Nashauri somo la physics liwe option kuanzia form one, mathematics liwe option pia

Ukisema wa chague wanafunzi..
Wanaingia form1 wakiwa na miaka 11_12 sikuhizi watawezaje kuwa na uwelewa wa kujua wanachokipenda au kukimudu??
 
Siasa

Wanasiasa wanataka kufurahisha wananchi,

Wazazi

Hawa ndo tatizo, wamekataa chukua majukumu yao ya kuwalinda, kuwasomesha watoto, wameiachia serikali. Serikali haijali maana mtoto wa mtu akiwa mjinga haiwahusu wao. Inawahusu wazazi ma familia ya mtoto.

Jamii

Ikitokea matokeo yakawa mabaya, jamii hulalamika kuwa wameonewa,
Serikali kwa kutaka kura, inarekebisha matokeo


NB: Serikali ikubali lawama, kila mtu alipie gharama za shule kwa mtoto wake. Serikali iwekeze kwenye ubora wa wanafunzi hata ikipata wahitimu 100,000 bora kati ya 1,200,000 kwao si kesi. Hao 100,000 waendelezwe zaidi ili chuo wamalize angalau 30,000 walio bora

Kwa kufanya hivyo taifa letu litaendelea kuwepo, sababu kuna watu bora watakaoendeleza ubora.

Kila kitu kina gharama ila mwisho wa siku lazima tukubali kuwekeza kwenye ubora
 
Kwa siku za karibuni curriculum imehama sasahivi tupo kwenye competence based, Mwanafunzi anaelewa nini, hapo nadhani ndio kuzinguana kunaanza kwa maana mwalimu anakua na content ndogo ambayo haiwafikii wanafunzi vizuri pia wanafunzi wenyewe ni viazi hawako tayari kupokea, pia ulivyosema ni kweli madarasa ya chini wapunguziwe mambo labda wataanzs kuyapenda taratibu.
 
Tunawapokea secondary wengi sana wasioweza hata kuandika majina yao kwa ufasaha, je huyu ataipenda physics na Mathematics?
 
Ukisema wa chague wanafunzi..
Wanaingia form1 wakiwa na miaka 11_12 sikuhizi watawezaje kuwa na uwelewa wa kujua wanachokipenda au kukimudu??
Mimi nikipokea wanafunzi au mwalimu yoyote akipokea wanafunzi wapya, ndani ya week naweza/ Anaweza kujua mzembe na mpambanaji.
 
Sahii.
 
Unataka kusema hesabu ni ngumu kuliko physics?
 
Nasubiri komment ya mwalimu wetu mpwayungu village

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Hiyo ndio system inayotumiwa na wenzetu walioendelea. Mtu anayefaulu vizuri ndio anakuwa mwalimu wa secondary, halafu anaendelea na masomo ya juu na hatimaye anakuwa lecturer wa university.
 
Mimi sio mwalimu ila nahisi shida ipo Kwa walimu sunajua wanaenda kusomea ualimu wakishafeli, sasa unafundishwa na mtu alopata four advance unategemea nini
Nilikuwa nasubili comment yako haya ya kwanza umekuja kama nilivyokuwa nafikiria [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo waondoe Physics na Maths wanabakishe somo la vishazi huru na tegemezi na lile la Mfekane war? Ushauri wako haufai kabisa kwenye nchi inayopambana kujikwamua. Wababe wote wa hii dunia wamefika walipofika kupitia sayansi na teknolojia... msingi wa hayo yote ni hiyo Physics na Maths. Naona waache hivyohivyo hata kama atafaulu mmoja.
 
Mimi sio mwalimu ila nahisi shida ipo Kwa walimu sunajua wanaenda kusomea ualimu wakishafeli, sasa unafundishwa na mtu alopata four advance unategemea nini
Shida ni Serikali ya CCM maana yenyewe ndo ilitunga sheria na policy ya Division 4.28 kusomea Ualimu

Mabadiliko ya Elimu yatatokea kama Serikali ikiamua acha siasa na wanasiasa waendeshe elimu yetu.

Tofauti na hapo Mungu alete kizazi kipya
 
Soma
Soma uelewe Mkuu, hatujasema lifutwe lakini liwe option tuangalie quality sio quantity
 
Physics nayoiona katika mfumo wa elimu ya Tanzania 🇹🇿 sioni msaada wake ktk kumtengeneza kijana.

Sio rahisi kuitumia hii Physics kwakua haina uhalisia , tukichukulia mfano wa mada moja ya ELECTRONICS si rahisi mwanafunzi kua Competent kwan mwanafunzi yupo ki nadharia zaid wala si kwa vitendo , unasoma kuhusu chaji paspo hata kujua ktk uhalisia chaji ni kitu gani na kinaopareti vp,


Ili walau tufike robo ya ndoto za vijana wetu ni lazima serikali ione umuhimu wa kuwekeza ktk elimu, tunahitaji kubadili mfumo wa elimu, tuachane na haya ma theory twende ktk vitendo, hii itasaidia vijana kua na uwezo wa kujiajili kulingana na taaluma zao.
 
Shida ni Serikali ya CCM maana yenyewe ndo ilitunga sheria na policy ya Division 4.28 kusomea Ualimu

Mabadiliko ya Elimu yatatokea kama Serikali ikiamua acha siasa na wanasiasa waendeshe elimu yetu.

Tofauti na hapo Mungu alete kizazi kipya
Hujui hata unachokipigania,

Vp hata walimu wa vyuo wana div 4?

Unadhani tatizo la huko juu halipo ktk ngazi za msingi na SEKONDARI?
 
Ukweli physics na Mathematics sio masomo ya kila mtu hata kama kuna walimu wazuri kiasi gani . Wanaofaulu physics au hesabu ukiachana na msaada wa tuition au mwalimu mzuri lakini mwanafunzi ana uwezo wa kujisomea baadhi ya topic mwenyewe bila msaada wa mwalimu. Hapo zamani kidogo tulijisomea baadhi ya topic na kuzimaliza na kuanza kusolve maswali bila hata kufundishwa na mwalimu.

Sasa kama ni slow learner ni ngumu kuanza kujisomea topic na kuielewa. Ni ukweli kabisa Physics na Mathematics sio ya kila mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…