Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
RAIS NA KIONGOZI WA MHIMILI MWINGINE 'HANA IMANI'
SPIKA AMEPOTEZA IMANI YAKE KWA BUNGE NA CHAMA
Jana Jumatatu Spika wa Bunge la JMT Mh Ndugai alifafanua kauli ya 'mikopo na mnada wa nchi'
Spika alijitokeza baada ya 'kushukiwa vikali' na makundi ya chama na viongozi wa serikali
Spika alisema 'amenukuliwa vibaya, kipande cha video kinachozunguka si sahihi kwa alichosema'
Mwisho wa ufafanuzi ,Spika alimuomba radhi Mh Rais na Wananchi kwa ''usumbufu'' uliojitokeza bila ufafanuzi ikiwa atawachukulia hatua gani waliosambaza kipande cha video.
Mh Spika hakukana sauti ya video au kutilia shaka iwapo video imechezewa
Alichosema imepotoshwa bila kuonyesha wapi na kwa vipi.
Swali linafuata, je, alichukua hatua gani dhidi ya vyombo husika? na kwanini ilimchukua muda mrefu kujibu hoja yenye hisia kama ilivyo?
Mh Spika anasema alikuwa mgonjwa na kutoweza kujitokeza, hata hivyo ofisi ya Spika ni kubwa ingeliweza kutoa taarifa za awali ikisubiri hali ya Mh kuimarika. Hili halikutokea
Kabla ya mkutano mitandaoni kulikuwa na mazungumzo kwamba atapojitokeza atasema 'amenukuliwa vibaya' Huu ni utamaduni wa viongozi wanapokwepa kukiri au kuomba msamaha kwa matendo au kauli zao
Jumanne ya leo ndani ya Ikulu kulifanyika hafla ya taarifa ya utekelezaji wa mpango wa serikali unaohusiana na pesa za mkopo unaozungumziwa kwa utata
Viongozi wote wa serikali na chama walisomeka kwa kauli zao 'kumshambulia' Mh Spika
Mh Rais alionekana kukereka na ukweli kwamba 'taarifa za mikopo zinapita katika nyumba ' na kisha mtu anasema yaliyosemwa
Mh Rais anasema nguvu yake ni kutokana na kuungwa mkono na Wananchi katika sakata hili
Na kwamba ''wanaotazama 2025' waondoke wakajiandae vizuri
Ukifuatilia kwa undani msamaha wa Mh Spika haukupokelewa na mhimili wa serikali achilia mbali Chama chake
Mh Spika alikuwa na machaguo mawili.
Kwamba asimame na kile alichosema akiamini ni maoni yake, au
Kutoomba radhi asubiri kutetea hoja zake kwa mantiki bila kujali nini kitafuata
Kitendo cha kutochukua hatua dhidi ya ''wapotoshaji' na kitendo cha kuomba msamaha kinamwacha na chaguo moja 'Ajiuzulu'
Mh Spika atakuwa amepoteza ''vote of confidence' kutoka ''Caucus'' ambayo ni asilimia 90+
Mh Spika amepoteza 'Vote of confidence' katika Chama kufuatia matamko ya viongozi
Mh Spika amepoteza 'vote of confidence' kwa kiongozi wa Mhimili mwingine, hakusimama na kauli yake
Katika nchi nyingine hili la mihimili kutofautiana ni la kawaida, kwa nchi yetu ambako kuna mihimili imejichimbia, hili si la kawaida na linamwcha pagumu
Katika mazingira hayo Mh Spika hana pa kusimama tena kwa maana ya kwamba haungwi mkono na sehemu yoyote ya jamii japo kwa uwazi na amebaki kisiwani
Spika alipaswa kufanya alichofanya Waziri wa fedha enzi hizo bwana Edwin Mtei.
Mtei alipotofautiana na Mwl Nyerere kuhusu sera za nchi kwendana na matakwa ya IMF na WB, alijiuzulu. Miaka mingi baadaye ilibainika Mtei alikuwa Sahihi kwa maamuzi
Hadi leo Mzee Mtei anabaki heshima yake na ''role model'' ya namna gani viongozi wanapaswa kusimama na hoja zao kwa kuamini kile wanachoamini
Spika Ndugai hana uungwaji mkono ,hata kama ataendelea, kazi itakuwa ngumu sana
Kila kauli yake itakuwa sawa na kutembea juu ya miba.
Hii italiacha Bunge kupoteza nguvu zake zote kwasababu Spika ni 'symbol' ya Bunge
Mh Spika ni wakati wa Kujiuzulu, hakuna ajuaye nini kitatokea ndani ya chama chako.
Ikitokea vinginevyo aibu itakuwa kubwa kuliko ilivyo sasa.
Ni wakati ufanye tathmini na uchukue uamuzi mgumu
Jiuzulu, usimame na kile unachoamini , siyo dhambi wala kosa! ni ukomavu na ubaki mbunge
Sehemu II tutaangalia ufafanuzi wa deni na kauli za nchi duniani zinakopa
Tusemezane
Tulia Akson Mwanjala ameshaanza kupasha misuli moto.Lolote linaweza kutokea.Wadau Watanzania Wote Tumeusikia na kuutazama MPAMBANO baina ya MIHIMILI Miwili yaani SERIKALI NA BUNGE.Mpambano huo Unatokana na Serikali kuamua Kutekeleza Bajeti iliyopitishwa na BUNGE iliyohusisha UKOPAJI.
