Hao babu na bibi zako unaowatania unawajua? Huenda hata kijijini kwenu haukujui na hawakujui, wewe hauwatanii bali unawasimanga.
Madhara ya kuzaa watoto mijini hawajui Mila zao hawa ndio unakuta Kaka anamla dadake au baba linakula bintiye mama analiwa na mwanae.
Kizazi cha nyoka wanasahau uzee utajikuta tu. Tunaishi na wazee wetu they were once handsomest and beautiful creatures lakini uzee ni uzee tu.
Maisha ni safari, unaweza kuchuma ujanani na ukaishi vizuri Ila ikakutokea ajali ya maisha,
Wazee walisema, usitukane ukunga ingali uzazi ungalipo. Kuna siku aliyeandika hii thread atajikuta anajilaumu sana maana maisha ni safari ndefu.
Nina umri mchache Ila nimeona watu walikuwa matajiri na wakadhulumiwa, wakafilisiwa na wake zao, wakanyang'anywa Mali na serikali, wakaumwa mpaka biashara zikafa, wakakabidhi ndugu wakaziua zote, Yani mifano ipo hapahapa duniani.
So ukiwa na bahati ya kupata uzee wenye ahueni kimaisha shukuru Mungu na usikufuru wasionacho maana hawakupendan
Hakuna kitu kibaya kama uwe mzee na huna pesa maana ndio umri ambao magonjwa ni mengi, upweke, vijana ndio hawa wanapoona mzee wanahisi age tu hana maana ya kuishi.
Tusijitafutie laana tukaishi kwa tabu duniani.