Nashauri somo la physics liwe option kuanzia form one, mathematics liwe option pia

Nashauri somo la physics liwe option kuanzia form one, mathematics liwe option pia

Means?,maadam mtoto wako anajua coding, watoto wa kindendeule huku lingusenguse wasijue coding, upumbavu huu
Anachoongelea mkuu ni tu-base kwenye quality(ubora) sio Quantity(wingi) wanafunzi wa michepuo ya sayansi wapo
wengi kweli na huwa zinajaa kila mwaka shule za sayansi tena kwa miaka ya sasa bila kuwa na B-flat kwenda mfano PCB ni kimbembe
lakini huko kwenye kada ya afya nini kimeongezeka!? jibu ni hakuna.
Ndio wenye akili wanaangalia quality tuwe na watu wachache ambao watukuwa mathink tank kwenye sayansi kuleta
evolution mpya, wale wakawaida waende wakaajiliwe huko
 
Tatizo ni serikali kuamua beba mizigo ya watu wajinga na wapumbavu.

Ingeacha wajinga waendelee kuwepo kuliko kuwa na wahitimu wengi wasio elewa kitu
Mkuu sio wajinga sema wanakalama zao ambazo mifumo ya elimu imezificha
mfano wanamichezo, wabunifu nk. elimu ikiwa inclusive ikaweza kutambua vipaji vyao wangali
watoto wanaweza kuwa lulu kwa taifa tunaona brazil inategemea mpira kwa kiwango kikubwa
na waliuendeleza na umewatoa.
Maywether hajui kusoma wala kuandika(kwa definition yako ni mjinga) lakini hakuna profesa anayemzid kwa mefanikio tukija kwenye pesa
pengine toka ulimwengu uanze
 
Au mwalimu mpwayungu village unasemaje?

Hii ni thathmini fupi ya masomo ya physics na mathematics kwenye matokeo ya form two yaliyotoka juzi.

1. PHYSICS
A - 0.4% (2,519)
B - 0.77% (4,874)
C - 4.73% (29,851)
D - 12.30% (77,586)
F - 81.79% (515,734)

2. MATHEMATICS
A - 1.96% (12,389)
B - 1.35% (8,532)
C - 4.84% (30,674)
D - 8.41% (53,246)
F - 83.44% (528,344)

Tatizo ni nini?
Je nani alaumiwe? Serikali? Wazazi? Walimu?..

Mwanafunzi anaingia form one huku uwezo wake ukiwa mdogo sometimes hata kusoma hajui, tukianza kuwashushia zigo walimu wa primary kwamba hawaandai watoto vizuri wanaweza kuja na hoja chanya nyingi tu juu ya kwanini watoto wanapandishwa wakiwa na uwezo mdogo.

Mtoto anapandishwa secondary baada ya kupiga chabo akifika anakuta mambo ni tofauti na magumu mnoo,

Nyie ni wazazi mnaweza kutoa ushuhuda humu, kwa waliomaliza form four before 2010, je ulianza kutumia simu lini? Sasa hivi wanafunzi wote wana simu tena wengine Kali kuliko walimu wao, suala la sex ndio usipime vijana wa siku hizi wameanza mapenzi primary ubongo umeshavurugika saana.

Turudi kwenye mada husika,

Kiukweli physics au Mathematics is not for everybody nitapinga saaana labda uje na hoja nzito sana inafaa mtu atulize akili aweze kuyamudu na kufaulu haya masomo.

Naiona juhudi ya serikali kuajiri walimu wa masomo hayo tena hao walimu wakiwa bora sana, lakini wanakuta nature ya watoto husika imeshabadilika mentality ya kusoma na kuyapenda hayo masomo hamna, ukisema uwachape serikali nayo inakuja juu.

O-level nimesoma tuition ya physcs na mathematics kwa mwalimu mmoja maarufu pale mwanza Michael mnyama pale ubungo secondary, jamaa alikua anapiga fimbo vibaya mno usipofanya kazi aliyoiacha ndio kilichonijenga nikaiva kidogo.

