Nashauri serikali ipige marufuku homework kwa watoto wa shule

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Kwa mtazamo wangu, homework ni ushahidi kuwa walimu wameshindwa kutimiza wajibu wao. Mtoto akiwa shule anatakiwa amalize mambo ya shuleni hukohuko. Akirudi nyumbani awe na majukumu mengine ya nyumbani ili akili zake zitanuke katika vizio vyote.

Mbaya zaidi ni likizo. Likizo maana yake ni mapumziko. Sasa kuna ujanjaujanja wa wa shule za kisasa kumrundikia mtoto mafurushi ya vitini wanaita HOLIDAY PACKAGE. Hii ni ishara pia hwajiamini kama mtoto waliyomfundisha yamekaa. Mtoto aachwe arelax likizo ndio maana ya likizo. Hakuna tunakowahi.

Tuache amsalimie babu, ajichanganye na wenzake, ajifunze kupika, bustani,ujasiliamali kidogo na kazi za nyumbani.

Ni hayo tu.
 
Mimi niliishia darasa la nne, kiingereza hakipandi hata robo. Anarudi kijana akiwa na rundo la homework za kiingereza, alafu eti natakiwa nimsaidie. Sikumlipia ada ili aje kunitesa asee!

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Mkuu uko sahihi. Kama muda wa masomo hautoshi, waongezewe mambo ya shule mtoto ayamalizie hukohuko, asijekusumbua wenzake huku.

Wanawawahisha watoto wapi, mbona sisi tulifaulu shule za kayumba bila hizo mikogo. Nakumbuka tukitoka shule, ni michezo, na ujasiliamali kidogo kupata pesa ya kununua vitumbua. Usiku koroboi mafuta budget ni kulala mapema hakuna mbwembwe za homework.

Mashule mengi yanabrainwash watoto waonekane kama hawaelewi hadi waibe muda wao wa kupumzika nyumbani wautumie kama wako shuleni kumbe wako nyumbani.
 
Hii ndio sababu ya familia kuporomoka. Maana hata mzazi aliyekulia homework akifika kazini anajipa homework ya mambo ya kazini badala kutumia muda huo kukaa na familia. Familywork.
 
Students are easy to forget so to give them honework is the best way to remind their memories and moments of school so we have to do it to improve our education
Kuna ushahidi au hofu za kujitengenezea.
Mbona hawasahau games, movie wasahau mambo ya shule, inawezekana walimu ndio shida sio watoto.
 
Kwa mtazamo wangu, homework ni ushahidi kuwa walimu wameshindwa kutimiza wajibu wao. Mtoto akiwa shule anatakiwa amalize mambo ya shuleni hukohuko. Akirudi nyumbani awe na majukumu mengine ya nyumbani ili akili zake zitanuke katika vizio vyote.

Mbaya zaidi ni likizo. Likizo maana yake ni mapumziko. Sasa kuna ujanjaujanja wa wa shule za kisasa kumrundikia mtoto mafurushi ya vitini wanaita HOLIDAY PACKAGE. Hii ni ishara pia hwajiamini kama mtoto waliyomfundisha yamekaa. Mtoto aachwe arelax likizo ndio maana ya likizo. Hakuna tunakowahi.

Tuache amsalimie babu, ajichanganye na wenzake, ajifunze kupika, bustani,ujasiliamali kidogo na kazi za nyumbani.

Ni hayo tu.
Cha kwanza wazaz ndio wanakimbia majukumu yao kwa Zama hizi.
Mtoto kuanzia mwaka 0 hadi 5 ni jukumu la mzaz kumfundisha mtoto lugha,Na utambuzi Wa vitu mbali mbali na matendo,lakin Leo mtoto miaka 2 teyar yuko huko mnakokujua.

Kuanzia miaka 6 anatakiwa awe chekechekea hapo anakuwa anajua kila kitu Na nini anatakiwa kufanya

Kuanzia miaka 7 hapo ndio anaanza la kwanza

Swala la homework si kwamba walimu wameshindwa Bali wana wakumbusha wazaz majukumu yenu kwa watoto wenu

Ukiwa kama.mzaz lazima uhakikishe mtoto wako swala lake la elimu liko vizur

Ndio maana watoto Wa Wa Leo nidhamu hawana sababu ya wazaz mwalimu Ana asilimia 25 ya masaa 9,masaa yote 15 unayo mzaz Na mwanao
 
Wazazi wengine bana... hata homework inakupa hasira!!!
Binafsi napenda mwanangu anapo kuja na hm work...hapo najifunza kupima uelewa wake.. maana unaweza ona Mtoto ana excellent kumbe haelewi kitu.... Holiday package nayo humsaidia asisahau....huwa natoa copy nampa anachezea mwisho nampa ile original afanyie kazi.....

