Napitia changamoto kubwa, mke wangu anachanganyikiwa!

Napitia changamoto kubwa, mke wangu anachanganyikiwa!

Kwanini wafrika tunapenda waza waswala ya Imani imani(Dini au waganga) wakati hilo swala liko wazi ni matatizo ya akili .

Huo muda anahangaika na wachungaji ambao hawatamsaidia kitu angetakiwa ahangaike na hospitali za akili aweze tatuliwa changamoto yake.

Tatizo mtu anakuwa na tatizo la akili(ukichaa) hatupendi kukubali tunaamini linatibika tuu kawaida kumbe hapana.

Mtu akiambiwa mpeleke mgonjwa MIREMBE anahisi kama anamdhalilisha mgonjwa kumbe ndo sehemu sahihi.
Yaani ni yule mtu mnaweza kushinda naye vizuri tu,lakini anachokiwaza yeye anachukulia kama ni kweli umekifanya na ndipo anapoanza kuongea au kulalamika kwa sauti
 
Chanzo cha tatizo kinaweza kuwa nini?
Mimi nahisi ni ubongo tu hauko vizuri,sababu haya yanaambatana na kupoteza kumbukumbu maana kunawakati anaweza kupasahau hata nyumbani tunapoishi,niliwahi kumpeleka Mloganzira wakaseme kuna mishipa ya umeme kwenye ubongo imeachia nazani watalamu watakuwa wanajua vizuri
 
Kuna mengi,,,, kipato chako kimepungua au kiko vile vile ? Upendo wako kwake upoje ? Pengine ushamzoea unamchukulia wa kawaida ,,,,
Kipato kipo vizuri tu,ila inaitaji moyo sana,mfano anaweza kukuchenjia ndani ya basi akakunyan'ganya simu kukutuhumu unachati na wanawake na likawa zogo kubwa, au mko nyumbani ukachelewa kurudi sababu ya mihangaiko akaanzisha zogo,kuna wakati kama binadamu huwa najikuta nashindwa kuvumilia,
 
Kipato kipo vizuri tu,ila inaitaji moyo sana,mfano anaweza kukuchenjia ndani ya basi akakunyan'ganya simu kukutuhumu unachati na wanawake na likawa zogo kubwa, au mko nyumbani ukachelewa kurudi sababu ya mihangaiko akaanzisha zogo,kuna wakati kama binadamu huwa najikuta nashindwa kuvumilia,
Nendeni kwa viongozi wenu wa imani muwashirikishe,,, pia jitahidi kumuongoza awe karibu sana na anakoabudu !
 
Mpe upendo mwenzio. Utamuumiza sana ukimuacha. Huyo anakupenda ila anahitaji msaada wa kisaikolojia. Msaidie mwenzio,

be a man and hold that inconveniences with dignity and patience as a man, don't be like a boy to run away from disturbances
Nampenda kwa kweli na huwa namuonyesha upendo wa hari ya juu sana,kumnunulia zawadi kumtoa out na vitu vingi ili kumpunguza mawazo,sababu naamini anayopitia hata mimi siku moja ninaweza kuja kuyapitia endapo nitamtendea vibaya basi na mimi nitakuja tendewa vibaya
 
Kama unaniruhusu naomba kufahamu, je wewe na mwenza wako mna imani ipi ya kidini?
Kwa kweli mimi ni Muisilamu lakini kutokana na shida yake nimefika mpaka kwa Mwamposa kwenye maombezi,kuna kipindi baada ya kuombewa alitulia kabisa na hata nilivyokuwa namsimulia aliyokuwa ananifanyia akawa anasikitika sana lakini baada ya mda hari ikarudi tena
 
Back
Top Bottom