Nashauri Rais awekwe mbali au apunguziwe access na mitandao ya kijamii

Nashauri Rais awekwe mbali au apunguziwe access na mitandao ya kijamii

Mkuu huu ubabe wa kunyimana taarifa kuna watu wananufaika nao,
ila uzuri digital age haibahatishi na internet never forgets
Mama akichanganya teule zake na opinion za humu anaweza kuja na combination ya viongozi wazuri walio neutral.
Kabisa
 
Mimi nadhani asiwe mbali na mitandao ya kijamii Bali aangalie na aina ya mitandao.
Kweli Twitter imekua ikitumika kwa viongozi walio wengi lakini angekua na account hapa jamii forum angepata maoni yalio iva.

Maana hapa wako watu wa aina mbali mbali wanaona mengi na kuyasikia lakini wasingependa kujulikana wanapotaka kutoa ushauri.

Pia hapa kutukanwa sio rahisi Kama huko Twitter kwa sababu hapa Kuna mods wanaweza kuzui au kufuta lugha mbaya kwa rais.

Kwa ufupi apite kote lakini jamii forum asikose.
 
Opinions nyingi za mitandaoni zinatolewa kwa malengo ya vukundi flani,

Ukifuatilia sana mambo ya mitandaoni itakua ngumu kufanya maamuzi binafsi, tutakua tunaongozwa na opinions za watu badala ya maamuzi ya kitaasisi,

Nimeandika kwa lengo jema tu, ushauri huu unaweza usizingatiwe pia.

Maamuzi ya kitaasisi si ndo hayo yalipeleka jina mkurugenzi wa taasisi nyeti mama? Mama baada ya kumjua zaidi kupitia social media akaamua kupindua uteuzi! Bado hujaona umuhimu wa mitandao?

Ukizumngumzia makundi ni kweli kwenye mitandao yapo, ila pia hata huko kwenye vetting organs kuna makundi pia. Ni swala la ku balance towards haki na facts.
 
Unaweza ukaliweka hivyo na ukaeleweka na baadhi ya watu ila lengo langu ni kumpa muda wa kuwa na maamuzi binafsi yasiyotokana na influence nyingine hasa wakati huu anapoanza kufanya kazi.

Huko mbeleni haina shida ila kwa sasa itamfanya asiwe na misimamo yake binafsi na watu watashindwa kuielewa misimamo yake yeye mwenyewe.
In order to make right decision you must be informed. Atakuaje informed kama hapitii maoni ya watu wake?
 
BAVICHA sio Raia? Huu ujinga wa kuamini watu wenye Imani tofauti kisiasa hawana haki za msingi kushiriki mema ya Nchi yanakifanya Chama Tawala kizalishe Vijana wajinga wajinga wanaosubiri Viongozi wafikirie kwa niaba yao.

Siku za Nyuma TANU/CCM ilikuwa ikizalisha Vijana wenye tija kwa Taifa, siku hizi inazalisha Vijana wenye tija kwa Viongozi wao, tena kimakundi. Wewe ni mfano mzuri wa kizazi cha sasa kwenye Chama.
Yaani feedback ya bavicha ndio unaona feedback ya raia? Mitandaoni wamejaa bavicha...
 
Kwa mtazamo wangu ili kumuwezesha kufanya maamuzi akiwa na fikra huru wampunguzie access au kumuweka mbali na mitandao ya kijamii.

Lisipofanyika hilo utendaji wake utaathirika pakubwa kwani maamuzi yake yanaweza athiriwa na opinions za watu ambazo kwa namna moja au nyingine zinaweza zisiwe sahihi.

Kwa siku hizi chache hilo ni jambo ambalo nimeona ni muhimu kufanyika na wasaizidi wake.

My few cents.
Mmmh sidhani kama itakuwa sawa, urais ni taasisi na sio kila kitu kilichopo mitandaoni hakifai, sometimes kuna issues za msingi tu na sometimes kuna whistleblowers wazuri tu ambao wanaweza kuisaidia taasisi ya urais kuyajua mambo mengi tu.

Kwa sasa suala la social media sio la kukwepa ila ni kujua namna ya kuishi nalo tu. Kumbuka hawa wanaoongea kwenye social media ni raia wenye nia nzuri ila hawana access ya kufikisha mawazo yao direct kwa wahusika.

Sema tu tatizo linakuja pale baadhi yao wanapokuwa na lugha za matusi au kuzusha uongo, hapo wapokea taarifa wanatakiwa kuwa makini kuchambua yaliyosahihi na yale ya hovyo kuyaacha.
Mimi nafurahi ninaposoma twits za mh.

Rais hii inaonyesha anajua umuhimu wa social media na anajua kinachoendelea huko. Narudia tena hatuwezi kukwepa social media ila tunatakiwa tujue namna ya kuishi nazo.
 
Swali vipi unaweza ishi pasipo kujitazama kwenye kioo?
Kiongozi makini hawezi jitenga na mitandao.Mitandao ni sauti ya watu.Mitandao ni kioo pasipo kioo taifa litaanguka.
 
Kwa mapema namna hii Rais wa Nchi kutegemea mitandao ya kijamii kutoa maamuzi ni janga...!

Rais ni taasisi inayopaswa iwe imara na isiyoyumba kwa maamuzi yake.Rais kutamka eti amelala saa 10 kwa sababu alikuwa anafuatilia mitandao ya kijamii inasema nini kuhusu uteuzi wake ni AIBU YA KARNE!

Kwa hakika ya nafsi yangu naanza kuingiwa na mashaka kumhusu kiongozi wetu huyo mpya hasa kwa yeye kutegemea mijadala isiyo rasmi kuamua kipi afanye.


Mungu ibariki Tanzania!
 
Akizingua Sir God anamuondoa , mi sina was was naongeza Tu popcorn
 
Uyo anavofanya mbona kawaida, Kuna kiongozi alikw anatoka usiku kupita majumbani kimyakimya kusikiliza manunguniko tu, kisha anajua watu wake wanataka nn.
Raisi lazima awe msikivu, na karne hii watu wanaongeza mitandaoni. Kwahiyo hana kosa hapo zaidi ya kutekeleza wajibu wake.
 
Back
Top Bottom