Nashauri kuwe na Siku Maalum ya Waafrika wote 'Kujiombea' kwa Mwenyezi Mungu Ili tuwe na Akili

Nashauri kuwe na Siku Maalum ya Waafrika wote 'Kujiombea' kwa Mwenyezi Mungu Ili tuwe na Akili

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
1. Mfano kuna Taifa Moja (siyo Rwanda) Wananchi wake kwa sasa wameanza Kuchagua Timu za Kushangilia katika Kombe la Dunia lijalo wakati Wao hata Kufuzu tu AFCON ni shida na hapo hapo tena kuna Timu imefuzu Kombe la 'Luzaz' lakini Wanashangilia utadhani Wametinga Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika kama Wenzao.

2. Mfano kuna Taifa Moja (siyo Rwanda) lenye lina 81% ya Utajiri wa Maji na Vyanzo vyake ila kwa sasa Wananchi wake hawaogi na wananuka tu Vikwapa kwa Mgawo wa Maji.

3. Mfano kuna Taifa Moja (siyo Rwanda) lenyewe lina Utajiri mkubwa sana wa Rasilimali ila Kutwa tu Kiongozi wake anarandaranda Angani kama Popo kwenda Kuomba Misaada kwa nchi ambazo zenyewe hata hazina Utajiri kama uliopo katika nchi hiyo.

4. Mfano kuna Taifa Moja (siyo Rwanda) lenyewe Waandishi wake wa Habari wako kwa ajili tu ya Kusifia Mamlaka Ili wapate Uteuzi na siyo Kuibua Masuala kwa Maendeleo ya hilo Taifa lao.

5. Mfano kuna Taifa Moja (siyo Rwanda) lenyewe 85% ya Wanawake wao wako katika Vikundi vya Kukopa na Kukopeshana ila Ukiwachunguza Kiumakini utakuta ndiyo Masikini kupita Maelezo.

6. Mfano kuna Taifa Moja (siyo Rwanda) lenyewe 99% ya Wasomi wake ni wale wanaopenda tu Kumiliki Certificates za Kitaaluma na Kutambiana ila Utendaji wa Kiufanisi kutokana na Elimu zao walizonazo ni bure na hovyo kabisa.

7. Mfano kuna Taifa Moja (siyo Rwanda) lenyewe Watu wenye Akili Kubwa (Great Thinkers) wanapingwa na mpaka kuchukiwa ila wale Wapumbavu (Fools) ndiyo Wanakubalika, Wanapendwa, Wanasikilizwa na Kuaminika sana.

Je, kwa hii Mifano yangu Saba ( 7 ) hapa juu hakuna Haja kweli ya kuliombea hili Bara letu la Afrika?

Na kinachonisikitisha na kuniumiza zaidi kuna nchi Moja (siyo Rwanda) Mwenyezi Mungu kaipendelea kwa kuwepo na Mtandao Mkubwa wa Kijamii wenye Watu Werevu tupu (Critical and Rational Thinkers) wa JamiiForums lakini hawautumii vizuri na badala yake ndiyo Kwanza Wanauchukia na hadi kutaka Kuuhujumu pia wakati ndiyo Mtandao ambao ungewasaidia kwa 99% kuondokana na Matatizo yao makubwa Manne ya Upumbavu, Maradhi, Umasikini na Ushamba.
 
Taifa la watu wazembe wazembe wasiowajibika.
Raia wanadhani kupatiwa huduma mbali mbali wanazolipia kodi ni hisani.
 
Taifa la watu wazembe wazembe wasiowajibika.
Raia wanadhani kupatiwa huduma mbali mbali wanazolipia kodi ni hisani.
Mpaka sasa lina Wendawazimu Milioni Saba ( 7,000,000 ) na huenda hiyo idadi ikaongezeka.
 
Ivi hili tahila kwann lisipigwe permanent ban, linakera namathread yake ya hovyo kama yametoka chooni looh, [emoji35][emoji35][emoji35][emoji35]
 
Labda ni kwa vile tuliuwa taifa letu Tanganyika na kuvamia utaifa mengine ndio maana hata zile baraka alizojaliwa Tanganyika hazimfikii Tanzania kwa sababu I'd au address yake haijulikani tena.

Ni sawa upewe barua kwa jina na anwani ya fulani, kabla ya ile barua kufika yule fulani akabadilisha anwani na utambulisho wake! Hio barua kamwe haitamfikia kamwe hata kama ilikua na thamani kiasi gani.
 
Role model wangu GENTAMYCINE
Asante sana na Ubarikiwe mno Mkuu. Hata hivyo kwa hii post yako tegemea kuambiwa na Wanaonichukia kwa Tunu ( Shani ) niliyonayo kwa Kubarikiwa na Mwenyezi Mungu kuwa hii ID yako ni yangu na hapa Nimejisifia tu.
 
Hii nchi ukiwa na akili sana unakuwa tishio kwa vialaza, inabidi wakuzime ili wajisikie vizuri..... Machawa ndo wanatoboa
 
6. Mfano kuna Taifa Moja (siyo Rwanda) lenyewe 99% ya Wasomi wake ni wale wanaopenda tu Kumiliki Certificates za Kitaaluma na Kutambiana ila Utendaji wa Kiufanisi kutokana na Elimu zao walizonazo ni bure na hovyo kabisa.

Hapa umeongea kweli mtani, Taifa lenyewe tunalijua, lakini kwanini Waafrika wote tujioombee kwa Mungu wakati tatizo ni kwa hilo taifa moja???
 
Ninawadharau watu wote wanaopenda kuifananisha nchi ya Tanzania na Rwanda. Hiyo ni insubordination ya hali ya juu kwa Mtanzania yeyote. Hatupaswi hata siku moja kujifananisha wala kuiga yanayotokea Rwanda. Rwanda labda ijifananishe na mkoa Mwanza +Simiyu kiuchumi na kijiografia. Kwa upande wa siasa na demokrasia hakuna cha kujifunza. Hatuwezi kuiga sera za ukandamizaji wa haki za kiraia na udikteta za Kagame. Tuko mbali mno pamoja na kwamba Magufuli alikuwa anakopi na kupaste staili ya utawala kutoka kwa PK.

Sisi tukitaka maendeleo tujaribu kujifananisha au kuwaiga Kenya na kwenye siasa na demokrasia tuangalie nchi ya South Africa au Botswana. Kujilinganisha na Rwanda ni KUJIDHARAU WENYEWE.
 
Back
Top Bottom