Nashauri Pascal Mayalla ateuliwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara

Nashauri Pascal Mayalla ateuliwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara

Ndugu yetu Pascal Mayalla amesugua benchi sana. Na kama kutumia uwezo wake kuwashawishi viongozi, ametumia wote.

Ni muda mwafaka sasa wa mwana JF mwenzetu kuukwapua ukuu wa wilaya ya mtwara. Bwana Pascal Mayalla anayohaiba ya kuwa mkuu wa wilaya na anaijua miiko ya uongozi.

Napaza sauti yangu kwa nguvu kumuombea ndugu yetu huyu apate ukuu wa wilaya.

Mkuu wa wilaya ya mtwara katumbuliwa juzi. Nafasi ipo wazi.
KAMA HAKUUPATA KWA MSUKUMA MWENZAKE MAGUFULI HATAUPATA NG'OOO
 
Mh jamani mm penye ukweli nasema.kiukwel jamaa anamadhaifu kuyaondolea madarakani .ila namuona kama kiongozi mzuri maana kwa anakifua .anauwezo mkubwa kuvumilia kutofautiana bila kinyongo .kwa Tanzania nina wabunge washikaj zangu wa baa wakuu wa wilaya usiseme hilo hawana kabisa .Mimi ntampigia Chapuo mahali inshaalah
 
Rungu limeanzia juu na mpaka leo hii tumempata nambari nne wa nchi hii, mara ya mwisho kuwa na nambari nne katika nchi hii ilikuwa utawala wa Rais Mwinyi.

Rungi sasa linaelekezwa kwa wakurugenzi wa mashirika ya umma, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilata. Bila kuwasahau RAS, DAS na DED.

Ndugu yangu Pascal Mayalla ukipitwa na hili ujue basi tena, maana uzee nao unakunyemelea, na huwezi kuwa mkuu wa kitengo nyeti baada ya hapa. Ukiukosa ukuu wa wilaya katika teuzi zinazofuata basi tena ndugu yangu.

Nakusihi uanze kushona suti kabisa maana imani huzaa imani. Usinisahau mimi ndugu yako Venus Star kule utakapokwenda.

Ndugu zangu wana JF tumuombe ndugu yetu maana huu uteuzi ni wa mwisho kwake hatapata tena hii Golden Chance.
 
Back
Top Bottom