Nashauri tufute vyama vya upinzani vilivyopo tuanze upya harakati za kudai mageuzi ya kweli

Nashauri tufute vyama vya upinzani vilivyopo tuanze upya harakati za kudai mageuzi ya kweli

Huwezi kuwaacha CCM ambao ndio chanzo cha upinzani kudidimia, halafu unataka viundwe vyama vipya vya upinzani viendelee kuwepo na CCM, navyo vitakuja kuwa havina maana iko siku utarudi hapa utake vifutwe tena.
Tatizo letu tumeharibiwa na ufuasi wa vyama hata mahali pasipowezekana kabisa ilimradi ni mrengo wa chama unacokishabikia unaona inawezekana.

Kwenye andiko langu nimesema ccm ni tatizo lakini limekuwa tatizo zaidi pale ambapo aina ya upinzani tulionao ni kama unafanya kazi kwa manufaa ya ccm, ilimradi dunia ione nchi yetu ina upinzani wakati uhalisia haipo hivyo.
 
Hivi kweli kama unafikiri vizuri inawezekanaje ukajiita mpinzani huku Kila siku uko bize kumuomba unae pambana naye akutangenezee mazingira mazuri?

Angalia mataifa jirani yanayotuzunguka aina ya upinzani walionao. Ili tufike huko tukubaliane hivi vyama tulivyo navyo Leo tunaita vya uipinzani vife ili yaanze makundi ya harakati yenye mrengo wa kupambana na madhila.

Nikuhakikishie hivi vyama vimefika upeo wa kufanya mambo na sivilaumu maana si kosa lao, ni tatizo la mfumo tulionao. Ili kupambana na huu mfumo Kwa ufanisi ondoa vyama anzisha vuguvugu najua hilo vuguvugu litaungwa mkono na wengi maadamu tu liguse maslahi ya wengi.

Kwa inavyotafsirika sasa hawa wapinzani wetu na kama wasaka tonge tu maana hawana maamuzi wala kishindo kikubwa kinachoweza kuwasumbua watawala.
 
Harakati za kudai mageuzi ya demokrasia katika nchi yetu yalianza miaka miaka mingi iliyopita.

Hatimae Kwa shinikizo la mataifa makubwa tukakubali kuruhusu mfumo wa vyama vingi ndani ya muundo wa chama kimoja.

Kwa maoni yangu ikiwa tunahitaji upinzani utusaidie kweli kweli lazima tuanze upya harakati za kudai mageuzi ya kidemokrasia nje ya vyama vya upinzani vilivyopo sasa.

Kwa maoni yangu vyama vya upinzani vilivyopo sasa vinatumika tu kama rubber-stamp ya kuhalalisha kuwa nchi yetu ina upinzani kwa manufaa ya ccm.

Hata tukisema tunataka katiba mpya bado huo mchakato utahodhiwa na ccm Kwa kuwa ndiyo inayohodhi system nyingi.

Ukisha futa upinzani utaibua vuguvugu la upinzani lisilo na sura ya kichama lakini lenye sura ya kiharakati ili liwe na uwezo wa kuabsorb ajenda zote zitokeazo njiani.

Upinzani uliopo sasa umeishiwa maarifa ya kupambana na ccm na kuzidiwa mbinu na ccm Kwa mbali sana.

Kivyovyote iwavyo ili kuibua kundi litakalo aminiwa na raia kwamba wanaopigania maslahi ya wananchi basi lazima hilo kundi litokane na harakati.

Nilipowasikia chadema juzi nikawashangaa eti wanaomba ridhaa ya kufanya siasa Toka Kwa serikali inayoongozwa na ccm. Hii ndio dalili ya wazi kwamba tunahitaji aina mpya ya kudai mageuzi.
Ya kufutwa ni CCM kwani haina tofauti na bokoharam tu
 
Mkuu ni muhimu sana katika taifa kuwa na upinzani na ushindani madhubuti ili kuwafanya walioshika madaraka waone kwamba hawako peke yao. Ni sawa na timu ya mpira kukiwa na wachezaji wawili wenye viwango vinavyokaribiana kwenye namba au nafasi moja inawafanya wajitume mpaka kiwango Chao Cha mwisho ilimradi wasikose namba jambo ambalo hugeuka kuwa faida Kwa kocha timu na hata mashabiki.

