Kumwondoa Ndugai ni kukata tawi ukitegemea mzizi wa uvunjwaji wa katiba na haki za binadamu utang'oka pia, lakini pia ukitegemea kupata mfumo sahihi wa uendeshwaji na usimamizi wa Serikali automatically.
Hakuna ushahidi kwamba Ndugai hakkutaka Mama aongoze nchi. La sivyo asingewapigia kampeni 2015 na 2020.
Uendeshwaji wa bunge, usiokuwa na mtengamano upo siku zote tangu siasa ya vyama vingi iingie nchini. Tofauti ni hekima na viwango vya ugandamizaji. Ndugai amefanya ugandamizaji kwa kiburi, pasipo busara, heshima wala aibu, na kiwango kimekuwa cha juu kwa kuwa huko awali hatukuona Speaker akienda mbali kiasi cha kutaka kuthibiti hata haki za kuishi za wapinzani. Mtakumbuka kipindi cha "Wanaoafiki ni wengi wameshinda..", hata pale ilipobainika vinginevyo, lakini hatukuona personal and personality attacks.
Lakini pia, ufahamu kwamba kazi ya Bunge siyo UNAFIKI wa kujenga urafiki ama kuendana na Serikali. Kazi ya Bunge ni kuisimamia serikali na kuhakikisha inatembea katika njia sahihi. Kitu ambacho mwandishi amezoea ni ile hali ya bunge kupiga makofi kila kitu kinacholetwa na serikali bila kukichambua na kukitathimini kitaalam. Labda hapa ndipo hitaji la kubadili katiba kuhusu sifa za wagombea wa Ubunge.
Kwa mtazamo wa agenda iliyoko mezani, Ndugai kama amefunguka macho na kuona kuna madudu mengi yanayofanyika ama yaliyopitishwa na bunge, ama yasiyofuata utaratibu kama ambavyo ccm imezoea akiwemo yeye mwenyewe na mihimili yote; alipashwa kuonyesha ukomavu wa kifikra, na kiuongozi.
a) Ni kweli hakutakiwa kunyamaza kwa sababu kufanya hivyo ni kuendelea kulihujumu taifa makusudi.
b) Hakupashwa kuongea mitaani kama mtu asiyekuwa na namna ya kutatua hizo ndivyo sivyo.
c) Alipashwa kupeleka agenda hizo bungeni zikajadiliwa kwa kina na yeye kama kiongozi wa Bunge, kama anavyoweze kuinfluence uvunjaji wa katiba na wabunge wasihoji, (matibabu ya LIsu, wabunge 19 wasio wateule wa rais, na wasio na vyama, n.k), bila shaka angeinfluence michango makini ya kuchambua tatizo lililopo, kiwancho chake, athari zake na suluhisho la muda mfupi na la muda mrefu. Hata kama ccm waliozoea uovu wasingempenda, Watanzania na dunia ingemwelewa sana.
d) Alikuwa na uwezo wa kukaa na viongozi wa mihimili mingine akawapa tahadhari ama akapata ufafanuzi wa hayo na kutoa ushauri yakini. Kama angeliona kuna undani usio mwema, bado alikuwa na nafasi nzuri ya kupambania haki za Watz kwa njia bora kwa sababu nafasi yake imempa access nyingi, ambazo naomba nisi list hapa.
e) Lakini pia ifahamike kwamba aliyosema, amesema mambo ya maana sana ambayo yanapashwa kuzingatiwa kama hayakuwa yakizingatiwa na diyo sababu hakuomba radhi kwa maneno aliyosema bali kwa hali iliyotokana na kusema kwake. Mwenye akili na afahamu.
f) Na kwamba si kila analolisema Ndugai, ni ofisi ya speake imesema. Kumbuka ni binadamu ambaye kama yeye anayohaki ya kuwaza, kusema na kuona kama anavyotaka bila kuunganishwa na ofisi yake. Nalazimika kuamini kwamba yote ameyazungumza kama Ndugai na si kama speaker wa bunge.
g) Visasi si mfumo wa kutoa ama kupata haki kwa jamii ya watu wastaarabu. Ndugai asishambuliwe kwa lengo la kumlipiza visasi, ama kumtweza kwa maslahi ya binafsi ya watu, bali lengo liwe kutengeneza msingi imara wa uendeshaji wa vyombo ya umma, uhuru na democrasia ya kujieleza na kutoa maoni ya watu, na kujenga Uhuru wa watu kukosoa Mamlaka zinapokosea bila kuvunja heshima ya viongozi ama kuwadhalilisha.
h) Kudhalilisha wakuu wanchi ni kuwadhoofisha na kuwafanya wasitumikie wananchi kwa morali kitu ambacho ni hasara ya kila mtu. NATEGEMEA KWA KUSEMA HIVI NITAELEWEKA SIFURAHII NA HAIFAI HATA KIDOGO pale watu wanapomtukana Mwl Nyerere, Hayati Mkapa na Hayati Magufuli bila kuelewa kwamba wale walikuwa icon za nchi yetu na kuwadhalilisha ni kudhoofisha taasis ya urais ambako mwisho wake ni dhiki kwa watu wote.
i) Ccm acheni kujigundisha kwenye taasisi ya urais kwa sababu si nafasi yenu. Sasa kwa ajili ya mambo yenu ya hila na misuguano yenu na ndani, mnataka kutuharibia nchi kwa kuanzisha marumbano na taasis ya Urais. Hatutaki. Mambo yenu huko kwenye chama lakini Serikali iacheni ifanye kazi ya kuwatumikia wananchi.