Nashauri serikali haya masomo mwanafunzi apewe choice ya kuchagua kuyasoma tokea akiwa form one, ili wale wanaojitambua wachache wapate fursa ya kuyaeelewa na kufanya vizuri, kuliko kujaza darasa wanafunzi 200 na wengine wakiyakataa kabisa hayo masomo wanasubiri form three wayakimbie. Kwanini yasiwe option kuanzia form one?
Imagine mwalimu wa mathematics au physcs akichukua wanafunzi wake 30 form one mpaka form four hakika hutokuja kuona matokeo mabovu ya Mathematics au Physics.

Ndio maana walimu wa chemistry na physics form four wanafaulisha sana kwa sababu form two wameshajichuja.

Nilikua naona matokeo ya st Francis waliofanya mtihani ni 92, miaka yote wako hivyo hivyo hawapungui wala hawaongezeki unadhani kwanini? Pale interview wanafanya hata 1500 but wanataka cream yao 92 tu, hakuna slow learner anaesoma pale.

mpwayungu village unaonaje wewe? Au wewe ni mwalimu wa history na language? 😁😁
Ushauri wako ni sawa na kusema mtu akidaiwa deni, ajifungie Ndani ili asionekane.
Mimi napingana na wewe kwa Asilimia 100% Tatizo la msingi hapa ni miundo msingi ya kufundisha hayo masomo.
Nikupe changamoto kidogo ukafanyie utafiti; tafuta wastani/idadi ya waalimu wa shule za msingi wanaofundisha somo la hesabu, walio pata ufaulu wa angau D ya Hesabu kidato cha nne; Ukisha pata majibu, rudi tena hapa kutoa ufafanuzi kuwa TUNAVUNA TULICHO KIPANDA!!!
Mimi siwalaumu kabisa waalimu, kwani wanajitoa ilikuziba pengo la walimu wa hesabu....
 
Mkuu sio wajinga sema wanakalama zao ambazo mifumo ya elimu imezificha
mfano wanamichezo, wabunifu nk. elimu ikiwa inclusive ikaweza kutambua vipaji vyao wangali
watoto wanaweza kuwa lulu kwa taifa tunaona brazil inategemea mpira kwa kiwango kikubwa
na waliuendeleza na umewatoa.
Maywether hajui kusoma wala kuandika(kwa definition yako ni mjinga) lakini hakuna profesa anayemzid kwa mefanikio tukija kwenye pesa
pengine toka ulimwengu uanze
Nchi haiwezi endelea kwa kukata mauno, kupigana, kucheza mpira.

Nchi inaendelea kwa kuzalisha mali.
Nchi zote hupimwa kwa GDP
 
Nchi haiwezi endelea kwa kukata mauno, kupigana, kucheza mpira.

Nchi inaendelea kwa kuzalisha mali.
Nchi zote hupimwa kwa GDP
Nimesema tu-invest kwa wale wanayoyaweza na kuyapenda masomo husika nimekutolea
mfano Elias Kihombo nini amefanya licha ya kuwa amebarikiwa uwezo mkubwa katika hayo masomo
ya sayansi, ninachoongelea ni isssu ya quality(ubora) sio quantity(wingi/idadi)
Tuwe na wanasansi kweli kweli kutoka kwenye damu kama kin Eistein, Newton, Tesla wale
wengine wenye mahaba na mambo mengine na wenyewe wapewe fursa kuonyesha uwezo wao
bila shaka kila mwisho wa wiki unaangalia mpira ligi ya england na sio kusoma majarida ya wanasayansi japo
kila siku utamia vitu hivyo maana yake kila kitu tukipe umhimu unaostahili
 
Solution yako ni hipi kama mdau wa elimu? Zigo tumuangushie nani? Hali inazidi kua mbaya sana, watoto haswa shule hizi za kata uwezo ni mdogo sana.
Nimesoma PCB pale Old Moshi high school, masomo ya sayansi ili yawe rahisi yanahitaji kufundishwa kwa practical zaidi. Mimi niliipenda sayansi hapo Old Moshi, tofauti na O level kwa sababu wale walimu (physics tulikuwa na Mwl Mrusi, Chemistry Mwl mmarekani na Biology mtanzania from UDSM) ilikuwa full practice. Yule Mrusi alikuwa ni full engeneer, alifufua mpaka magari ya shule yaliyokuwa yamekufa... Alikuwa na vifaa kibao vya kufundishia.. Sijui mambo ya speed of light, sound waves, kinetics, velocities etc.. Hii mambo ya kukariri tuu newton's law of motion, archemedes principles etc haisaidii kabisa kwa sababu Kiingereza ni tatizo kubwa sana kwenye shule zetu.
 
