Nashauri Rais awekwe mbali au apunguziwe access na mitandao ya kijamii

Nashauri Rais awekwe mbali au apunguziwe access na mitandao ya kijamii

Mimi sidhani kama anaweza kusoma kitu mtandaoni halafu akakibeba hivyo hivyo.
Lazima atafanya uchunguzi wake kujiridhisha.

Na sio kwamba ndio anategemea mtandao as a main source.Naamini hii ni mojawapo tu kati ya njia zake nyingi kupata taarifa na kushauriwa.

Inawezekana pia haya ni maamuzi ya system yake na wanamsaidia kuhakikisha anapata anachotaka na sio kwamba ni yeye mwenyewe yuko mtandaoni full time au kwamba yeye personally ndio anaendesha zile accounts zake.

Inawezekana pia uwepo wake mitandaoni unaleta mtazamo fulani kwa jamii ambao in turn unaipa system feedback fulani wanayoitaka kirahisi tofauti na kama wangejificha na kutokuwa public.

Pia pre emptying ni mojawapo ya faida inayoweza kupata system ya mama kwa wao kuzoeleka mitandaoni kama hivi.(kama una idea ya intelijensia utanielewa hapo).

System inabadilisha mbinu kila wakati kulingana na mahitaji ya wakati kwa namna wao wanavyotaka kuendesha nchi.

Hivyo hata baadhi ya tabia kiongozi anafundishwa kuziadopt ili awe na taswira fulani katika jamii kwa wakati fulani na sababu fulani.

Nikudokeze tu kwamba sio mama pekee aliyeingia mtandaoni,viongozi wa serikali ya awamu ya sita wengi wameanza kuwa very active mitandaoni.

So nadhani this is planned na system iko aware na huenda ndio architecture wa hili kwa sababu wajuazo wao.
Sipingi dhana zako moja kwa moja maana una hoja za msingi, na maangalizo yenye mantiki. Lakini matumizi ya mitandao ni mambo ya wakati, na yoyote anayetumia mitandao anafikia jamii kwa urahisi kuliko anayetumia njia nyingine yoyote. Hili la mama kutumia mitandao ni utashi wake binafsi na sio ushauri wa system, labda system nayo iadapt kwenye matumizi ya mitandao, lakini sio jambo planned na system.

Alichofanya mama ni kuachana na siasa za mtangulizi wake za chuki, akamua kuongea lugha ya maridhiano zaidi, ndio maana Kawa rafiki humu mitandaoni. Kama ingekuwa ni jambo planned na system, Dr.Mpango, Mwigulu nk wangepata mwitikio chanya kama wa mama.
 
Magufuli was good mitandaoni alikuwa anapita mwenyewe na kufahamu mambo mengi na ikawa ngumu kwa wasaidizi wake kumdanganya.

Mama amerithi utamaduni huo na anashiriki kwa kutweet kabisa.

Huu ni utamaduni mzuri,unamuwezesha kuwa karibu na raia na kupata feedback ya kinachoendelea ground.

Naamini kabisa wasiotaka Rais na wasaidizi wake wa karibu kutumia mitandao wana nia mbaya ya kumweka Rais viganjani wamwendeshe wanavyotaka wao,wamwaminishe yale wanayotaka wao na kumshauri mnayotaka nyinyi.

Acheni mama ajivinjari mitandaoni,msimpangie.

La jana limewaumizeni sana mataga,mnataka kumcontrol Rais,haiwezekani.Acha awe huru.
Tofaufi na Mama, baba yetu hakufanya maamuzi yake kwa ushauri wa kutoka mitandaoni na mara nyingi alifanya kinyume kabisaa! Hii ilitokana na umahiri wake binafsi ktk kufocus kwenye vipao mbele vya serikali yake pasipo kuyumbishwa! Sasa kama mama hata kuwa na talent hizo, kuyumba atayumbishwa sana na mapopoma wa mtaa wa ufipa!
By the way, kama anataka kujua wananchi wake 2nataka nini yy aje mtaani atutembelee ndio watu tutamtiririkia tunayoyataka! Sio kukaa na smartphone akipita mitandaoni na kujiaminisha kwa uvivu kuwa ndio maoni ya watz! Rais wetu sio rais wa mtandaoni😡! Atafanana na akina Zito na Mbowe na saccos zao za mitandaoni! Uhalisia upo mtaani, yy mama atoke aje kutusikiliza ataelewa wananchi wake watakalo! Sio hawa washinda mitandaoni tu huku wakisubiri kuitwa chakula kimeiva mfyuuuuuu 😡!
 
kwa kweli ajilimit muda wa kuingia mitandaoni,unaweza usilale eti na ukilala usingizi wa mang'amung'amu
 
Unayewategemea akina Kibajaji, Musukuma, Japipo, and the like, endelea nao. Lakini Mh. Rais Samia anajua kuwa wabunge ni sehu ndogo sana ua umma wa Watanzania.
 
Kwa mtazamo wangu ili kumuwezesha kufanya maamuzi akiwa na fikra huru wampunguzie access au kumuweka mbali na mitandao ya kijamii.

Lisipofanyika hilo utendaji wake utaathirika pakubwa kwani maamuzi yake yanaweza athiriwa na opinions za watu ambazo kwa namna moja au nyingine zinaweza zisiwe sahihi.

Kwa siku hizi chache hilo ni jambo ambalo nimeona ni muhimu kufanyika na wasaizidi wake.

My few cents.
Samia hua hakaachi ka iPhone6 kake
 
M
Kwa mtazamo wangu ili kumuwezesha kufanya maamuzi akiwa na fikra huru wampunguzie access au kumuweka mbali na mitandao ya kijamii.

Lisipofanyika hilo utendaji wake utaathirika pakubwa kwani maamuzi yake yanaweza athiriwa na opinions za watu ambazo kwa namna moja au nyingine zinaweza zisiwe sahihi.

Kwa siku hizi chache hilo ni jambo ambalo nimeona ni muhimu kufanyika na wasaizidi wake.

My few cents.
Mwesiga unaendeleaje?
 
Mama yuko vizuri acha apige kazi ili 2025 akipewa nafasi ya kugombea azoe kura za vyama vyote,naamini itakua hivyo.
Vyama vingine vipo mitandaoni tu kitaani avipo.
Mungu mbariki Rais wetu Samia suluhu.
 
Back
Top Bottom