Napitia changamoto kubwa, mke wangu anachanganyikiwa!

Napitia changamoto kubwa, mke wangu anachanganyikiwa!

Mpe upendo mwenzio. Utamuumiza sana ukimuacha. Huyo anakupenda ila anahitaji msaada wa kisaikolojia. Msaidie mwenzio,

be a man and hold that inconveniences with dignity and patience as a man, don't be like a boy to run away from disturbances
Swali la kujiuliza ni kwamba if the roles were reversed huyo mwanamke angemvumilia mshikaji?
 
Kuwa makini hiyo hali isije kuhamia kwako, ikiwa ni adui anafanya hivyo, chunguza mapema, ujue chanzo cha tatizo ni nini.

Ikiwa ametupiwa pepo, fanya uchunguzi ujue chanzo ni nini.
Hakuna atakayeishi milele usiogope mambo ya dunia hata kama kuna mtu anakutesa hawezi kukutesa kwa miaka mia,naye hawezi kuishi miaka mia
 
Kwa kifupi sana ndoa yako imekumbwa na pepo la mafarakano.

Pepo hili hufanya kazi kwa kuangalia line of weakness kwa mmoja wa wanandoa na linaingia hapo. In this case mkeo amekuwa weak spiritual na limetua hapo.

Mwenye nafasi ya kuokoa hii ndoa na kumsaidia mkeo ni wewe mwenyewe. Sikushauri habari za kwenda kuombewa, rather nakushauri uombe mwenyewe. Kuna tofauti kubwa kwenye kuombewa na kuomba mwenyewe.
 
Yaani inasikitisha na inahitaji uvumilivu,Tumeowana kama miaka 20 iliyopita tuna mtoto mmoja na mmoja alifariki.

Kama miaka 4 iliyopita hivi ndivyo mwenzangu alipoanza kupitia changamoto za kuchanganyikiwa, anaweza akaazisha zogo bila sababu kunituhumu namroga au mimi malaya,kila mtu kwake ni mchawi,yaani yeye ni mtu wa kulalamika tu, tuachane nimpe taraka na mambo chungu nzima
Anaweza anzisha zogo sehemu yoyote ile iwe kwenye gari sokoni au sehemu yoyote ile
Kwa kweli inahitaji moyo ukitegemea wakati namuowa alikuwa vizuri tu
Kaka apa unaibiwa hivyo anajaribu kujikinga kwa kuiuwekea tuhuma ili usielewe chochote kumuhusu izi mmbo zishapitwa na wakati
 
Kwa kifupi sana ndoa yako imekumbwa na pepo la mafarakano.

Pepo hili hufanya kazi kwa kuangalia line of weakness kwa mmoja wa wanandoa na linaingia hapo. In this case mkeo amekuwa weak spiritual na limetua hapo.

Mwenye nafasi ya kuokoa hii ndoa na kumsaidia mkeo ni wewe mwenyewe. Sikushauri habari za kwenda kuombewa, rather nakushauri uombe mwenyewe. Kuna tofauti kubwa kwenye kuombewa na kuomba mwenyewe.
Asante. Post #45 nimeongea kidogo kuhusu habari za kuombewa.

Kwa kifupi kama nilivyosema kinacholeta hizo fujo sio mkeo, ni pepo la mafarakanao limemvaa. Ndo maana alikuwa anashangaa maana sio yeye. Kuna point of weakness kwake.

Sasa kwa nini nimeshauri usiegemee kwenye kuombewa badala yake ujenge tabia ya kuomba mwenyewe? Pamoja na kwamba wewe ni muislam naomba usome upate mwanga halafu mwishoni ukuwa na uelewa)

Maandiko matakatifu yanasema hivi;
Luka 11:24-26
[24]Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema, [25]Nitairudia nyumba yangu niliyotoka. [26]Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza.

Hapo aplipoandikwa kuwa atarudi kwenye nyumba aliyotoka, ni kwa mtu aliyekuwepo mwanzo.

Sasa basi, ukienda kuombewa tu na kiongozi wa dini bila wewe kushiriki, ni kweli pepo linatoka. Lakini kutoka huku linaenda huko likivizia mwenendo wa huyo mtu liliyemuacha. Liliona kasimama kwenye maombi, haliwezi kurudi lakini lilikuta mtu amestarehe, linaenda kuchukua wengine wengi tena wenye nguvu zaidi wanakuja. Ndio hapo unaona mtu anaharibika kuliko mwanzo maana mwanzoni lilikuwepo moja au machache na sasa ni mengi, yenye nguvu tena makali zaidi.

Sasa ndio maana mkeo sa hizi anaonekana kuwa worse kuliko awali maana yamemvaa mapepo mengi makali na yenye nguvu.

