Narudia tena, Usafiri wa daladala hapa Dar es Salaam ni kwa ajili ya watu masikini

Narudia tena, Usafiri wa daladala hapa Dar es Salaam ni kwa ajili ya watu masikini

unajipa matumaini lakini matajiri kama hawataki kutumia magari yao basi wana kodisha bolt au uber ....hayo mambo ya kubanana kwenye madaladala si ya kitoto .....yaani mtu uwe na kauwezo halafu ugombanie daladala mara ukanyagwe,upumuliwe ...duh hiyo wanaweza Wakinga tu au yule tajiri anayemiliki kampuni kuuubwa ya GALILAYA manake ni utajiri wao ni wa masharti...
Hapo ulipo akaunti yako ya benki haya 30,000 hauna halafu unakuja kuandika uharo. Gari kitu gani jenga mijengo miliki nyumba za kifahari upangishe totoz.
 
Usafiri wa daladala hapa Dar ni kwaajili ya maskini.

Vijana tutafute pesa huku tukimwomba Mungu atuepushe na Usafiri huu uliojaa karaha na kadhia.

Haiwekani mtu una pesa zako usimame Kariakoo mpaka Mbagala, au usimame Kariakoo mpaka Tegeta.

Jioni ukitoka mjini kwenda pembezoni mwa jiji unavizia basi la kugeuka nalo ili upate siti, nako ukishangaa hupati.

Makonda jioni wanaringa kama wasichana mabikira.

Watu wananuka sigara mnapumuliana.
 
Sio lazima usimame mkuu unaweza chuchumaa,kupiga magoti na hata kujiegemeza kwenye miguu ya abiria mwenzako aliyesimama au hata kukaa.Haijazuiwa unaweza kufanya kati ya hayo.
 
Back
Top Bottom