Narudi zangu kijijini, maisha ya mjini siyataki tena

Kweli mkuu, simu ni kisababishi namba moja kilichosababisha kupungua kwa upendo katika jamii; imeondoa ile dhana ya kutembeleana na kusaidiana.​
Simu ni mtihani mkubwa sana kwa jamii
Kuna watoto wa shule ulaya waliulizwa mmoja mmoja kuwa je unatumia simu masaa mangapi kwa siku?
Yaani wengine mpaka masaa 7 kwa siku
Watu wazima ndio kabisa
Mtu unamkuta anawasiliana na ndugu kwa simu ilhali anaweza kwenda na kukaa nao hata saa moja
Maadili yamekufa kisa simu
Simu ni mpango mzima wa kuwafanya wengi wasiwe wabunifu
Kutwa jitu linacheka na simu badala ya ku socialize na wenzie
Ukiuliza unaweza kuiacha simu kwa siku ngapi bila kuigusa wengine wanakuambia eti ntakufa ndio uhai wangu 😄
Ukimuuliza tena inakuingizia sh ngapi anakenua meno
 
Kuna vijiji vina mandhari nzuri sana, hatujazaliwa ili tukue,tuzeeke, na tufie sehemu zenye msongo wa mawazo; kubadili mazingira ni muhimu.
Kabisa mkuu maisha ya dar kero nyingi hewa Chafu hulali vizuri kelele za bar na vigodoro ni shida tupu ukitaka kwenda sehemu hujui utafika saa ngap kero tupu maisha ya dar nilikimbia mda sana
 
Sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…