Hpo anatoa speech kwenye chuo fulani ujerumani.....
Wabana pua hawawezi harakati hzo
Ova
View attachment 1146995
Ananiudhi sana uvaaji wake, anavaa kifalafala tu, tunaijua hiphop, hiphop haihusiani na uchafu hiyo ni tabia binafsi
Tazama tangu enzi za NWA, kina Ice Cube, Eminem, Dre, Pac, Big, Nas nk hakuna mchafu mchafu
Walisuka nywele, waliweka vipini nk ili wapendeze, miaka ya nyuma sana kweli walivaa hovyo lakini sio kwamba ndio hiphop ni kwa sababu za kiuchumi, tazama baada ya kushika hela wote wanashine na wanafanya hiphop, ingekuwa kushine kunahusiana na muziki wao wangebadili aina ya muziki pia.
Sasa wasanii wetu wa hiphop wanafikiri kuna uhusiano kati ya hiphop na uchafu, angalau kuna baadhi wanajitambua wanapendeza siku hizi kama tamaduni, weusi, kina Darasa nk
Mtu asiniambie Nash hashine sababu hana hela ni uongo, uwezo wa kuvaa anao sema anachanganya sana hiphop na imani yake
Anavaa hovyo hovyo sana sio sio msanii wa mfano, ni mfano mbaya kwa hiphop na asichojua anafikiri anakuza hiphop kumbe anaiua, ili aina ya muziki ikue ni ipate waimbaji wengi, sasa hakuna aliye nje ya muziki atatamani kuingia kwenye hiphop kwa kumtazama Nash
Kijana akimtazama Nash anaiona dhiki kuu ndani ya hiphop, anaamua kubana pua tu maana huko vijana wanajaribu sana kuficha njaa hata kama hawana kitu