Nash MC ana elimu gani?

Nash MC ana elimu gani?

endeleeni kumpa kichwa wakati mwenzenu anaangamia ni nini anachohamasisha jamii ikiwa yeye mwenyew hataki kutoka kwenye wimbi la umasikini alikuwa nao kakosa plan b ndio mana amebakia kuwa mtu wa wakulalamika tu na kutukana media mbona wenzie wakina niki mbishi wametulia na wana respect msimpe kichwa kiivyo mshaurini abadilike anajifanya ni mjuaji mno kitu ambacho anaharibu
we ndo kitobo kweli Nash na nikki kwenye mahusiano yao na media ni mtu na pacha wake
 
Huyu jamaa naweza sema ni mwanahip hop bora Tanzania ambaye hajawahi kubadilika,wako malegends kama Sugu au Jay ila huyu jamaa ukisikiliza nyimbo zake utagundua ni msomi,na pia anatumia kiswahili sanifu.

Album yake mpya kuna nyimbo kama maneno,barua toka Bangui,viwango vyake vya mashairi inaonekana mtu tafiti.


Nadiriki kusema ni msanii wa hip hop asiyebadilika na mwenye mashairi yanayofundisha
PhD in Musicology
 
Amefuzu 'Elimu ya Mtaa' na akaelimika vyema kwenye elimu hiyo.

Sikiliza wimbo wake 'Naandika' then utajua ni msanii mwenye elimu gani.

KINASA forever.

-Kaveli-
 
Nilimuelewa kwenye nyimbo ya tabia na mitihani baada ta hapo sikuweza kumsikia tena mana kwenye media ni kama kakosa promo

Ni miongoni mwa hip hop emcee bora hapa bongo, lakini mainstream inambania sana airtime.

Kwanini anabaniwa airtime? Alishajibu kwenye nyimbo zake 'Maneno' na 'Maswali ya Kiwack'... na pia kwenye 'HASI 15'.

-Kaveli-
 
hajui kingereza tatizo

Acha uongo. Possibly wewe humfikii Nash kwenye spoken English.

Kwa hip hop emcees wa bongo, Maalim Nash anajitahidi saaaana kutema lugha ya malkia. Check hii alipokuwa Berlin Germany mwishoni mwa mwaka 2018:


-Kaveli-
 
Huyo Mc Ni Chama gani?

Swali lako haliwezi kupata JIBU.

Ila naamini utapata JAWABU la swali lako endapo ukisikiliza nyimbo zake zifuatazo:

-Mchochezi
-Maalim Ponda
-Shujaa
-Beti

-Kaveli-
 
Hpo anatoa speech kwenye chuo fulani ujerumani.....
Wabana pua hawawezi harakati hzo

Ova
View attachment 1146995
Ananiudhi sana uvaaji wake, anavaa kifalafala tu, tunaijua hiphop, hiphop haihusiani na uchafu hiyo ni tabia binafsi
Tazama tangu enzi za NWA, kina Ice Cube, Eminem, Dre, Pac, Big, Nas nk hakuna mchafu mchafu
Walisuka nywele, waliweka vipini nk ili wapendeze, miaka ya nyuma sana kweli walivaa hovyo lakini sio kwamba ndio hiphop ni kwa sababu za kiuchumi, tazama baada ya kushika hela wote wanashine na wanafanya hiphop, ingekuwa kushine kunahusiana na muziki wao wangebadili aina ya muziki pia.
Sasa wasanii wetu wa hiphop wanafikiri kuna uhusiano kati ya hiphop na uchafu, angalau kuna baadhi wanajitambua wanapendeza siku hizi kama tamaduni, weusi, kina Darasa nk

Mtu asiniambie Nash hashine sababu hana hela ni uongo, uwezo wa kuvaa anao sema anachanganya sana hiphop na imani yake

Anavaa hovyo hovyo sana sio sio msanii wa mfano, ni mfano mbaya kwa hiphop na asichojua anafikiri anakuza hiphop kumbe anaiua, ili aina ya muziki ikue ni ipate waimbaji wengi, sasa hakuna aliye nje ya muziki atatamani kuingia kwenye hiphop kwa kumtazama Nash

Kijana akimtazama Nash anaiona dhiki kuu ndani ya hiphop, anaamua kubana pua tu maana huko vijana wanajaribu sana kuficha njaa hata kama hawana kitu
 
Back
Top Bottom