Nashauri somo la physics liwe option kuanzia form one, mathematics liwe option pia

Nashauri somo la physics liwe option kuanzia form one, mathematics liwe option pia

Ni mawazo yangu tu, but kipi kifanyike unadhani kupunguza zero za Mathematics na physics? Unaonaje? Tunakwama wapi ku-implement system hiyo iliyoko India?
Zero zisitufanye kuache kusisitiza umuhimu wa Maths. Nadhani tuweke sheria kali na ikiwekwa watu wataweka juhudi katika maths. Siamini mtu kutopata angalau D ya maths Form Four kuwa anaweza kuwa makini katika profession yoyote baadaye
 
Ni mawazo yangu tu, but kipi kifanyike unadhani kupunguza zero za Mathematics na physics? Unaonaje? Tunakwama wapi ku-implement system hiyo iliyoko India?
Ni kuyawekea mkakati kabambe tu masomo hayo. Kwa nini iwe Tanzania tu na sio nchi zingine?! Unataka kusema nchi zingine wana akili kuliko Watanzania? Mungu alituumba wote na akili sawa, isipokuwa kuna mahala tumelega!
 
Au mwalimu mpwayungu village unasemaje?

Hii ni thathmini fupi ya masomo ya physics na mathematics kwenye matokeo ya form two yaliyotoka juzi.

1. PHYSICS
A - 0.4% (2,519)
B - 0.77% (4,874)
C - 4.73% (29,851)
D - 12.30% (77,586)
F - 81.79% (515,734)

2. MATHEMATICS
A - 1.96% (12,389)
B - 1.35% (8,532)
C - 4.84% (30,674)
D - 8.41% (53,246)
F - 83.44% (528,344)

Tatizo ni nini?
Je nani alaumiwe? Serikali? Wazazi? Walimu?..

Mwanafunzi anaingia form one huku uwezo wake ukiwa mdogo sometimes hata kusoma hajui, tukianza kuwashushia zigo walimu wa primary kwamba hawaandai watoto vizuri wanaweza kuja na hoja chanya nyingi tu juu ya kwanini watoto wanapandishwa wakiwa na uwezo mdogo.

Mtoto anapandishwa secondary baada ya kupiga chabo akifika anakuta mambo ni tofauti na magumu mnoo,

Nyie ni wazazi mnaweza kutoa ushuhuda humu, kwa waliomaliza form four before 2010, je ulianza kutumia simu lini? Sasa hivi wanafunzi wote wana simu tena wengine Kali kuliko walimu wao, suala la sex ndio usipime vijana wa siku hizi wameanza mapenzi primary ubongo umeshavurugika saana.

Turudi kwenye mada husika,

Kiukweli physics au Mathematics is not for everybody nitapinga saaana labda uje na hoja nzito sana inafaa mtu atulize akili aweze kuyamudu na kufaulu haya masomo.

Naiona juhudi ya serikali kuajiri walimu wa masomo hayo tena hao walimu wakiwa bora sana, lakini wanakuta nature ya watoto husika imeshabadilika mentality ya kusoma na kuyapenda hayo masomo hamna, ukisema uwachape serikali nayo inakuja juu.

O-level nimesoma tuition ya physcs na mathematics kwa mwalimu mmoja maarufu pale mwanza Michael mnyama pale ubungo secondary, jamaa alikua anapiga fimbo vibaya mno usipofanya kazi aliyoiacha ndio kilichonijenga nikaiva kidogo.

Nashauri serikali haya masomo mwanafunzi apewe choice ya kuchagua kuyasoma tokea akiwa form one, ili wale wanaojitambua wachache wapate fursa ya kuyaeelewa na kufanya vizuri, kuliko kujaza darasa wanafunzi 200 na wengine wakiyakataa kabisa hayo masomo wanasubiri form three wayakimbie. Kwanini yasiwe option kuanzia form one?
Imagine mwalimu wa mathematics au physcs akichukua wanafunzi wake 30 form one mpaka form four hakika hutokuja kuona matokeo mabovu ya Mathematics au Physics.