Wengine wanapinga tution wengine hm working tena jamani!!!
 
Dah na zimekuwa ngumu hizo kuna muda mpaka unagugo nako kanaona😂😂😂.....

Aiseee kuna haja ya kurejea namna ya elimu yetu aiseee
 
Cha kwanza wazaz ndio wanakimbia majukumu yao kwa Zama hizi.
Mtoto kuanzia mwaka 0 hadi 5 ni jukumu la mzaz kumfundisha mtoto lugha,Na utambuzi Wa vitu mbali mbali na matendo,lakin Leo mtoto miaka 2 teyar yuko huko mnakokujua.

Kuanzia miaka 6 anatakiwa awe chekechekea hapo anakuwa anajua kila kitu Na nini anatakiwa kufanya

Kuanzia miaka 7 hapo ndio anaanza la kwanza

Swala la homework si kwamba walimu wameshindwa Bali wana wakumbusha wazaz majukumu yenu kwa watoto wenu

Ukiwa kama.mzaz lazima uhakikishe mtoto wako swala lake la elimu liko vizur

Ndio maana watoto Wa Wa Leo nidhamu hawana sababu ya wazaz mwalimu Ana asilimia 25 ya masaa 9,masaa yote 15 unayo mzaz Na mwanao
Kwamba Homework ni kwa ajili ya kuwalea watoto vyema!!!!?yani tabia njema zinatengenezwa na bidii ya mzazi katika kumsimamia mtoto wake Homework?kweli!!!!!
 
Mkuu uko sahihi. Kama muda wa masomo hautoshi, waongezewe mambo ya shule mtoto ayamalizie hukohuko, asijekusumbua wenzake huku.

Wanawawahisha watoto wapi, mbona sisi tulifaulu shule za kayumba bila hizo mikogo. Nakumbuka tukitoka shule, ni michezo, na ujasiliamali kidogo kupata pesa ya kununua vitumbua. Usiku koroboi mafuta budget ni kulala mapema hakuna mbwembwe za homework.

Mashule mengi yanabrainwash watoto waonekane kama hawaelewi hadi waibe muda wao wa kupumzika nyumbani wautumie kama wako shuleni kumbe wako nyumbani.
Darasa 40
Darasa 200
 
Wazazi wengine bana... hata homework inakupa hasira!!!
Binafsi napenda mwanangu anapo kuja na hm work...hapo najifunza kupima uelewa wake.. maana unaweza ona Mtoto ana excellent kumbe haelewi kitu.... Holiday package nayo humsaidia asisahau....huwa natoa copy nampa anachezea mwisho nampa ile original afanyie kazi.....

Wengine wanapinga tution wengine hm working tena jamani!!!
Kwa nini home work?
Unadhani kwa nini mambo ya shule yasiishie shule. Maana bado ataenda tena kesho yake.
Huwezi kumpima kwa aliyojifunza hukohuko shuleni.

Nyumbani apimwe kwa shedule za homework, schoolwork sibaki hukohuko.
Mtoto akue multidimensionally. Shule ni asilimia ndogo sana la hitaji la mtoto kama unataka awe na tija.
 
Kwamba Homework ni kwa ajili ya kuwalea watoto vyema!!!!?yani tabia njema zinatengenezwa na bidii ya mzazi katika kumsimamia mtoto wake Homework?kweli!!!!!
Muda Wa kuangalia mambo ya ushoga katika TV Na vitu vya hovyo yuko katika homework,homework ina maana kubwa sana si kuandika Na kupiga mahesabu Na kuchora vikatuni ni Chakula kizuri cha akili cha mtoto
 
Sasa hata akirudi nyumbani kusalimia nyie wazazi mnaweza hata kulea watoto wenu?
Watoto kutwa unapishana nao kwenyebanda za kubani movie, na miziki tu, kuchukua smartphone za dada zake na wazazi wake kujipiga picha, wengine likizo wanatumia vizuri kuingia kwenye ngono tu, kwani haya hamuyaoni huko mtaani?,

Hizo ni jitihada tu walimu kumfanya angalau mtoto ajishughulishe asijiachie sana, .

Hivi mtoto wako asipopewa home package mwalimu ananufaika na nini? Anaweza asimpe kazi yyt lakini anafanya hivo kumsaidia tu mtoto wako ili kutwa asibaki kwenye Tv mchana kutwa
 
Wewe unayeongea haya ni mwalimu ama umesomea ualimu. Kama ni ndio rudi chuo ila kama sio nakushauri fanya mambo menginebo ya taaluma yana wataalam.wake.ova
 
Back
Top Bottom