Ukweli ni kwamba mtakiuwa chama cha Mwalimu nyinyi wenyewe kwa kukosa ujasiri tu wa kukataa uhuni huu unaofanywa ndani ya chama kwa kutumia jina lake.
CCM inayo misingi imara sana ambayo leo hii akitokea kiongozi mwenye dhamira ya kukirekebisha chama hicho, waTanzania watarudi temna na kukitazama chama hicho kwa umakini mkubwa.
CHADEMA ni chama kichanga sana; hasa baada ya kuvurugwa na kiongozi wao wa miaka mingi. Chama hiki bado kinahitaji sana kujitanua hadi huko chini ilikoenea vizuuri sana CCM. Hii ni kazi ngumu na kubwa sana isiyoweza kufanyika katika muda mfupi huu wa dharura.
Lakini yanayofanyika sasa hivi ndani ya CCM, italazimu wananchi wakibebeshe majukumu makubwa sana chama hiki kichanga; kama kilivyobebeshwa TANU, enzi zile za kupata uhuru.
Samia na GENGE lake; pakiwa na TUME HURU, na uchaguzi ufanyike kwa HAKI, hana njia ya kubaki madarakani.
Sasa uchaguzi ni wenu. Mbakisheni Samia akiongozwa na Genge; au jirekebisheni wenyewe huko ndani kwa ndani kwa dharura, ili mbaki na uwezekano wa kukiokoa chama chenu.