Sasa kwa kuwa wewe ni muislam, tafuta msaada kwa viongozi wako wa kidini wakushauri kwa dini yako situation kama hii suluhisho lake likoje.

Angalizo, usiende kwa waganga, maana kule kwa waganga na mapepo wote ni watoto wa baba mmoja, shetani. Wanatofautiana tu jinsi wanavyofanya kazi lakini wana boss mmoja. So mtu hawezi kumfukuza ndugu yake, atakudanganya tu au watafanya maelewano ambayo yatakugharimu wewe maana ndiye utakayelipia gharama za hayo maridhiano.
 
Mimi nahisi ni ubongo tu hauko vizuri,sababu haya yanaambatana na kupoteza kumbukumbu maana kunawakati anaweza kupasahau hata nyumbani tunapoishi,niliwahi kumpeleka Mloganzira wakaseme kuna mishipa ya umeme kwenye ubongo imeachia nazani watalamu watakuwa wanajua vizuri

mpeleke MOI pale muhimbili , nenda kakutane na madaktari wa ubongo na mifumo ya fahamu, Dr rutabasigwa, Dr lemeli na wengineo.

hao watu watakupa solution baada ya kuucheki ubongo wake kwa vipimo vya kisasa
 
Kwanini wafrika tunapenda waza waswala ya Imani imani(Dini au waganga) wakati hilo swala liko wazi ni matatizo ya akili .

Huo muda anahangaika na wachungaji ambao hawatamsaidia kitu angetakiwa ahangaike na hospitali za akili aweze tatuliwa changamoto yake.

Tatizo mtu anakuwa na tatizo la akili(ukichaa) hatupendi kukubali tunaamini linatibika tuu kawaida kumbe hapana.

Mtu akiambiwa mpeleke mgonjwa MIREMBE anahisi kama anamdhalilisha mgonjwa kumbe ndo sehemu sahihi.
Kwani akili ni nini?

Na ubongo ni nini?

Nini kimevurugwq hapo?
 
Huu uzi kuna namna mods wasaidie kuuweka vizuri na kupin 📌. Wanaume wengi tunapitia hizi changamoto ndani ya ndoa ila tunakomaa nazo.

Naamini hapa kuna watu wazoefu wanaweza kutoa ushauri mzuri ili kuokoa hili janga wanaume mtetezi wetu ni sisi wenyewe hakunaga akiwezeswa anaweza.

Mimi nimekumbana na ishu za kufanana na hizo hadi wife na familia ikawa kama isolated na jamii since 2021. Ila nashukuru Mungu mambo yanaenda yanapungua.

Kitu nilichojifunza na kukiona haya mambo yanaanzia kwenye koo zetu na huko makanisani then yakilipuka unajichanganya unaenda kule kule kanisani walau zamani makanisani walikuwa na saikolojia nzuri siku hizi na ni wachochezi, pia usiende kwa waganga watahitaji pesa.

Jaribu kuchunguza uhusiano wa ukoo pande zote kwako na kwake. Swala la hela najua linaweza lisiwe tatizo kabisa maana unaweza kumuachia hata milioni kila wiki na asijue kitu cha msingi cha kufanya utapoteza hela kinoma.

Pia usiache kutafuta muda wa kupumzika na mkeo, tafuta maeneo tulivu muongee na kufanya reflection ya maisha yenu mkiwa wawili tu, na sehemu tofauti na nyumbani kabisa. Hospitali za matatizo ya akili wanaweza ila sina uzoefu kwenye hilo.

Wangu hadi sasa amerudi kanisani kwake Catholic anasema KKKT wachawi, japo najua ipo siku atarudi tu maana anamjua Mungu kweli kweli anasali balaa hata mimi sifui dafu. Kuna mambo nataka nifanye trial ikiwa ni pamoja na kushift makazi kureset almost everything kwenye mfumo wa social capital.
umesema vizuri mkuu naunga hoja mkono
 
Yaani inasikitisha na inahitaji uvumilivu,Tumeowana kama miaka 20 iliyopita tuna mtoto mmoja na mmoja alifariki.

Kama miaka 4 iliyopita hivi ndivyo mwenzangu alipoanza kupitia changamoto za kuchanganyikiwa, anaweza akaazisha zogo bila sababu kunituhumu namroga au mimi malaya,kila mtu kwake ni mchawi,yaani yeye ni mtu wa kulalamika tu, tuachane nimpe taraka na mambo chungu nzima
Anaweza anzisha zogo sehemu yoyote ile iwe kwenye gari sokoni au sehemu yoyote ile
Kwa kweli inahitaji moyo ukitegemea wakati namuowa alikuwa vizuri tu
Kuna mambo anashindwa kuyachakata, hayana majibu. Akishaanza kuona mapichapicha anavurugikiwa maana hayana majibu.

