Nasikitika kusema kwamba, Katiba Mpya tunayoitafuta kwa nguvu nyingi haiwezi kutusaidia

Nasikitika kusema kwamba, Katiba Mpya tunayoitafuta kwa nguvu nyingi haiwezi kutusaidia

Shida sio kuandikwa katiba ingine,, shida ni implementation za hyo mpya,, kama ya zaman inawashindwa mtaweza mpya[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] #allpoliticiansarefilthyliers

..mimi nadhani tuandike mpya, tena bora.

..baada ya hapo ndio tutajua kwamba tuna uwezo wa kuilinda au hapana.
 
..mimi nadhani tuandike mpya, tena bora.

..baada ya hapo ndio tutajua kwamba tuna uwezo wa kuilinda au hapana.
Sawa tuandike,, but tambua kuwa duniani tanzania ndio nchi ya kwanza inayopenda #kitonga cheap things are our style,,na hakuna kitu kilicho expensive as having katiba inayosimamia virtue za kuwa responsible na kuwa held accountable kwa kazi zinazofanyika na hao #liers
A good example ni curriculum yetu,, in terms of a a written document na aims zake ni best in east Africa,, when it comes to implementation,, [emoji28][emoji28][emoji28] God only knows,,,
A piece of advice ,, don't trust em
 
Shida sio kuandikwa katiba ingine,, shida ni implementation za hyo mpya,, kama ya zaman inawashindwa mtaweza mpya[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] #allpoliticiansarefilthyliers
Ndiyo maswali nayojiuliza mkuu, Ningeshauri hawa wenzetu hasa chadema, Maskini wee, wangejitahidi sana kushawishi na kuwaelimisha wananchi ili angalu kuonekane ile Sura ya Kitaifa kwamba, tunataka katiba kweli

Sasa unakuta ni wao tu wanaimba wimbo wa katiba ili hali wengine wengi wako tu hawana habari hata kidogo

Ni bora hizi fedha za kukodisha kumbi kwa ajili ya makongamano haya, wasekeze kwenye eneo lingine
 
Ndiyo na ni ukweli kabisa, Katiba tunayojaribu kuitafuta kwa jasho jingi na Energy nyingi, nasikitika kusema, haitatusaidia popote kama nchi.

Kama kuna mtu anapingana na mimi, Embu atusaidie kujibu maswali haya

Ni kweli tumekuwa na katiba isiyokidhi matakwa yetu hususani katika midhania ya kisiasa, kwa maana, katiba iliyopo, ilitungwa chini ya Chama kimoja, hivyo kuvifanya vyama vingine kukosa uhalali wa kulindwa na katiba hii tuliyonayo

Kingine, Katiba hii iliyopo, inamfanya Rais wetu kuwa mfalme, ni kama yeye ni mtu wa kwanza na wa mwisho, kwa lugha ys kiyunani, ni Alfa na Omega, n.k

Sasa basi, Ukisikiliza kwa umakini, wengi wa wanaharakati wetu kwenye majukwaa ya kisiasa na majumkwaa mbalimbali mbali, Utasikia wakisema, Tunataka katiba itakayotuwezesha kuwaajibisha wote wanaovunja katiba

Ni jambo jema, maana mtu yeyote anayediriki kuvunja makubaliano yetu na katiba yetu , ni sawa na matusi kwa watu woote kama taifa

Tumeshuhudia katiba yetu ikivunjwa waziwazi na baadhi ya viongozi wetu,

Bahati mbaya ni kwamba, kuna waliovunja katiba hata kwa wale ambao, katiba hailindi ouvu wao kama ilivyo kwa Maraisi wa nchi, lakini wanapovunja, Hasira zetu tunazielekeza kwa kiongozi mkuu, tunamsagia meno, Wakati huohuo, Katiba yetu mbovu tuliyonayo, ni kumlinda Raisi wa nchi na maovu yote kipindi awapo madarakani, na kwamba Hawezi kushitakiwa kwa kosa lolote awapo madarakani

Na bila shaka, shida yetu inaanzia hapo


Okay, Achilia mbali makosa ya Rais kwa mjibu wa katiba mbovu tuliyonayo kwamba, hatoshitakiwa kwa makosa yoyote aliyotenda akiwa madarakani, Hili tunaweza kusema, lipo juu ya mamlaka ya kawaida ya mwananchi kumwajibisha Raisi wao kwa kuwa katiba inamlinda

Upande wa pili kwa kosa hilohilo la kikatiba, Tumeshuhudia Bunge lisilo halali, Ni bunge ambalo wabunge wenginewe waliomo humo bungeni si wabunge halali kwa mjibu wa katiba za vyama vyao pia kwa mjibu wa katiba ya nchi, kwamba hawana uhalali wa kuwa wabunge kwa kuwa, hawatambuliki na vyama vyao na katiba haitambui mtu wa aina hiyo kuwa sehemu ya bunge

Sasa basi

Nionyesheni ni wapi ambapo huyo mkuu wa mhimili huu wa Bunge alipohalalishiwa na katiba hii mbovu tuliyonayo kwamba naye hawezi kuwajibishwa,

Je sasa, ni nani wa kumwajibisha?
Ni kwa nini tunataka katiba mpya, Je, ni nani atakuwa mbadala wetu wa kusimama na kuwawawjibisha wote wavunja katiba?

