Nashauri: Kuongea Kiingereza kwa unyoofu (fluency) ibaki kuwa kigezo cha kumpima Mtanzania mwenye Degree

Nashauri: Kuongea Kiingereza kwa unyoofu (fluency) ibaki kuwa kigezo cha kumpima Mtanzania mwenye Degree

umesahau hili mkuu yaani degree watu wasiwe wanasoma fani yoyote, hizi sijui sociology watu wasome wakiwa form five na six, mtu akifika chuo ni kusoma english course tu miaka mitatu tutafanikiwa sana, maendeleo hayana chama.
Hii ni yako mkuu. Degree unasomea fani hiyo fani jitahidi uwe na uwezo wa kuilezea kwa lugha ya kiingereza kwa kujiamini maana hukufundishwa kwa kiswahili.

Lakini isiihie hapo, uwe na uwezo wa kujieleza kwenye mambo mengine yoyote ya kijamii na kimataifa kwa lugha ya kimataifa. Sio msomi mjanjamjanja the the the nyingi kama STD 7 Kayumba.
 
Ndo maana enzi zile walituibia kila litu kizuri wanatangaza kipo kwao na wazungu wakawaamini. Mfano mlima Kilimanjaro
Kuna wazungu wanajua TZ ni mkoa ulioko 🇰🇪 . Kama huwezi kujieleza kimataifa, anayejua atakutumia kwa maslahi yake binafsi
 
Ndo maana enzi zile walituibia kila litu kizuri wanatangaza kipo kwao na wazungu wakawaamini. Mfano mlima Kilimanjaro
Usipojelezea kwa kueleweka huwezi kusikilizwa. Atasikilizwa anaeyeweza kufanya na kujielezea vizuri kwa ufasaha.
 
Huwa naona kama Baba wa Taifa kwa hili la KISWAHILI kuwa lugha ya kufundishia kwa elimu ya MSINGI hakuwa SAWA..tungekuwa tu kama wenzetu wa Kenya,Uganda+ SADC yote,ukitoa Msumbiji
Waru waliosoma kabla ya uhuru na shule za kikoloni. Wanauwezo mkubwa wa kuongea kiswahili na kiingereza tena bila kuchanganya kama wasomi wajanjawajanja wa kisasa.
Hapo tu unajua angeendeleza tungefika mbali. Yeye mwenyewe nimeona anatwanga English kali sana wazungu wanamsikiliza kwa akili zote.

Ila amefanya nafasi yake, tunamshukuru pia.
 
Hii ni yako mkuu. Degree unasomea fani hiyo fani jitahidi uwe na uwezo wa kuilezea kwa lugha ya kiingereza kwa kujiamini maana hukufundishwa kwa kiswahili.

Lakini isiihie hapo, uwe na uwezo wa kujieleza kwenye mambo mengine yoyote ya kijamii na kimataifa kwa lugha ya kimataifa. Sio msomi mjanjamjanja the the the nyingi kama STD 7 Kayumba.
mkuu unanikataa, mimi nataka kufanya kazi russia kiingereza sikihitaji, angalau ungesema mtu awe fluently lugha yoyote ya kimataifa na kiswahili lazima, kulazimishana kiingereza ni utumwa mkuu, au wewe bado minyororo unayo shingoni imekamata kichwa na ubongo wako.
 
Eti mtu ana degree hajui kutaja entrepreneurship
Inatakiwa vyuo vianzishe vile vibao vya kuvalishwa Swahili Speakers hadi mabwenini kwao.

Pia midahalo ya mambo ya kimataifa kwa kiingereza ziwepo, vijana akili zichangamke. Sio mtu unaongea kila baada ya nomino unachomeka neno THE ili uvutevute muda wa kufikiria Vitenzi na nomino za kiingereza za kujazia 😅
 
Kuna interview nilienda kufanya nikamkuta mdada mmoja wa kibongo na mzungu mmoja. Japo nilipita ila mpaka leo huwa nikikumbuka aibu nilizopata mule nabaki kusononeka.

Mtoto wangu nitajitahidi nimuandae mapema kwenye lugha kuna watu kibao wamepishana na fursa kibao tena za maana kisa kutokujua lugha vizuri.

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
 
mkuu unanikataa, mimi nataka kufanya kazi russia kiingereza sikihitaji, angalau ungesema mtu awe fluently lugha yoyote ya kimataifa na kiswahili lazima, kulazimishana kiingereza ni utumwa mkuu, au wewe bado minyororo unayo shingoni imekamata kichwa na ubongo wako.
Kiingereza ni Lugha ya kimataifa. Warusi wanaotaka kufunguka nje ya Urusi wanakijua. Vladimir Putin anakijua, Dimirty Medvedev anakitwanga tena kilichonyooka.
Wachina wanajifunza, waarabu wanajifunza. Lazima ukijue kwa maslahi mapana nje ya Urusi. Dunia nzima ni Yetu sio busara sana kuufunga ubongo kwa mipaka ya kinchi.
 