Ndio maana walimu wa chemistry na physics form four wanafaulisha sana kwa sababu form two wameshajichuja.

Nilikua naona matokeo ya st Francis waliofanya mtihani ni 92, miaka yote wako hivyo hivyo hawapungui wala hawaongezeki unadhani kwanini? Pale interview wanafanya hata 1500 but wanataka cream yao 92 tu, hakuna slow learner anaesoma pale.

mpwayungu village unaonaje wewe? Au wewe ni mwalimu wa history na language? 😁😁
Mkuu naona uko sahihi kabisa.
Kuna aina takribani tisa za u-genius(shule inadili na u-genius mmoja tu uwe na rational reasoning na uwezo wa kukumbuka ulivyosoma basi) kuna watu wanazaliwa natural wakiwa na u-gineus wa
mathe japo unaweza ukafundishika sisi tunakazana kila mtoto awe anaweza vyote ambavyo
mfumo wa elimu umeweka nadhani Albeit Einstein hatuwezi kumhukum samaki ni mpumbavu kwa
kushindwa kupanda mti yeye muweke ziwani/baharini ataogelee.
Maywether ndio mwanamichezo anayeongoza kwa pesa nyingi ila hajui kusoma wala kuandika, nchi ndogo kama equdor inashiriki kombe la dunia mara kwa mara ila TZ yenye 60 mil hata afcon ni kudra.
Maana yake tunaweza kuwa na watoto wachache wanaosoma hizo physics and mathematics na tukawekeza nguvu
kwao ili waje kuwa bora zaidi au tuendelee kupambana kila mtu ajue quantum physic tuishie kupata wote vilaza
kuna ule msemo wa kiingereza ukikimbiza sungura wawili hutapata hata mmoja na Mzee mkapa alikuwa anapenda kusema ukiwa sungura huwezi ukapaata swala(ameoambania sana education reform).
nini kifanyike:
Elimu ya shule ya msingi ndio iwe elimu ya kusaka vipaji(u-gineus wa mtoto) mfano
kama mtoto anapenda umbea huyu secondary aende kwenye mambo ya uandishi wa habari
Ni mtu wa mahesabu huyu aende kwenye technology na technical schools
Ni mtu ana-leadership skills na mzalendo(sio ule wa kuvaa tai kama ya Madelu) huyu akienda
kwenye mambo ya uongozi atawafaa.
Ni mwanamichezo huyu moja kwa moja apelekwe shule zenye academy kama alliance kutamfaa kuendana
na mchezo wake.
Wale wanaopenda kusoma waende wakasaidie kwenye tasnia ya elimu.
Wale wabunifu nao waende kwenye shule zitakazoendeleza ubunifu wao.
Matokeo:
Tutapata viongozi bora, Tutashiriki kombe la dunia, tutakuwa na wanasayansi wazuri, tutakuwa na wanasanaa wakubwa, nchi yetu itaendelee na tutaifanya dunia kuwa sehemu bora zaidi ya kuishi.
tutakuwa tuko vizuri angalau kila sekita kwa kuendeleza vipaji vya watoto wetu wao wanataka kuwa
nani na sio wazazi au serikali inataka wawe nani.
Mtu kama Elias Kihombo(RIP) serikali ingemuendeleza alikuwa ni Tesla mwingine duniani.
NB: Huko ulaya kwenyewe sio kila mtu anajua haya ma-quantum physics au ma-intergration na algebra
btn basic mathe watasoma primary
 
mathematics haiwezi kuwa option, hilo ni somo la lazima.

Tutashindwa hata kumtuma mtoto dukani kama hesabu zitawekwa kwenye option.
Dunia nzima maths ni lazima, hata China Maths na English ni compulsory,

Rishi Sunak anataka wanafunzi UK wasome hesabu mpaka umri wa miaka 18 ingawa amepingwa sana

Hata mwalimu aliemfundisha katia neno
Lakini hesabu ni lazima tangu watoto ila wenzetu vifaa vya kufundisha hesabu wanavyo sana kuanzia toys

Sisi ni hesabu tu ndio maana watoto wanaona somo gumu tofauti na wenzetu wao hesabu wanafanya kwa watoto kama mchezo na Kadri wanavyokuwa wanazidi kuelewa zaidi

Hesabu ni ngumu kwa wengi lakini muhimu sana
Screenshot_20230108_144917_Chrome.jpg
 
Au mwalimu mpwayungu village unasemaje?

