huyu atakuwa analo tatizo kichwani; hata kama ni tofauti na matendo ya yule aliye mrithi.
 
Hivi CCM wanatumia "njia za halali" kuendelea kuwepo ikulu?

Utahimiza vipi upande mmoja utumie halali, na kushangilia upande unaotumia haramu ukiwa mtu mwenye fikra nzuri?
CCM huwa inashinda kihalali. Wale watu wanaodharaulika na CHADEMA ndo huipigia kura CCM. Upinzani unawathamini vijana wa twitter na kuwadharau watu wengine. Kwa mfano yule mzee kule Mara aliyedhalilishwa na mdogo wake Heche kisa kavaa shati la CCM unadhani ataipigia kura CHADEMA? Vijana wa Bajaj Sumbawanga waliodhulumiwa malipo yao wataipigia kura CHADEMA?
 
Mimi nilidhani unatofauti na baadhi ya watu humu ambao michango yao kila mara inajulikana kuwa ya hovyo, kumbe ni kundi lilelile?

Basi, imetosha kujibishana na wewe.
 
Marehemu AKWILINA Mungu Akupe Pumziko STAHIKI Damu yako haitamwagika hivi hivi NAO watakufuata tu kama sio Wao hata VIZAZI VYAO huyu mzee alikuwa Mkurugenzi wa Manispaa Kinondoni ndie aliyezuia barua za Mawakala wa Chadema na kusababisha Maandamano yakiyopelekea Kupigwa risasi AKWILINAView attachment 2530807
Noma sana
 
Mimi nilidhani unatofauti na baadhi ya watu humu ambao michango yao kila mara inajulikana kuwa ya hovyo, kumbe ni kundi lilelile?

Basi, imetosha kujibishana na wewe.
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Kurejeshwa kwa Kailima kuwa Mkurugenzi wa NEC akichukua nafasi ya Dr. Mahera, ni sawa na kejeli na dharau kubwa sana kwa Watanzania, Jambo hili ni sawa na matusi ya nguoni kwa Watanzania.

Huyu ni miongoni mwa Makada wakubwa kabisa wa CCM wa tangu enzi na enzi.

Ushahidi huu hapa akiwa na Mwigulu enzi zao UVCCM.

View attachment 2530740

Wakati Kagulumujuli akihujumu uchaguzi wa Kinondoni na kusababisha mauaji ya Akwilina , Kailima alikuwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi na akanyamaza , Kailima alihusika na kukamatwa kwa Salum Mwalimu aliyekuwa Mgombea wa Chadema kwenye vituo vya kupigia kura Magomeni akishirikiana na RC wa DSM wakati huo Paulo Makonda , Mtu kama huyu awezaje kuaminiwa na kurejeshwa tena Tume ya uchaguzi , kwa uteuzi huu Rais Samia ana malengo gani na Demokrasia ya Tanzania ?

Hata kama Watanzania ni Wajinga lakini si wajinga kwa kiwango ambacho mamlaka ya uteuzi inawaona , ni nani aliyesahau madudu ya Kailima hapo Tume ya Uchaguzi ?

Hakika kwa Uteuzi huu ninaamini Mungu hawezi kukubali na ATATENDA JAMBO , haliwezi kwisha hivi hivi tu .
Nchi yetu Ina mambo ya hovyo sana
 
Back
Top Bottom