Je, katiba hii mbovu ilipokuwa ikivunjwa, ni nani anafahamika ambaye yeye anapaswa kudili na wavunja katiba yetu? Je, alifanya kazi yake?


Na kama alishindwa kuwashughurikia hao waharifu wa kikatiba, Ni kwa vipi anadhani itakuwa rahisi kuwashughurikia kukiwepo katiba mpya?

Ni nani asiyejua kwamba, Watanzania, Watanzania kwao ni wazuri wa kuhamaki mitandaoni pekee ila nje ya hapo ni watu wanafiki na wapole kama maji ya mtungi? na ndiyo maana hata Asiyelindwa na katiba aweza kuvunja katiba na ikawa salama??

Mkinionyesha atakayekuwa zamu ya kuwashughurikia wahalifu wa kikatiba badala yetu, ndipo nitakubali kwamba, Tunataka kweli katiba na tumemaanisha

Katiba haijilimdi, haijipeleki mahakamani, haiandamani na wala haimtishi mvunja katiba, Nionyesheni mlinzi wa katiba

Tanzania hoye?
Hata kama Katiba mpya inahitajika, haiwezi kulazimishwa na handfuls walioko mitandaoni na ughaibuni. Katiba mpya italetwa na Watanzania.
 
Unajua sana mkuu haya mambo!

Katiba siyo ya kikundi fulani, ni ya kitaifa
Umeonaee! Watu wanafikiri Katiba ni kitu kidogo! Wamarekani wana kamsemo kazuri,"...We the People... !" Sijui kama vijana wa mtandaoni wanaelewa maana yake!
 
Wakati Kenya walipokuwa wanasubiri katiba yao mpya ilikuwa kila mtu ana mategemeo yamabadiliko ya kila kitu.Hata mtu akigombana na mwenzie anamwambia ngoja katiba mpya ije utaona ,mtu akienda dukani akikuta bidhaa bei ipo juu kidogo anajiapia kabisa kuwa hawa wanaopandisha bei vitu watakoma katiba mya ilkipatikana.Siku ilipozinduliwa Katiba iliyoitwa mpya walisherehekea na wa walipolala na kuamka asubuhi wakajikuta wako vilevile kama walivyokuwa juzi.[emoji3][emoji3][emoji3]
Unaweza ukawa na kitu kipya lakini sio bora.sasa ni mjinga peke yake atakayefikiri kwamba sisi kama watanzania hatuna akili zakutengeneza kitu kizuri na bora kwa ajili ya maendeleo yetu ya sasa na vizazi vijavyo
 
Kama hadi sasa unawaza katiba ni kwa ajili ya wanasiasa itakua una tatizo la kufikiri.
Nikikuuliza wewe hio katiba iliyopo inakusaidia nini so far? Unaweza kunijibu kwa ufasaha labda! Inakunufaisha in what ways mpaka utake nyingine as if you have stakes on it!?
 
Wakati Kenya walipokuwa wanasubiri katiba yao mpya ilikuwa kila mtu ana mategemeo yamabadiliko ya kila kitu.Hata mtu akigombana na mwenzie anamwambia ngoja katiba mpya ije utaona ,mtu akienda dukani akikuta bidhaa bei ipo juu kidogo anajiapia kabisa kuwa hawa wanaopandisha bei vitu watakoma katiba mya ilkipatikana.Siku ilipozinduliwa Katiba iliyoitwa mpya walisherehekea na wa walipolala na kuamka asubuhi wakajikuta wako vilevile kama walivyokuwa juzi.😀😀😀
Lakini we Jamaa, Nimesomaaa nikarudia tena, na sasa nimekuelewa saaana, Ingawa umeandika kimasikhala sikhala, lakini ndani yake mna ujumbe mkubwa sana

Jambo hili la katiba tunawapa wananchi matumaini makubwa mno, tunasahau kwamba, Katiba haizuii uhalisia wa mambo, Katiba haitafuti wala kuandaa viongozi bora

Katiba, haina ufahamu wowote wa kujua mgombea atayegombea atakuwa ni muungwana ama laah!!
 
Umeandika mada yako kishabiki sana na inaonyesha unafanya tu makusudi kujifanya hujui katiba bora ikoje .ila nataka nikupe jambo ulitafakari.Hivi hii nidhamu ya hali ya juu unayoiona kwenye jeshi la wananchi wa Tanzania(Jwtz) unadhani ni nani anaisimamia?.Majibu utakayoyapata yatafakari.
 