Tatizo ni serikali kuamua beba mizigo ya watu wajinga na wapumbavu.

Ingeacha wajinga waendelee kuwepo kuliko kuwa na wahitimu wengi wasio elewa kitu
Basic education ni kwa watu wote. Wenye uelewa mzuri na wasio na uelewa wa kutosha. Haya ni maazimio ya dunia na Sisi ni signatory wa hizo protocol.
 
Ni kuyawekea mkakati kabambe tu masomo hayo. Kwa nini iwe Tanzania tu na sio nchi zingine?! Unataka kusema nchi zingine wana akili kuliko Watanzania? Mungu alituumba wote na akili sawa, isipokuwa kuna mahala tumelega!
Tuanzie na namna tunavyowapata walimu wetu, je mfumo huo unatoa walimu competent kwenye sayansi?
 
Mkuu naona uko sahihi kabisa.
Kuna aina takribani tisa za u-genius(shule inadili na u-genius mmoja tu uwe na rational reasoning na uwezo wa kukumbuka ulivyosoma basi) kuna watu wanazaliwa natural wakiwa na u-gineus wa
mathe japo unaweza ukafundishika sisi tunakazana kila mtoto awe anaweza vyote ambavyo
mfumo wa elimu umeweka nadhani Albeit Einstein hatuwezi kumhukum samaki ni mpumbavu kwa
kushindwa kupanda mti yeye muweke ziwani/baharini ataogelee.
Maywether ndio mwanamichezo anayeongoza kwa pesa nyingi ila hajui kusoma wala kuandika, nchi ndogo kama equdor inashiriki kombe la dunia mara kwa mara ila TZ yenye 60 mil hata afcon ni kudra.
Maana yake tunaweza kuwa na watoto wachache wanaosoma hizo physics and mathematics na tukawekeza nguvu
kwao ili waje kuwa bora zaidi au tuendelee kupambana kila mtu ajue quantum physic tuishie kupata wote vilaza
kuna ule msemo wa kiingereza ukikimbiza sungura wawili hutapata hata mmoja na Mzee mkapa alikuwa anapenda kusema ukiwa sungura huwezi ukapaata swala(ameoambania sana education reform).
nini kifanyike:
Elimu ya shule ya msingi ndio iwe elimu ya kusaka vipaji(u-gineus wa mtoto) mfano
kama mtoto anapenda umbea huyu secondary aende kwenye mambo ya uandishi wa habari
Ni mtu wa mahesabu huyu aende kwenye technology na technical schools
Ni mtu ana-leadership skills na mzalendo(sio ule wa kuvaa tai kama ya Madelu) huyu akienda
kwenye mambo ya uongozi atawafaa.
Ni mwanamichezo huyu moja kwa moja apelekwe shule zenye academy kama alliance kutamfaa kuendana
na mchezo wake.
Wale wanaopenda kusoma waende wakasaidie kwenye tasnia ya elimu.
Wale wabunifu nao waende kwenye shule zitakazoendeleza ubunifu wao.
Matokeo:
Tutapata viongozi bora, Tutashiriki kombe la dunia, tutakuwa na wanasayansi wazuri, tutakuwa na wanasanaa wakubwa, nchi yetu itaendelee na tutaifanya dunia kuwa sehemu bora zaidi ya kuishi.
tutakuwa tuko vizuri angalau kila sekita kwa kuendeleza vipaji vya watoto wetu wao wanataka kuwa
nani na sio wazazi au serikali inataka wawe nani.
Mtu kama Elias Kihombo(RIP) serikali ingemuendeleza alikuwa ni Tesla mwingine duniani.
NB: Huko ulaya kwenyewe sio kila mtu anajua haya ma-quantum physics au ma-intergration na algebra
btn basic mathe watasoma primary
Akili kubwa sana, comment bora ya kuanzia Mwaka.
 
Back
Top Bottom