Hii ni thathmini fupi ya masomo ya physics na mathematics kwenye matokeo ya form two yaliyotoka juzi.

1. PHYSICS
A - 0.4% (2,519)
B - 0.77% (4,874)
C - 4.73% (29,851)
D - 12.30% (77,586)
F - 81.79% (515,734)

2. MATHEMATICS
A - 1.96% (12,389)
B - 1.35% (8,532)
C - 4.84% (30,674)
D - 8.41% (53,246)
F - 83.44% (528,344)

Tatizo ni nini?
Je nani alaumiwe? Serikali? Wazazi? Walimu?..

Mwanafunzi anaingia form one huku uwezo wake ukiwa mdogo sometimes hata kusoma hajui, tukianza kuwashushia zigo walimu wa primary kwamba hawaandai watoto vizuri wanaweza kuja na hoja chanya nyingi tu juu ya kwanini watoto wanapandishwa wakiwa na uwezo mdogo.

Mtoto anapandishwa secondary baada ya kupiga chabo akifika anakuta mambo ni tofauti na magumu mnoo,

Nyie ni wazazi mnaweza kutoa ushuhuda humu, kwa waliomaliza form four before 2010, je ulianza kutumia simu lini? Sasa hivi wanafunzi wote wana simu tena wengine Kali kuliko walimu wao, suala la sex ndio usipime vijana wa siku hizi wameanza mapenzi primary ubongo umeshavurugika saana.

Turudi kwenye mada husika,

Kiukweli physics au Mathematics is not for everybody nitapinga saaana labda uje na hoja nzito sana inafaa mtu atulize akili aweze kuyamudu na kufaulu haya masomo.

Naiona juhudi ya serikali kuajiri walimu wa masomo hayo tena hao walimu wakiwa bora sana, lakini wanakuta nature ya watoto husika imeshabadilika mentality ya kusoma na kuyapenda hayo masomo hamna, ukisema uwachape serikali nayo inakuja juu.

O-level nimesoma tuition ya physcs na mathematics kwa mwalimu mmoja maarufu pale mwanza Michael mnyama pale ubungo secondary, jamaa alikua anapiga fimbo vibaya mno usipofanya kazi aliyoiacha ndio kilichonijenga nikaiva kidogo.

Nashauri serikali haya masomo mwanafunzi apewe choice ya kuchagua kuyasoma tokea akiwa form one, ili wale wanaojitambua wachache wapate fursa ya kuyaeelewa na kufanya vizuri, kuliko kujaza darasa wanafunzi 200 na wengine wakiyakataa kabisa hayo masomo wanasubiri form three wayakimbie. Kwanini yasiwe option kuanzia form one?
Imagine mwalimu wa mathematics au physcs akichukua wanafunzi wake 30 form one mpaka form four hakika hutokuja kuona matokeo mabovu ya Mathematics au Physics.

Ndio maana walimu wa chemistry na physics form four wanafaulisha sana kwa sababu form two wameshajichuja.

Nilikua naona matokeo ya st Francis waliofanya mtihani ni 92, miaka yote wako hivyo hivyo hawapungui wala hawaongezeki unadhani kwanini? Pale interview wanafanya hata 1500 but wanataka cream yao 92 tu, hakuna slow learner anaesoma pale.

mpwayungu village unaonaje wewe? Au wewe ni mwalimu wa history na language? [emoji16][emoji16]
Somo la hesabu ndiyo linatakiwa kuwa msingi wa kwenda chuo chochote hata vya ufundi unesi , kilimo ,biashara, hata kujiunga kwenye majeshi pia
 
Dunia nzima maths ni lazima, hata China Maths na English ni compulsory,

Rishi Sunak anataka wanafunzi UK wasome hesabu mpaka umri wa miaka 18 ingawa amepingwa sana

