Nashauri nafasi ya Urais tumpe Mzungu ili atuletee maendeleo

Nashauri nafasi ya Urais tumpe Mzungu ili atuletee maendeleo

Sheria zikifuatwa kila kitu kitaenda sawa
Linatakiwa Bunge liwe na meno na kuwawajibisha wote wanaopindisha sheria hata kama ni Rais
 
Maendeleo hayaletwi ndio maana hayafiki, maendeleo yanajengwa. Maendeleo yanajengwa na wananchi kwa kushirikiana na serikali.

Kama maendeleo yangelikuwa bandarini au uwanja wa ndege kila kiongozi angeweza kuyafikisha kwa wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni Rangi tu kwanini tuswakabidhi Albino wetu waiendeshe Nchi.

Nadhani tatizo letu liko kwenye Mindset zetu.
 
Wapo watakao beza hoja yako hii lakini ukweli ni kwamba upo sahihi kabisa nchi hizi za Africa nyingi zinatakiwa kuwa recolonized kwa miaka 100 mingine kama akivyosema Trump! Uhuru wa kujiendesha umetushinda kabisa lazima tuwe wakweli kama Zimbabwe wamesahihisha makosa na nchi zingine ziige mfano angalau kuruhusu njia kuu za uchumi kuwa chini ya wakoloni tukiwa mbioni kuwaachia kiti cha mjengoni!
 
...mfano mzuri Mr.Scott (rip),ndiye mzungu aliyeiletea heshima sarafu ya zambia (kwacha )na alitawala less than 9mths,Leo hapa tunduma unahitaji 110ths ili upate 1 zambian kwacha, noti ya juu kabisa ni 100,Tanzania tuna 10,000 na kuna wapumbavu humu wanataka noti ya 100,000,welcome to Zimbos
Mbona R.i.p?
Si bado yupo?
 
KAZI ya uraisi inatakiwa iwe ni nafasi ya kuomba ajira na sio ya kugombea maana hawana cha maana zaidi ya kutuibia tu
 
Maendeleo ya nchi huletwa na mifumo imara ya nchi yenye uwezo wa kusimamiana na kudhibitiana!. Usije ukategemea kuwa kuna mtu yeyote anaweza kukuletea Maendeleo bila kuwepo mifumo hiyo imara!.
 
Kqwlo
Ndugu zangu Watanzania napendekeza Wazungu wagombee nafasi ya Urais ili watuletee maendeleo,tumeona katika shughuli za kimaendeleo tumewapa bandari ndugu zetu DP World,tumefanikiwa, Tanesco napo panasua sua tumwongezee DP World aweze kuleta Umeme wa uhakika wakikataa tuwaite tena Net Solution ili watuendeshee shirika letu la Umeme,bado tuna idara nyingi pia zimedorora kama idara za maji zote za mijini na vijijini nchi nzima kama nyongeza,baada ya hapo wapewe na hospitali/zahanati/vituo vya afya vyote nchi nzima kama bonus ila nimeona tunazunguka bure tufanye kama walivyofanya Zimbabwe,wamewaita tena Wazungu waje walime kwenye mashamba makubwa plantations maana Wazimbabwe hawawezi kulima,Wazungu wameitikia wito wamekuja na wameanza kulima, Zimbabwe imeanza kuwa ya kijani badala ya jangwa,kwa nini sisi Watanzania tusiwaite Wazungu waje wagombee urais na chawa wawapigie kampeni washinde urais na nchi yetu iongozwe tena na mzungu,tuanze kula nyama za kwenye kopo,tufufue kile kiwanda cha Tanganyika Packers, tufufue Ceramic kiwanda cha vyombo vya Udongo pale Morogoro,Tufufue viwanda vya nguo Polyester na Mwatex,Viwanda vya kutengeneza magari aina ya Nyumbu,viwanda vya kutengeneza viatu kama Moro Shoes,Wazungu walete ofisi zao kubwa kubwa za UN na NGO's makubwa tuongee kiingereza kama Kenya,hatutaongea kiswahili tutaongea kiingereza,mnaonaje Watanzani
Kweli aisee.....Mzungu anaamini ktk mafanikio ya wengi sio kama hawa wa kwetu
 
Back
Top Bottom