Narudi zangu kijijini, maisha ya mjini siyataki tena

Kijijini maisha sio marahisi kama unavyofikiri.

Utajuta na kutamani kurudi mjini.

1. Hospitali zipo mbali.

2. Baadhi ya maeneo hakuna maji safi na salama.

3. Ushirikina uliopitiliza.

4. Wivu uliopitiliza.

5. Barabara za vumbi.

6. Kukaa gizani ni kawaida .

7. Huduma za kifedha zipo mbali.
 
Umenikumbusha kupiga hodi mtoni tulipokuwa tunaenda kuoga mtoni
 
Maisha ya mjini kila siku ni mateso, muda mwingi unaupoteza bara barani; achilia mbali stress za hapa na pale
Kuna jamaa yangu tulikutana baada ya miaka kadhaa kukatika ananiuliza dogo umekuwa mlevi halafu mbona unazeeka hivi wakati hata bia sinywi ila nilikuwa nauza ndani ya vingunguti

Ujue ikiwa unachelewa kulala na unaamka mapema ngozi inafubaa unapoteza mvuto hata akili inapunguza ubora wake wa kufikiri, kumbukumb n.k
 
Kuishi mjini haswa dar kuna hitaji uwe na moyo mgumu, sisi tusiopenda heka tulikimbia muda sana aisee, na hiyo hali ya hewa ilivyo ngumu nduo balaaa... Karibu karne ya tisa mkuu, huku tunaishi kijamaa mjini ni ubepari.
Mjini mkikutana mtaani mnakuwa kama hamjuani, kila mmoja ana changamoto zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…