Wasomi wengi hawawezi kuongea Kiingereza kwa unyoofu na kwa kujiamini.

Kuna msomi mmoja ilibidi nimuandikie barua ya kazi maana alikuwa anaenda kuabika kwa madudu aliyoandika. Ajabu ana 1.6 ya HGL na UpperSecond ya Sociology.

Naamini kama huwezi kujieleza kwa unyoofu na kwa lugha nyepesi kule unachokielewa basi wewe hukielewi na kama ulijifunza kwa Kiingereza tunataka ukieleze kwa uzuri kwa lugha hiyo.

Moja ya majuto yangu katika elimu ya juu, nikutojipa muda wa kutosha kujiendeleza kuongea na kuandika kiingereza kwa ufasaha. Niliashumu najua.

Nini maoni yako?
Kama English ni mafanikio , wote waliofanikiwa wangekuwa wanazungumza kiingereza Kwa ufasaha
 
Kuna interview nilienda kufanya nikamkuta mdada mmoja wa kibongo na mzungu mmoja. Japo nilipita ila mpaka leo huwa nikikumbuka aibu nilizopata mule nabaki kusononeka.

Mtoto wangu nitajitahidi nimuandae mapema kwenye lugha kuna watu kibao wamepishana na fursa kibao tena za maana kisa kutokujua lugha vizuri.

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
Mimi nakubali nimechelewa, nafosi kukipiga brashi ili kinyooke maana kuna watu bila kuwaongelesha kwa kiingereza hawawezi kunichukulia siriasi.

Ila watoto, nimeapa kuwawekea KPI nimarufuku kumaliza STD 7 bila kujua kiingereza kuandika, kusoma na kujeleza katika level ya kimataifa. Hata ulaya kuwapeleka ili wapate mwamko wataenda mshiko ukiwepo.

Kuna jamaa amesoma Uganda, Form six aliingia Usahili na Graduate kampuni moja ya ndge ya ulaya. Wale wasahili walitoka Uholanzi, na walikuwa wanapita baada ya usahili wanatoa majibu wanakwaa pipa, jamaa alikula chaka akawapiku wazee wa the the. Nilikutana naye airport flani akawa ananipa stori ya jinsi alivyopata kazi, na wamempeleka kozi nyingi yuko vizuri sasa.

Lazima tukubali kujishusha. Tusitetee ujinga.
 
Kama English ni mafanikio , wote waliofanikiwa wangekuwa wanazungumza kiingereza Kwa ufasaha
Kiingereza sio mafanikio. Ila kuwa mhitimu wa elimu ya juu alafu hujui kuandika, kusoma na kuongea kiingereza kwa ufasaha ni ujinga.

Mfano mimi Mkulima nikifungua Biashara kubwa na kutaka watu watakaonipa koneksheni za kimataifa kupata masoko nje. Ukija na kadigrii uchwara hujui kuongea umbombo wenye ushawishi nakupiga chini walahi. Niko ladhi nikodi wasahiri ili wakupime vzr.
 
Kiingereza ni Lugha ya kimataifa. Warusi wanaotaka kufunguka nje ya Urusi wanakijua. Vladimir Putin anakijua, Dimirty Medvedev anakitwanga tena kilichonyooka.
Wachina wanajifunza, waarabu wanajifunza. Lazima ukijue kwa maslahi mapana nje ya Urusi. Dunia nzima ni Yetu sio busara sana kuufunga ubongo kwa mipaka ya kinchi.
maslahi gani mkuu kuombea mikopo au, mbona hata kiswahili ni lugha ya kimataifa hujui east afrika yote kiswahili kinazungumzwa kwa ujumla watu zaidi ya millioni 200 wanakipiga, ulienda lini libya au afuganistani
ukakuta wanapiga kiingereza mkuu, wale talibani wajifunze ngeli ya nini mkuu, ulienda lini poland ukakuta wanapiga ngeli ulienda lini ufaransa ukakuta wanapiga ngeli, ni mawazo yangu kila mtu ajifunze lugha ya kimataifa anayoitaka, hakuna kufungwa minyororo na kiingereza.
 
Me I didn't now to speaking English best, but now I trying to speaking good than after.
Watoto wa njano njano, fanyieni marekebisho ya kidhungu changu.
Personal, I don't know how to speak English well, but now am trying to speak well than before.

🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Mjuongeaji mzuri wa lugha huwa hchanganyi changanyi. Utaona mtu anahojiwa kwa kiswahili, halafu anajilazimisha kuweka maneno ya kiingereza " ... to me, mimi naona it is better ku-translate tafsri hii kutoka kiswahili kuwa english directly moja kwa moja."
Kiswanglish yaani kuchanganya kiswahili na kiingereza ni default language ya wasomi yaani sio wanajifanyisha ila hio ndio ipo automatically kwao sasa suala la kuongea dull English hapo tatizo
 
Back
Top Bottom