Kwa hiyo kama huamini katika upinzani naomba nikushawishi Leo kwamba upinzani madhubuti utalisaidia sana taifa letu kiuongozi.

Mkuu huo upinzani unaoutaka ukija ndio utaepuka vikwazo vya haya matumizi ya vyombo vya dola? Maana hadi sasa tatizo sio vyama vya upinzani, hata kama kuna mapungufu kadhaa kwenye upinzani. Kama chaguzi zinaendeshwa kisha matokeo yanatangazwa yasiyo sahihi kwa nguvu ya vyombo vya dola, hapo tatizo ni vyama vya upinzani vilivyopo? Au una agenda nyingine nyuma ya pazia?
 
.Unatakiwa ujue mageuzi au mabadiliko yoyote hayaletwi na vyama vya upinzani bali yanaletwa na wananchi wenyewe.vyama vinatumika kama bebeo la hiyo agenda.Kwahiyo tatizo lililopo hapa sio la vyama vya upinzani bali la wananchi wenyewe wako katikati ya usingizi wa pono.Ulipaswa ushauri nini kifanyike hili hayo mageuzi yaje.Ccm imeshakua chama dola ili kitoke madarakani au kiwajibike kwa wananchi kunahitajika akili kubwa sana na ni jambo linalohitaji muda kulingana na uelewa na mazingira ya nchi yalivyotengenezwa.Tupaze sauti watu waelimike na tupiganie mupata katiba bora itakayosaidia kurekebisha baadhi ya mambo ya msingi.Hadi sasa kupepigwa hatua kubwa sana cha msingi tuunge mkono harakati zakujikomboa kwasababu mapambazuko ni karibu.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Umeongea vizuri sana kama vyama vipo lakini having ubavu wa kufanya chochote vipo ili iweje?
 
Naona hapa unaungana na mimi kuwa mageuzi huanzia kwa raia na sii Kwa vyama ila vyama ni kama mbebeo sasa hapa tuna changamoto kwamba mbebeo ni mbovu na wananchi ambao ndio wadau wa mabadiliko wamekatishwa tamaa na mbebeo Kwa kuwa hawaziamini
 
Umeongea vizuri sana kama vyama vipo lakini having ubavu wa kufanya chochote vipo ili iweje?

Hicho unachotaka kiwepo kitapata wapi ubavu wa kufanya hayo utakayo? Fahamu kuwa kwa sasa hakuna CCM, bali kuna nguvu ya dola. Labda hicho chama chako kianzie msituni.
 
Tatizo letu tumeharibiwa na ufuasi wa vyama hata mahali pasipowezekana kabisa ilimradi ni mrengo wa chama unacokishabikia unaona inawezekana.

Kwenye andiko langu nimesema ccm ni tatizo lakini limekuwa tatizo zaidi pale ambapo aina ya upinzani tulionao ni kama unafanya kazi kwa manufaa ya ccm, ilimradi dunia ione nchi yetu ina upinzani wakati uhalisia haipo hivyo.
Naona wewe ndio hukielewi unachokitetea. Kama ukijua mazingira ya kisiasa yaliyopo hapa Tanzania sio sawa, CCM iko kama chama dola, na dola inajulikana ina silaha za moto, na sheria za nchi zinakataza vyama vya siasa kuwa na vikundi vya ulinzi, sioni hapo unavilaumu vyama vya upinzani kwa sababu ipi zaidi.

Kama hivyo vyama vyako unavyovitaka vitaruhusiwa kushindana na CCM vikiwa na polisi na silaha wao, hapo sawa, lakini kinyume na hapo, hakuna kitakachobadilika kwa sheria hizi zilizopo huku CCM ikiendelea kutawala.

Huo upinzani unaofanya kazi kwa maslahi ya CCM kwangu hauna maana, mimi nauona ule wa Mbowe kubambikiwa kesi, Lissu kupigwa risasi, na Lema kukimbia nchi, sio ule wa Zitto na serikali ya Umoja wa Kitaifa kule Zanzibar.
 
Back
Top Bottom