Shida hata hao wanaosema wanatibu akili wataanza kukuelezea ubongo.

Anahitaji utulivu wa akili, kama una nafasi ungeweza kutoka nae na kwenda kupiga kambi hata mbuga za wanyama kwa wiki, ukitoka huko leta mrejesho hapa.
 
Yaani inasikitisha na inahitaji uvumilivu,Tumeowana kama miaka 20 iliyopita tuna mtoto mmoja na mmoja alifariki.

Kama miaka 4 iliyopita hivi ndivyo mwenzangu alipoanza kupitia changamoto za kuchanganyikiwa, anaweza akaazisha zogo bila sababu kunituhumu namroga au mimi malaya,kila mtu kwake ni mchawi,yaani yeye ni mtu wa kulalamika tu, tuachane nimpe taraka na mambo chungu nzima
Anaweza anzisha zogo sehemu yoyote ile iwe kwenye gari sokoni au sehemu yoyote ile
Kwa kweli inahitaji moyo ukitegemea wakati namuowa alikuwa vizuri tu
Pole sana..Kwenye shinda na raha.. sasa hapo ndio kipindi cha shida sasa..

Kwanza uliza kama kwao kuna historia ya ugonjwa huo kama ndio huwa wanadeal nao vipi kama lah then anza kumpeleka kwa wataalam huko watampima na kumfanyia uchunguzi na kuanza tiba ..

Mungu awaponye na kumponya mkeo maisha yaendelee kama awali.
 
Kama nakuona namna unavyoisha mwili....Bora kununa kuliko kelele....yaan ni hatari kwa afya.
Huyo mrudishe home kwao atibiwe au msihi aache kwenda kwa waganga
Hapo anapokaa na mumewe ndo kwao. Au unataka ampeleke kwa Ndugulile zake?
Wanaume tukishaanzisha family kwetu ni hapo na watoto na mke.
Yeye atafutr tiba ndugu zake watamsaidia akiwa hapo kwake.
 
Huu uzi kuna namna mods wasaidie kuuweka vizuri na kupin 📌. Wanaume wengi tunapitia hizi changamoto ndani ya ndoa ila tunakomaa nazo.

Naamini hapa kuna watu wazoefu wanaweza kutoa ushauri mzuri ili kuokoa hili janga wanaume mtetezi wetu ni sisi wenyewe hakunaga akiwezeswa anaweza.

Mimi nimekumbana na ishu za kufanana na hizo hadi wife na familia ikawa kama isolated na jamii since 2021. Ila nashukuru Mungu mambo yanaenda yanapungua.

Kitu nilichojifunza na kukiona haya mambo yanaanzia kwenye koo zetu na huko makanisani then yakilipuka unajichanganya unaenda kule kule kanisani walau zamani makanisani walikuwa na saikolojia nzuri siku hizi na ni wachochezi, pia usiende kwa waganga watahitaji pesa.

Jaribu kuchunguza uhusiano wa ukoo pande zote kwako na kwake. Swala la hela najua linaweza lisiwe tatizo kabisa maana unaweza kumuachia hata milioni kila wiki na asijue kitu cha msingi cha kufanya utapoteza hela kinoma.

Pia usiache kutafuta muda wa kupumzika na mkeo, tafuta maeneo tulivu muongee na kufanya reflection ya maisha yenu mkiwa wawili tu, na sehemu tofauti na nyumbani kabisa. Hospitali za matatizo ya akili wanaweza ila sina uzoefu kwenye hilo.

Wangu hadi sasa amerudi kanisani kwake Catholic anasema KKKT wachawi, japo najua ipo siku atarudi tu maana anamjua Mungu kweli kweli anasali balaa hata mimi sifui dafu. Kuna mambo nataka nifanye trial ikiwa ni pamoja na kushift makazi kureset almost everything kwenye mfumo wa social capital.
Yaani ilianza kama utani familia yake ikaniambia nimpeleke kwa waganga,kutokana na imani yangu nikawakatalia,baadaye nikampeleka kwa dada yake maana hana baba wala mama,kibao kikanigeukia wakasema mganga kasema mimi ndiye ninayemloga, sijawahi kuloga hata kuku, mimi ni mfanyabiashara shughuli zangu nategemea ubunifu na akili yangu aliyonipa Mwenyezi Mungu,kaka zake wakaingilia kati ndiyo wakampeleka mloganzira,maana mimi siishi Tanzania,
Lakini kuna wakati akianza matatizo yake anasema hata mwanaye wa kumzaa aliyemaliza form four mwaka huu anamroga, sasa sijui ni mapepo au vipi ingawa najitaidi sana uvumilivu yaani ni mtihani mzito, unamuuguza mtu anayekutuhumu wewe mchawi inaitaji upendo wa hali juu sana
 
Back
Top Bottom