Nashauri safari za mabasi kutembea saa 24 zisitishwe, vifo vitamaliza watu

Habar za kishamba unaleta izo aisee,ajal mda wwote tu ule acha watz wafurarah maisha na safar za usiku hasa wafanya biashara imesaidia sana pia imetoa ajira nying sana kampun zimeongeza mabus drivers wamepata shavu conductors pia wakisitisha watu wataenda wap maana safar zitapungua kutokana na mda wa kukaa barabara hmna so acha ushamba huo na kimbelembele ahadi ikifika imefika halafu ajar haina muda mzee so acha ushamba
 
Sometimes we need to risk.
Maisha kama yapo,yapo tu.
Kikubwa ni kuwa na Imani ya safari kuwa nzuri,vinginevyo tutarudi nyuma.
Nafikiri itafutwe namna ya kuboresha.
Ushauri: Kila baada ya Km 50 pawepo na ukaguzi,lakini pia ifungwe mifumo ya ufuatiliaji wa Magari na mwisho Magari yote ya safari za usiku yafanyiwe maalumu.
 
Mmeanza kuomba pooo?

Si tulisema humu lakini haikueleweka?!

Learning by mistakes is very cost ful
 
Ndio maana tunasema safari za usiku sio tatizo bali madereva wa kuendesha kwa kuchukua tahadhari ndio shida kuwapata katika Nchi hii !!
Na baadhi ya matajiri wa mabasi hayo wanafurahia mabasi yao yanapofika mapema sana huko yaendapo hivyo huwa hawawakatazi madereva wao kwenda mwendo wa kasi !!

Vinatakiwa vidhibiti mwendo kwenye mabasi !
Basi lisiwe na uwezo wa kukimbia zaidi ya 80 kph !
Na iwekwe sheria ya kifungo kwa atakaye kiharibu kidhibiti mwendo kwenye Basi !
 
Hata hivyo ni enforcement kuimarishwa na elimu ya usalama barabani kwa wote abiria na madereva.

Maana hata mchana ajali zinatokea nyingi tu .
 
Usiku safari ziendelee lakini enforcement , ukaguzi wa magari , elimu itolewe mara kwa mara.

Na maeneo ya mijini kufungwe CCTV Cameras
Tutakuwa Taifa la watu wa ajabu wa kushikiwa akili kiasi hicho kwamba dereva asiweze kujitambua kuendesha gari kwa usalama bila shuruti?!
 
Je zile ajali kibao za mchana kweupee una maoni gani
 
Ni kweli service huwa ina ratiba(schedule)

Niliwahi kuona service tag kwenye gari fulani iliandikwa service imefanyika (mf 234300KM halafu itafanyika tena 235300KM)

Ukiangalia hapo ni baada ya mileage fulani ndio service itafanyika.

Pia service inaweza kufanyika kwa dharura ikitokea.
 
Mkui wewe ulijuaje kama gari halina service?
Ulikagua nini na nin?
 
Uko Sahihi 💯 kuendesha gari usiku kunaitaji uzoefu mkubwa na umakini Kwa Sababu usiku sio mchana sababu zilizopelekea kuruhusu safari hizi ni za kibiashara Zaidi sio kiusalama wewe fuatilia maeneo mengi kama utaona trafick usiku au tochi usiku ni uhuru wa manyani TU.
 
Bado kuna uzembe katika usimamiaji,inaweza kuwa ni kweli kuna udhaifu kwa madereva lakini pia inaweza kuwa kuna uzembe kwenye mamlaka za usimamizi....
Kwahiyo Mkuu gari imetembea Kilometres 1,000 ikifika hamna kuikagua ngoma isambe, ndio hiki unachojaribu kutuambia wewe unayemiliki gari?
 
Sheria zetu kwenye adhabu ya uzembe wa kupelekea upotevu wa maisha au ulemavu wa kudumu ni butu.

Imebaki kuwatishia kuwafutia leseni tu basi.

Sasa kufutia leseni kuna noma gani kwa mfano?

Maisha mbona huendelea shega tu !
 
Si mlitaka ruti za usiku
Haya hizo hapo
Mnalialia nini tena,wabongo tatiZo
Hamjuwi mnataka nini!

Ova
 
Karibia nchi zote usafiri ni masaa 24. TUAMKE
Natamani pamoja na hoja yako hi usleze kidogo kuhusu mambo yafuatayo;
1. Miundombinu inaruhusu?
2. Mamlaka zinakuwepo barabarani usiku?
3. Watanzania wanaweledi na wanautumia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…