Rais ni Nembo ya nchi yetu na ni sauti halali ya watanzania wote. Kwa misingi hiyo bila kujali mawazo yangu binafsi dhidi ya Rais Samia, lakini anapokuwa anatekeleza majukumu yake kama Rais wa nchi hapaswi kubezwa na mtu yeyote hadharani. Mtu akifanya hivyo anakuwa ametudhalilisha watanzania wote tuliompa dhamana Rais wetu kutenda na kuongoza kwa niaba yetu.
Kwa hiyo mh Ndugai tumng'ang'ie na tumwajibishe ili liwe fundisho kwa yeyote mwenye mwelekeo wa kudhalilisha taasisi hii muhimu ya urais. NINAMWOMBA RAIS SAMIA ASIWASHIKE MIKONO WOTE WALIOAMUA KUMWAJIBISHA HUYU ALIYELEWA MADARAKA NA KUDHANI MAMLAKA YA URAÌS YANAPUNGUKA KAMA JINSI YA "KE" IKIWA IMEKALIA KITI CHA URAIS!!! Ndugai lazima ANG'OKE.