Nashukuru Mungu mwaka 2023 nimetimiza ndoto yangu ya kuishi Masaki japo ni chumba kimoja

Nilizaliwa nikajikuta niko mitaa ya Chole Oysterbay,
Mwaka 1988 kufumba na kufumbua roli aina ya Bedford limekuja nyumbani kutuhamisha kuelejea Tabata huwezi amini mizigo haikufika hata nusu ya roli lile,enzi hizo watumishi ukihamia nyumba ya serikali unakuta vitanda,nagodoro,sofa ,dinning table and chairs.Etc.
Kuja kugundua kumbe mzee anehamishwa kupelekwa Tabora kikazi,aliona asiende na familia kwa sababu fulani fulani hususani masomo na mama yake aliyekuwa ana clinic pale muhimbili.Wiki nzima tulikuwa tunalia tu huko kwenye makazi mapya,nyumba haikuwa na umeme tuliozoea,mazingira hatukuyaelewa sababu ya utoto

Wazee wa bata,Tabata imetoka mbali,mwaka huo 1988 hakukuwa na lami,mji ukiishia Tabata magengeni opposite na kanisa la Kristo Mfalme,maeneo ya Liwiti,Baracuda mpaka Segerea ilikuwa ni machimbo rasmi ya mchanga ,mchanga wote wa kujengea daslama yote ulitoka segerea,maeneo ya liwiti kulikuwa na kota za TAZARA,mbele kidogo kota za kiwanda cha sigara ,hapo baracuda kulia kota za chuo cha ufundi chang'ombe sasa VETA,.Kinyerezi na Kifuru ilikuwa msitu mkubwa sana na Simba walikuwepo

Ukiwa mgeni utachanganya na haya majina,maana Tabata kuna posta,chang'ombe na sigara,majina ambayo yanapatikaña maeneo nengine ya jiji.

Tabata enzi hizo ikiwa na baa kubwa mbili tu,Hai bar ya mzee Mushi na Camp bar ya mzee Mmari,wachaga shikamooni mlijua kuchungulia fursa kitambo.hakukuwa na bar ya maana zaidi ya gloceries.hapo Hai bar walikuwa wakionyesha sinema za bluce lee,mithun chakrabot,govinda ,etc,
Tabata nyumba zenye umeme zilikuwa za kuhesabu,maji ya bomba ilikuwa anasa ni visima kwenda mbele,kutoka mandela road mpaka liwiti ungetumia takriban lisaa lizima kwa gari,mbarabara ilijaa mashimo.

Dalili njema ilianza kwa kupata jengo la Aroma,timu ya pamba ikiwa na akina Fumo Felician,George Masatu,Hussein Masha,khalfan Ngassa ilikuwa ikifikia hapo na kufanya nazoezi kwenye uwanja wa Tabata shule au Tabata shooting Stars ,siku hizi kuna shule ya St Marrys.
Simba pia walikuwa wakifikia kwenye guest house ikijulikana kama sparkland maeneo ya ubayaubaya..tabata kimanga ilikuwa ni mapori tu,viwanja vya serikali vikiuzwa kwa sh 1200.lakini watu walikataa eti ni porini,ni mpaka Juma ikangaa na National Housing walipoanza kujenga maeneo ya mawenzi watu wakaanza kupaelewa.
Shule ya msingi kimanga walisomea chini ya mwembe npaka gazeti la mfanyakazi liliporipoti hali hiyo ndio mfadhili wa Simba Azim Dewji akajenga madarasa mawili,mpaka leo kwa wazawa ukitamka kimanga kwa dewji wanaelewa ni wapi.
Tabata siku hizi ina mastaa akina ally kiba,dully sykes,mr blue,tunda man,erasto nyoni,kapombe,domayo

Hali hii ya mazingira ilinisononesha sana japo nilikuwa mdogo nikasema ipo siku nitarufi masaki iwe isiwe,imenichukua miaka 35 kutimiza ndoto yangu

mwaka huu mwezi March nilipata servant Quarter room moja ba choo ndani kwa laki mbili,nitaishi humo mpaka nizeeke,au nifie humo maana uwezo wa kulipia nyumba nzima kwa dola 1000 kwa mwezi siuoni kwa siku za karibuni japo yote yanawezekana,Kumbuka nina makazi rasmi somewhere in town kwa ajili ya watoto na mama yao ambaye tulishatengana

Kumbuka enzi zile maeneo kama mbweni na Mbezi Beach hayakuchukuliwa kuwa maeneo ya kifahari so akili yangu haikuyazingatia mpaka leo

Kupanga ni kuchagua Usinipangie.
Masaki ilikuwa zamani.......
 
Ni sawa lakini haipendezi kuishi kisela hivyo hata kama ni kutimiza ndoto Kuna uzee unakaribia..
Uzee unakaribia ni kweli ila sina mpango wa kuoa hivi karibuni,na muda mwingi siko dar
 
Ilikuwa masaki kweli ila kwa mipango miji mibovu ya jiji letu,bado ni the best place iliyo karibu na city centre
Kwa miaka hii...city center haina mashiko...huduma zapatikana popote....serikali Dodomya
 
Hapo segerea karibu na car wash kuna single maza yangu moja toto la kikurya na kihaya mtt wa mzee mniko uyo single maza ni super delicious...Black,tall,cute.

