Unenikumbusha Miaka kadhaa nyuma; kuna Jamaa alikuwa mwanafunzi chuo flani amepanga kwa Msataafu mmoja anaishi na Familia yake..
Huyu Mwanachuo alikuwa mtu Wa Dini sana ilhali Vijana Wa Mzee Mstaafu walikataa shule wakawa watu Wa mitungi na Bhange tu. Mstaafu akatokea kumwelewa sana Bwana mdogo mpaka akamkabidhi Kadi yake ya Benki. Siku akitaka pesa anamwambia Dogo amtolee mpunga Kwenye ATM maeneo ya chuoni kwao akirejea maskani awe anampatia.
Maisha yakaenda hivyo, huku Familia haijui kuwa Mzee amekabidhi kadi kwa Dogo maana Mzee alimwambia wakijua watakusumbua.. Sasa siku moja Ghafla Mzee Presha ikapanda, ile kumwahisha Hospitali akafia njiani. Jioni Jamaa anarejea akakutana na msiba, Mama Analia na kuomboleza wataishije bila Mzee.
Dogo akala buyu tu mpaka walipomaliza kuzika ndipo akamwita Mama pembeni akamkabidhi kadi akamwambia hii alinipa Mzee niwe namtolea Pesa na kwenye akaunti kimebakia kiasi kadhaa. Mama hakuamini macho yake. Kuanzia siku ile Dogo akawa halipi kodi na akawekwa kwenye orodha ya msosi kama mmoja Wa watoto Wa Mama. Na jukumu la kutoa pesa Mama akamwachia aendelee nalo pindi akihitaji pesa.
Yule Jamaa alipomaliza chuo hakumaliza mwezi Mtaani akala Shavu kwenye Mashirika ya UN, Mshahara mnono na marupurupu ya maana. Mpaka Leo anamhudumia yule Mama pamoja na kuipa sapoti zote Familia ya Marehemu Mstaafu, na hata shughuli za kuozesha mabinti Wa Mstaafu Mama alimkabidhi Jamaa asimamie kama Kaka Mkubwa Wa Familia..