Nashukuru Mungu mwaka 2023 nimetimiza ndoto yangu ya kuishi Masaki japo ni chumba kimoja

Genta mi nakufahamu tumekua wote mtaa mmoja na akina Tony na mdogo wake aliyekufa kwa ajali maka kadhaa iliyopita
 
Ni kweli huyo mzee watu wa Umoja Road wote wanamfahamu alifanya kazi kubwa sana
 
Umenikumbusha mbali na mengi. Ila usingizi unasumbua. Mungu akijalia nitaandika kesho. 😍😍
 
Genta mi nakufahamu tumekua wote mtaa mmoja na akina Tony na mdogo wake aliyekufa kwa ajali maka kadhaa iliyopita
Hakuna Msiba ulioniuma kama wa jirani yangu, Rafiki yangu mkubwa na Mdogo wangu tokea Utotoni mwetu hapo Kitaani Chole Road kama wa Ngapasa.

Kaka yake Roy, Adinani na Dada yake wa Kipekee Happy niliosoma nao Oysterbay Primary School chini ya Mwalimu Mkuu wetu enzi hizo Marehemu Mama Ng'ambi hivi sasa wako wapi Mkuu?

Kama unavyonifahamu nami nakujua.
 
Ngapasa aliumiza wengi sana,ndio alikuwa ametoka kumaliza IFM miaka michache tu,alikuwa mtu poa sana
 
Bibi yangu alikuwa na shamba pale Mbezi Beach Tangi Bovu. Palepale lilipokuwa Tangi Bovu kwa upande wa pili.

Tabata tulikuwa tunaenda kitambo miaka ya 1980s nyumba za Bima. Enzi hizo wadogo tunaona mbaalinkweli kama tunakwenda nje ya mji.

Ubaya Ubaya stand up!
 
Nyumba za bima za kitambo sana zote alizinunua mama Rwakatare RIP,Tabata ulikuwa mbali kweli ila sasa hivi dah pamekuwaje karibu
 
Nyumba za bima za kitambo sana zote alizinunua mama Rwakatare RIP,Tabata ulikuwa mbali kweli ila sasa hivi dah pamekuwaje karibu
Dah, kumbe zile nyumba alizinunua yule Mama? Alikuwa anakuja sana home.

Sijafika huko kitambo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…