Nashangaa mzazi mwenzangu bado ana number yangu ya simu mpaka leo.

kyanyangwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2018
Posts
1,511
Reaction score
4,369
Aliondoka nyumbani hapa na watoto na kila kitu chake tena kwa nyodo,akajiapiza hatokaa anitafute kwa lolote na number yangu ya simu anafuta.
Sasa leo ktk kuperuzi huko whatsapp nakutana na status yake kaweka vifungu vya biblia, nijuavyo mtu kama hana number yako akiweka status wewe huwezi kuona,sasa nimeshindwa kumuelewa huyu raia alisema anafuta number yangu but naona bado anayo.
Je nimuulize kwa nini bado anayo au nifanyeje?
 
Growup man, subiri akutafute
 

We inakuhusu Nini kama ajapiga? It's over, move on, mbona vijana mmekuwa walaini hivyo? What does she has to offer? Si ni uchi tu? Forget her, do your thing
 
Kwanini ww usiifute yke?

Kma mm ningeifuta yke on the spot sipendi kujikera kwa jambo ambalo halina maslahi na mimi
 
Kwa nini wewe umebakiwa na namba yake?
 
We mwenyewe mbona hujishangai bado unayo namba yake?unamshangaa yeye🤣
We bado unayo ya Nini?
Vichwa vya wanaume wa siku hizi bwana...sa mfano mwanao Yuko hoi anaumwa atakupaje taarifa?si mzazi mwenzio mnalea bado?

Bora kuzaa na ng'ombe kuliko mwanaume wa kiafrika.hayanaga akili kabisa.
 

Mkuu umefika pabaya kuhusu Kufananisha Wanaume wa kiafrika na Ng'ombe.
 
Wewe ndo unayo nambake ndio maana status zake unaview ungekuwa huna nambake usingeona stat zake
 
Umeshasema mzaz mwenzako mmezaa watoto Sasa kwann asiwe na namba zako? Haya sawa kafuta wewe huitaj kujua maendeleo ya watoto wako? Akiii wanaume mmekuaje
 
Wanawake mna mambo. Hao watoto si wako wanawake wawili hawawezi zaa labda kama alipandikiza na bado pia si wako. Wewe amua kuolewa na yeye labda ameshaolewa.
 
Wewe kenge mtetea sikia sawa? Usirudie tena kuita baba zako na kaka zako hayanaga akili, punda we
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…