Hata mwalimu aliemfundisha katia neno
Lakini hesabu ni lazima tangu watoto ila wenzetu vifaa vya kufundisha hesabu wanavyo sana kuanzia toys

Sisi ni hesabu tu ndio maana watoto wanaona somo gumu tofauti na wenzetu wao hesabu wanafanya kwa watoto kama mchezo na Kadri wanavyokuwa wanazidi kuelewa zaidi

Hesabu ni ngumu kwa wengi lakini muhimu sanaView attachment 2473846
Hiyo picha uliyoweka inapingana na hoja yako
Unaongea in general sana hesabu gani unayoongelea!?
Hesabu ya mhim ni kujumlisha, kutoa, kuzidisha na kugawanya kwa mtu ambaye hana mpango wa kwenda
kwenye matechnical, technology na science education.
Mtu umesoma public speaking, tourism, communication skills, journalist, mwanamichezo au artist Calculas itamsaidia nini kwenye real life!?
Messi, Ronaldo, Tigger wood, Maywether, Chris Brown, Celine Dion, Selina Gomez hizo hesabu zinawasaidia nini!?
kwa kuwa kasema wazir mkuu wa uingereza haifanyi kuwa yuko sahihi
 
Hesabu na physics ni common disease huwa nafarijika na nafurahi nikiangalia matokeo yangu ya form 4 na form 6 ya hesabu mm sio mwalimu lkn mpk leo hii hesabu na physics sijsahau na pia huwa nawafundisha wanafunzi

Ngoja nikuambie tatizo ni walimu asilimia kubwa hawajui hesabu wala physics wamekariri mwalimu mzuri ni yule anaejua vizuri na aliyefaulu hivyo wanaopata division 1 ndio wawe walimu
 
Watoto laki tano wanapata F? Hapa tatizo siyo wanafunzi, tatizo ni elimu inayotolewa na namna inavyotolewa. wazo langu, masomo haya na elimu yote ingefundishwa kwa kiswahili, maana yanahitaji kuelewa na si kukariri. Mtoto anatakiwa kuelewa logarithm ni nini na si kukariri zile formula. Physics ndiyo kabisa, mtu anatakiwa kuelewa concepts na si kumeza mambo.
 
Mathematics is & must be a compulsory subject.

Ukija kwetu Kenya somo la hisabati Ni lazima kwa kila mwanafunzi.

And when it comes to science subjects, a student must take at least two science subjects.For instance chemistry & physics, physics & Biology or Biology & chemistry.

Nadhani serikali zetu zinatakiwa zihamashishe Zaidi umuhimu wa somo la hisabati na science miongoni mwa wanafunzi pamoja na kuwapatia materials za kutosha zinazohusiana na hayo masomo.
 
Mmeifanyia nini dunia kwa kufanya yote hayo!?
 
Siwezi jibu swali la kipuuxi Kama hili lako.
Wewe Ni mmoja wa waliofeli masomo ya hisabati na Physics huko Tz
Nimesoma mpaka hizo quantum physics...,
Huna jibu, sijawahi kumsikia mwanasayansi mkubwa kutoka Kenya, zaidi ya wakimbiaji
ambao nina uhakika hawajawahi kutumia hizo calculas kwenye mbio zao kama pengine walizisoma
 
Mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri kamwe hawezi kushindwa Hesabu, na anayefaulu Hesabu basi na masomo mengine ya sayansi hufaulu.

kila siku watu wanalalamika kwamba mbona wasomi ni wengi lakini wanaonekana kutokuwa na impact kubwa kwenye jamii?!.

Jibu ni kwamba wengi wa wasomi hao wanapuuzia Hesabu, hivyo wengi ni wasomi wanaokariri tu, hawaumizi vichwa vyao sana katika kuchimba na kutafuta ukweli wa mambo ambapo tabia ya kufanya hivyo huambatana na kupenda Hesabu.

Hesabu ni maisha, hivyo uwekwe mkakati wa kuwalazimisha wanafunzi kupenda Hesabu.
 
Back
Top Bottom