Niamini mimi aiseeee.
 
Ngoja wamsake wahuni
 
Nilizaliwa nikajikuta niko mitaa ya Chole Oysterbay,

Mwaka 1988 kufumba na kufumbua roli aina ya Bedford limekuja nyumbani kutuhamisha kuelejea Tabata huwezi amini mizigo haikufika hata nusu ya roli lile,enzi hizo watumishi ukihamia nyumba ya serikali unakuta vitanda,nagodoro,sofa ,dinning table and chairs.Etc.

Kuja kugundua kumbe mzee anehamishwa kupelekwa Tabora kikazi,aliona asiende na familia kwa sababu fulani fulani hususani masomo na mama yake aliyekuwa ana clinic pale muhimbili. Wiki nzima tulikuwa tunalia tu huko kwenye makazi mapya,nyumba haikuwa na umeme tuliozoea,mazingira hatukuyaelewa sababu ya utoto

Wazee wa bata,Tabata imetoka mbali,mwaka huo 1988 hakukuwa na lami,mji ukiishia Tabata magengeni opposite na kanisa la Kristo Mfalme,maeneo ya Liwiti,Baracuda mpaka Segerea ilikuwa ni machimbo rasmi ya mchanga ,mchanga wote wa kujengea daslama yote ulitoka segerea,maeneo ya liwiti kulikuwa na kota za TAZARA,mbele kidogo kota za kiwanda cha sigara ,hapo baracuda kulia kota za chuo cha ufundi chang'ombe sasa VETA,.Kinyerezi na Kifuru ilikuwa msitu mkubwa sana na Simba walikuwepo

Ukiwa mgeni utachanganya na haya majina,maana Tabata kuna posta,chang'ombe na sigara,majina ambayo yanapatikaña maeneo nengine ya jiji.

Tabata enzi hizo ikiwa na baa kubwa mbili tu,Hai bar ya mzee Mushi na Camp bar ya mzee Mmari,wachaga shikamooni mlijua kuchungulia fursa kitambo. Hakukuwa na bar ya maana zaidi ya gloceries.hapo Hai bar walikuwa wakionyesha sinema za bluce lee,mithun chakrabot,govinda ,etc,

Tabata nyumba zenye umeme zilikuwa za kuhesabu,maji ya bomba ilikuwa anasa ni visima kwenda mbele,kutoka mandela road mpaka liwiti ungetumia takriban lisaa lizima kwa gari,mbarabara ilijaa mashimo.

Dalili njema ilianza kwa kupata jengo la Aroma,timu ya pamba ikiwa na akina Fumo Felician,George Masatu,Hussein Masha,khalfan Ngassa ilikuwa ikifikia hapo na kufanya nazoezi kwenye uwanja wa Tabata shule au Tabata shooting Stars ,siku hizi kuna shule ya St Marrys.

Simba pia walikuwa wakifikia kwenye guest house ikijulikana kama sparkland maeneo ya ubayaubaya..tabata kimanga ilikuwa ni mapori tu,viwanja vya serikali vikiuzwa kwa sh 1200.lakini watu walikataa eti ni porini,ni mpaka Juma ikangaa na National Housing walipoanza kujenga maeneo ya mawenzi watu wakaanza kupaelewa.

Shule ya msingi kimanga walisomea chini ya mwembe npaka gazeti la mfanyakazi liliporipoti hali hiyo ndio mfadhili wa Simba Azim Dewji akajenga madarasa mawili,mpaka leo kwa wazawa ukitamka kimanga kwa dewji wanaelewa ni wapi.
Tabata siku hizi ina mastaa akina ally kiba,dully sykes,mr blue,tunda man,erasto nyoni,kapombe,domayo

Hali hii ya mazingira ilinisononesha sana japo nilikuwa mdogo nikasema ipo siku nitarufi masaki iwe isiwe,imenichukua miaka 35 kutimiza ndoto yangu

mwaka huu mwezi March nilipata servant Quarter room moja ba choo ndani kwa laki mbili,nitaishi humo mpaka nizeeke,au nifie humo maana uwezo wa kulipia nyumba nzima kwa dola 1000 kwa mwezi siuoni kwa siku za karibuni japo yote yanawezekana,Kumbuka nina makazi rasmi somewhere in town kwa ajili ya watoto na mama yao ambaye tulishatengana

Kumbuka enzi zile maeneo kama mbweni na Mbezi Beach hayakuchukuliwa kuwa maeneo ya kifahari so akili yangu haikuyazingatia mpaka leo

Kupanga ni kuchagua Usinipangie.
Hongera
 
Dah, kumbe zile nyumba alizinunua yule Mama? Alikuwa anakuja sana home.

Sijafika huko kitambo sana.
Alizinunua kitambo wanaishi staff wa St Marrys Tabata,kiukweli Tabata kumenoga
 
Back
Top Bottom