Kwa Mshangao MKUBWA Spika wa Bunge Alihutubia Wagogo Wenzake na KUIPONDA SERIKALI kwa KUKOPA na Kudai Huenda NCHI ikapigwa MNADA.Kutokana na KAULI hiyo ya SPIKA
Mh.RAIS amehitimisha MPAMBANO LEO.
USHAURI kwa SPIKA
Nichukue Nafasi kumtaka SPIKA NDUGUI Atumie UUNGWANA aliouonyesha Jana KUOMBA MSAMAHA KUTANGAZA "KUJIUZULU" kwani "HATAAMINIKA TENA"
Respect to Masoud .....
Zimafutwa na kuunganishwa nyingi tuu lakini wanazidiwaMods unganisheni hizi NYUZI sasa imekuwa kero kila mmoja ananzisha uzi content ni zile zile.
Usijiuzulu hata wazo hilo usiwe nalo. Kutoa maoni yako ni haki ya kikatibaNdugu zangu wa JF
Nitoe maoni yangu kama Mtanzania Mzalendo kufuatia kauli ya Ndugai kubeza kitendo cha Rais Samia kuendelea na Sera ya kukopa Fedha nje ya Nchi kugharamia miradi ya Maendeleo
Kauli ya Mheshimiwa Ndugai sio tu inabeza na kudharau mamlaka ya Rais bali inalenga kuhujumu jitihada za makusudi za Rais Samia kukamilisha miradi mikubwa ya maendeleo inayohitaji Fedha nyingi sana kuikamilisha
Mheshimiwa Ndugai akiwa Kiongozi wa Bunge ameshindwa kuonyesha uwajibikaji wa pamoja wa kidola na ameamua kwa makusudi kutumia nafasi yake vibaya kwa maslahi binafsi
Ieleweke Rais Samia anakopa fedha kwa maslahi ya Nchi yetu na amekuwa muwazi kwenye suala hili
Ieleweke kuwa Fedha za Tozo haziwezi kugharamia miradi yote mikubwa ya kimkakati na haiwezi kuwa mbadala wa kukopa Fedha
Mheshimiwa Ndugai angeliweza kuomba kuonana na Rais Samia na kumshauri aonavyo badala ya njia aliyoitumia ya kuropoka HADHARANI!
Kwa maoni yangu kauli ya Mheshimiwa Ndugai likusudia kukwamisha juhudi za Rais wetu kukamilisha miradi mbalimbali ya Maendeleo kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani ya CCM
Nashauri Mheshimiwa JOB NDUGAI ajiuzulu mara moja wadhifa wake wa Uspika na akishindwa kufanya hivyo mamlaka husika zimchukulie hatua za kumvua uanachama wa CCM kwani kwa sasa sio Mwenzetu tena
Tumpe ushirikiano Rais Samia
KaziIendelee
Wanajitahidi sana, naona wameshaunganisha huu uzi sasa. Ni kero kila ukiingia JF unakutana na habari zinazofanana.Zimafutwa na kuunganishwa nyingi tuu lakini wanazidiwa
Inategemea na mtu mwenyewe,Yaani mtu kutoa mawazo yake ndio ajiuzuru? una akili za ovyo sana wewe
Why ajiuzuru? Kwani yy amewekwa na Rais?
'Mtu mzima na akili yake...'' hili ni neno kubwa sana likhusisha akili , umri na kufikiri kwa Mh Spika
Ni kwamba Wananchi wamepewa dondoo za kutathmini uwezo wa kifikra wa Spika wao
Well, si lazima ajiuzulu kama watu wanavyoshauri hata hivyo ni wakati atathmini kama ana heshima tena mbele ya Bunge na jamii kwa ujumla. Jana pale Ikulu wenzake walitueleza mengi kuhusu yeye na kubwa zaidi ni uwezo wake wa kufikiri
Hapa lazima uelewe hoja ni niniTunatumia mazoea ndio shida, but kama akiamua anaendelea kukaa na bado kama kiongozi wa mhimili akawa anampinga Rais wake
Ni kawaida Sana inchi zingine,
Kama akijiuzulu means hakuna mtu anapaswa kuongea anything tofaut na mawazo ya rais
Hapa lazima uelewe hoja ni nini
Kumpinga Rais kama kiongozi wa mhimili mwingine si jambo geni au baya.
Alichozungumza si kibaya au kigeni
Tatizo ni hili, kusingizia alinukuliwa vibaya
Kuomba msamaha kwa aliyosema kwa maana hajui alisema nini au alikusudia nini
Kuzungumzia miswada iliyopita mikononi mwake kinafiki
Kuhojiwa uwezo wake ''kiakili'' na Viongozi wote wakuu wa nchi
Heshima yake haipo kwasasa mbele ya jamii. Ajiuzulu tu
Yes lakini hiyo haitaondoa ukweli kuwa popote atakapokaa, simama au kutembea watu watahoji swali moja, mkuu wa nchi alitilia shaka utimamu na umri wa Ndugai.Mpaka ndugai ameomba msamaha ujue kuna kikao kilifanyika, otherwise angechuna