1. Mfano kuna Taifa Moja (siyo Rwanda) Wananchi wake kwa sasa wameanza Kuchagua Timu za Kushangilia katika Kombe la Dunia lijalo wakati Wao hata Kufuzu tu AFCON ni shida na hapo hapo tena kuna Timu imefuzu Kombe la 'Luzaz' lakini Wanashangilia utadhani Wametinga Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika kama Wenzao.
2. Mfano kuna Taifa Moja (siyo Rwanda) lenye lina 81% ya Utajiri wa Maji na Vyanzo vyake ila kwa sasa Wananchi wake hawaogi na wananuka tu Vikwapa kwa Mgawo wa Maji.
3. Mfano kuna Taifa Moja (siyo Rwanda) lenyewe lina Utajiri mkubwa sana wa Rasilimali ila Kutwa tu Kiongozi wake anarandaranda Angani kama Popo kwenda Kuomba Misaada kwa nchi ambazo zenyewe hata hazina Utajiri kama uliopo katika nchi hiyo.
4. Mfano kuna Taifa Moja (siyo Rwanda) lenyewe Waandishi wake wa Habari wako kwa ajili tu ya Kusifia Mamlaka Ili wapate Uteuzi na siyo Kuibua Masuala kwa Maendeleo ya hilo Taifa lao.
5. Mfano kuna Taifa Moja (siyo Rwanda) lenyewe 85% ya Wanawake wao wako katika Vikundi vya Kukopa na Kukopeshana ila Ukiwachunguza Kiumakini utakuta ndiyo Masikini kupita Maelezo.
6. Mfano kuna Taifa Moja (siyo Rwanda) lenyewe 99% ya Wasomi wake ni wale wanaopenda tu Kumiliki Certificates za Kitaaluma na Kutambiana ila Utendaji wa Kiufanisi kutokana na Elimu zao walizonazo ni bure na hovyo kabisa.
7. Mfano kuna Taifa Moja (siyo Rwanda) lenyewe Watu wenye Akili Kubwa (Great Thinkers) wanapingwa na mpaka kuchukiwa ila wale Wapumbavu (Fools) ndiyo Wanakubalika, Wanapendwa, Wanasikilizwa na Kuaminika sana.
Je, kwa hii Mifano yangu Saba ( 7 ) hapa juu hakuna Haja kweli ya kuliombea hili Bara letu la Afrika?
Na kinachonisikitisha na kuniumiza zaidi kuna nchi Moja (siyo Rwanda) Mwenyezi Mungu kaipendelea kwa kuwepo na Mtandao Mkubwa wa Kijamii wenye Watu Werevu tupu (Critical and Rational Thinkers) wa JamiiForums lakini hawautumii vizuri na badala yake ndiyo Kwanza Wanauchukia na hadi kutaka Kuuhujumu pia wakati ndiyo Mtandao ambao ungewasaidia kwa 99% kuondokana na Matatizo yao makubwa Manne ya Upumbavu, Maradhi, Umasikini na Ushamba.