Umeandika mada yako kishabiki sana na inaonyesha unafanya tu makusudi kujifanya hujui katiba bora ikoje .ila nataka nikupe jambo ulitafakari.Hivi hii nidhamu ya hali ya juu unayoiona kwenye jeshi la wananchi wa Tanzania(Jwtz) unadhani ni nani anaisimamia?.Majibu utakayoyapata yatafakari.
wewe unalinganisha kitu kinaitwa Amri na katiba, katiba siyo amri,

Katiba siyo amri kwa sababu inaweza kubadirishwa, lakini Amri haibadiriki, ukiambiwa usizini utauwawa, hauhitajiki kupelekwa mahakamani, ni papo kifo kinakuhusu, halafu ulinganishe na katiba ambapo mtu baada ya kuivunja anatafuta na wanasheria wa kumtetea mvunjaji?

Unajua maana ya Amri lakini?
 
Watanzania hawajui kuandamana, hawajui kudai haki yao, wao wanaamini tu kwamba, Mungu ndiyo kila kitu

Hivi kwa nini kweli tunahangaishana kudai katiba?
Katiba Mpya ni muhimu... Sema watanzania wengi ukiwapa uchaguzi kati ya Katiba na peremende basi watachukua peremende!
 
Nikikuuliza wewe hio katiba iliyopo inakusaidia nini so far? Unaweza kunijibu kwa ufasaha labda! Inakunufaisha in what ways mpaka utake nyingine as if you have stakes on it!?
Wewe ndio hujui umuhimu wa katiba na jinsi inavyofanya kazi.jielimishe kwanza ndo urudi kwenye mjadala.
 
Mnakuwa na viongozi na Rais ovyo kabisa hapa chini ya jua halafu mnakuwa na Katiba bora zaidi duniani. Tutatoboa?

Mnakuwa na Rais na wasaidizi wake bora zaidi lakini katiba ndo hii hii. Tutatoboa?

China tuijuayo haipigi kasi ya maendeleo sababu ya katiba bora zaidi duniani. Hapana. Ni timu tu ya watu wenye uwezo na nia ya kuipeleka China mbele ndio msingi wa kasi ya maendeleo ya China

Hata sisi tukipata vichwa vizuri vya viongozi vikakaa pamoja na kufanya kazi lazima tutoboe. Katiba ni miongozo Fulani ambayo inaweza isifuatwe au ikakanyagwa makusudi na mkanyagaji asifanywe chochote

MNA katiba Bomba lakini viongozi wenu kutwa kucha kuwapigia magoti wazungu, wachina, waarabu, wahindi na nk mtatoboa kweli?
 
Hii kwangu ndio hoja ya msingi! Unashabikia katiba ili Mbowe anufaike na kumuingiza Lissu madarakani 😂😂😂 ni akili au matope hayo!
Wanaoshabikia katiba mpya ni wabinafsi na wapigaji kama majambazi wengine, mimi nawaza ajira bado wapumbavu wanataka tuandamane juu ya katiba mpya.
 
Wewe ndio hujui umuhimu wa katiba na jinsi inavyofanya kazi.jielimishe kwanza ndo urudi kwenye mjadala.
Ningeona umuhimu wa katiba na mimi ningepigania, nyie mnataka katiba mpya ili mpate njia nyepesi ya kupata uongozi wa nchi, pambaneni na hali yenu na mm napambana na njaa yangu.
 
wewe unalinganisha kitu kinaitwa Amri na katiba, katiba siyo amri,

Katiba siyo amri kwa sababu inaweza kubadirishwa, lakini Amri haibadiriki, ukiambiwa usizini utauwawa, hauhitajiki kupelekwa mahakamani, ni papo kifo kinakuhusu, halafu ulinganishe na katiba ambapo mtu baada ya kuivunja anatafuta na wanasheria wa kumtetea mvunjaji?

Unajua maana ya Amri lakini?
Hiyo amri iliwekwa na nani na inasimamiwa na nani?.Maana wewe umeuliza ni nani atakayeisimamia hiyo katiba na mimi nimekupa mfano rahisi sana kuuelewa.kwamba kama jeshini inawezekana kujiwekea utaratibu na wakazisimamia wenyewe ata sisi kama wananchi tunaweza kuweka utaratibu kupitia andiko linaloitwa katiba na tukaisimamia wenyewe.Ayo unayoyaona yamefanyika uko nyuma nikwasababu kama wananchi hatukuamua tuwe na kitu bora chakutusimamia ndo maana viongozi wachache wakaamua kuitumia hiyo nafasi kwa maslahi yao binafsi ila haimaanishi kwamba hatuwezi kua na katiba nzuri na ikajisimamia yenyewe.ata uko jeshini sheria zipo ni kazi ya askari kuifwata basi kinyume na hapo inakugharimu.
 
Ningeona umuhimu wa katiba na mimi ningepigania, nyie mnataka katiba mpya ili mpate njia nyepesi ya kupata uongozi wa nchi, pambaneni na hali yenu na mm napambana na njaa yangu.
Endelea kua na njaa kwasababu ujielewi.
 
Back
Top Bottom