Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Thread 'Huenda adui Mkuu wa utawala wa Rais Samia akawa ni Spika Ndugai?' Huenda adui Mkuu wa utawala wa Rais Samia akawa ni Spika Ndugai?Kwenye sanduku la kura 2020!! Uneelewa majukumu tarajiwa ya mgombea mwenza kwa mujibu wa katiba??
Mkuu Nguruvi3, kama kuna watu ndani ya taifa hili ambao nafasi walizoshika zinawazidi kimo ni huyo Job Ndugai. Ilikuwakuwaje hadi mtu mhuni kama huyo akazawadiwa nafasi nyeti kama hiyo...aah, eti ukada? Hebu msikilize tu anavyotamba hapa...Spika Ndugai it's time to go!
Hapo cha-chaHatakuwa na hoja ya kumshtaki Rais kwasababu keshauza 'ghala la silaha' kwa kuomba msamaha
Laiti angesimama na kauli yake pengine angeungwa mkono na mpambano ungekuwa na mantiki
Kabla ya kuitisha 'hoja hiyo'' kamati kuu itamwita na kumfyekelea mbali.
Kumbuka cheo cha Uspika hakina qualification ni fadhila tu ya chama
Heshima yake ipo sehemu moja, Ajiuzulu
baada ya hayo machache, sasa naomba tuendelee na mjadala kama Spika Ndugai anao "udhu" wa kuendelea ktk nafasi hiyo.
Ni kweli kabisa, option moja pekee iliyobaki, baada ya "kuvuliwa nguo" na Rais ni kwa Mheshimiwa Spika kujiudhuru. Full StopHuu ndio wakati wa Ndugai kujua nani ni marafiki wake wa kweli na nani ni marafiki wa wakati wa kula bata tu! Marafiki wa kweli watamshauri aachie ngazi ili kulinda heshima , lakini hao wengine watamdangaya kuwa akomae tu na angoje kusikia kwa wabunge watakaporudi kwani wanadhani wengi watamuunga mkono!! Ukweli ni kwamba hakuna mbunge atakayemuunga mkono hivi sasa watamkimbia kana kwamba ana ukoma!! Ni juu yake na wake zake watunze heshima yao kwa kumsihi ajiuzulu huo uspika kabla hawajakosa kila kitu. Hiyo ndio busara iliyoki kwake kwa wakati huu.
Ni kweli kabisa, option moja pekee iliyobaki, baada ya "kuvuliwa nguo" na Rais ni kwa Mheshimiwa Spika kujiudhuru. Full Stop
MH SPIKA JOBU NDUGAI TAFADHARI ZINGATIA USHAURI HUU Rais hana imani tena na wewe Ndugu yangu Spika. Hivyo kuna mambo mawili ambayo unapaswa kuyafanya.Kubwa zaidi ni pale Rais ambaye ni mwenyekiti wa chama anapotilia shaka ''Akili ya Spika'' hapo kuna jambo zito. Leo uongozi wa nchi umemshukia na Spika hana pa kushika tena
Pale kuna bunge kwani?Mfano akitaka iwe vita akaja na ile kuwa hatuna imani na rais? Sema sisi wananchi tutalivamia bunge nawaza kwa sauti😀😀😀
Rais SSH alikuwa 'ameghadhabika' na kauli za Spika Ndugai. Hakuwa katika hali ya kawaida..kuna mambo rais ssh ameyasema yamenishangaza kidogo.
Hili ndilo tatizo la viongozi wetu, kwamba, ni lazima azungumze 'kupendeza' hata kama kufanya hivyo ni kusema uongo! Viongozi hawana ujasiri wa kusema hapa sivyo!!...unakumbuka kauli ya Gavana wa BOT kwamba tuko vizuri deni sio tatizo?
Kaeleza ukweli kinyume na Gavana. Hivi kwani ilikuwa lazima Gavana wa BoT aseme jambo!..sasa leo rais ssh katoboa siri kwamba mh.mwigulu alimpigia simu usiku mkubwa akiwa na stress kuhusu madeni ya serikali!!
..raisi akaendelea kusema kwamba sehemu ya mkopo wa 1.3 trillion imetumika kulipa madeni / mikopo ambayo ime-mature.
Pengine Spika ana point, lakini kuna maswali mengi;..tunahitaji kuzungumzia deni la taifa kwa umakini zaidi.
Tulisamehewa na Paris Club chini ya uongozi wa PM CD Msuya.miaka michache iliyopita tulikuwa sehemu ya nchi zilizoitwa Highly Indebted Poor Countries, tukabembeleza ili tusamehewe madeni. Leo rais anazungumzia serikali kuchukua mkopo kulipia mkopo. Je, tuko salama huko tunakoelekea?
Mkuu kwa hali ilivyokuwa leo ni suala la kumwambia sasa ni 'najisi ' ...baada ya hayo machache, sasa naomba tuendelee na mjadala kama Spika Ndugai anao "udhu" wa kuendelea ktk nafasi hiyo.