Nashauri Rais awekwe mbali au apunguziwe access na mitandao ya kijamii

Yupo sawa kabisa, si wananchi au wadau wote wanaweza kumuona na kumshauri, hii nchi sio yake ni yetu, hivyo kama anasoma na kupitia anaangalia matatizo ya wananchi wake, nyie vipi mmezoea kutawaliwa kwa amri ndio mmeshazowea, yupo sawa kabisa kwa maana hiyo anaangaliwa raia zake wana shida na manunguniko na wanataka au kupenda nini.

Karne hayo ya mwaka alikuwanayo waliopita. Bora huku kwenye mitandao kuliko Ikulu iliyojaa wajumbe, wajumbe si watu wema au hulijui hilo.
 
Hii ni mwaka 2021 na si mwaka 47 fungua macho uione dunia ya leo.
 
Wewe unatumia nini wakati huu? Yaani mnataka wananchi wawe updated na teknolojia lakini viongozi wabaki analojia?
 
Amesahau kuna kiongozi wa kabila lake alikuwa anasoma meseji za wake za watu na kuzitoa hadharani?
 
Kile kitendo cha kuteua na Kisha kutengua Kwa muda huo huo sio Mwanzo mzuri

Na sasa kama Rais wa nchi, haipaswi ipite hivihivi hiyo, waliochangia kuhusiana na hilo, wakamshauri vibaya Mh Rais, aondoke nao, hii itafanya kitengo cha ushauri wa Rais, kijue kwamba, Wao ni washauri tu, Raisi ni mmoja tu
 
Mleta mada naona unazingua, na sisi hatutachelewa kukuzingua.

Muacheni Mama achape kazi mambo ya kutafuta kiki na kufokeana yalishapitwa na wakati
 
Mkuu ukigoma kwenda sawa na mabadiliko basi mabadiliko yatakufosi uende nayo sawa, hamna cha ajabu hapo aisee kusingekuwa na mitandao hata ulichoandika ungefanyaje?
 
Mafashisti anga limewakataa
 
Huko ndiko tunakotoa ya moyoni zaidi bila woga, ni vyema ukawajua vyema unaowaongoza itakusaidia sana. Hata mwenda zake alikuwa anakesha huko.
Tena ya moyoni yasio na chembe ya unafiki,wala hofu ya kusakwa kama ilivyo kuwa hapo awali,japo haikuwa yote iliyowaficha wachangiaji. Kwa jf sikuwahi kuwa na shaka, tuendapo Naona unafiki uliotokana na hofu ya kusakwa kwa kuonge utatoweka kabisa.
 
Mzee msindikize mwendazake tu...huwezi kuikimbia technology..
 
We upo dunia ipi? huko mitandaoni ndo kuliko na hao wananchi au umezoea wale waigizaji wa barabarani kujifanya wanatoa kero huku wamegeuza mashati, hahahaha Mama akiendelea hivi wallahi 2025 napiga kula ccm kwa mara ya kwanza tangu nazaliwa.
 
Daaa unaweza Kuta mama nae ni memba humu JF na fake ID na akitoa hoja tunamzodoa hahaha

All in all mitano tena
Au nasema uongo ndugu zangu
 
Sina shida na yeye kufuatilia reaction ya wananchi mitandaoni..tatizo tu majority ya wachangiani hapa bongo hawajui hata duniayao inaendaje.
 
Kuna mambo mawili.
MOJA HUWEZI BADILI LOLOTE
PILI HATA SAMIA AKIACHIA MADARAKA JPM HATORUDI.

USHAURI: KUBALIANA NA HALI.
 
Yule mwingine, mwenda zake alitaka kuzuia kabisa mitandao, magazeti, macho msione(You Tube)!
Zama zenu mmekwisha kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…