Pre GE2025 Nasikitika kusema mfumo wa CHADEMA bado hauna uwezo wa kupewa uongozi wa nchi, labda waufanyie marekebisho au tuwape muda zaidi miaka 10 au 15 ijayo

Pre GE2025 Nasikitika kusema mfumo wa CHADEMA bado hauna uwezo wa kupewa uongozi wa nchi, labda waufanyie marekebisho au tuwape muda zaidi miaka 10 au 15 ijayo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Pamoja na udhaifu huo lakini bado vyama vya upinzani vimeonyesha udhaifu mkubwa zaidi kwenye mifumo yao ya ndani

Angalia kuanzia mfano wa vyama vikuu tangu 1995 ukianza na Nssr, Cuf, na kule Chadema inakolekea kwa Sasa Hali ZAO kwa sasa

Pia piga picha ya Mfumo wa UKAWA wa 2015 Kama wangeongoza serikali Leo Mfumo wa uongozi wa nchi yetu ingekuwa katika Hali gani ????

..ukawa wangeongoza serikali mwaka 2015 kwa maana yake ni kwamba dola ingeanza kufanya kazi kwa niaba ya ukawa kuhujumu Ccm.
 
Naendelea kusikitika kusema

Kwa poor organization ya Cdm kwenye zoezi hili la serikali za mitaa bado Sana kupewa nchi
Gharama za kurusha chopa na bajeti zingine zisizo na mashiko zingeelekezwa kwenye zoezi hili
kuhakikisha kunakuwa na watu wao wa kufuatilia Kila kituo
Ni ngumu kushinda uchaguzi mkuu wakati umeshindwa uchaguzi wa serikali za mitaa wapiga kura ni wale wale
 
Nachokiona pengine viongozi wa juu wa Cdm wanawaza nafasi zao kugombea ubunge na ngazi za juu za chama ili wapate zao Posho
 
CHADEMA imewahi kuongoza Manispaa na majiji kadhaa baada ya kushinda uchaguzi.

Sasa ikiwa waliweza kuongoza majiji Dar ikiwemo,

Washindwe vp kuongoza Nchi?
 
CHADEMA imewahi kuongoza Manispaa na majiji kadhaa baada ya kushinda uchaguzi.

Sasa ikiwa waliweza kuongoza majiji Dar ikiwemo,

Washindwe vp kuongoza Nchi?
Hii nguvu mnayoitumia kuitetea ndio mnawalemaza
 
Nachokiona pengine viongozi wa juu wa Cdm wanawaza nafasi zao kugombea ubunge na ngazi za juu za chama ili wapate zao Posho
Hivi vyama vya upinzani vinashida sana kwenye kuuza ilani yao kupata tu ilani zao ni mtihani
 
Chama Cha siasa kinachoamini kwa MTU badala ya mifumo yake ni aibu kubwa sana
 
Habari wakuu

Nikiri Mimi ni muumini wa demokrasia ya vyama vingi na siasa za hoja za ushindani kwani naamini ushindani wowote huletea wananchi maendeleo

Ni moja ya watu tunatamani kuona tunakuwa na vyama vya siasa imara vinavyoweza kubadilishana madaraka Kila wakati pale kilichopo kinaposhindwa kufikia matarajio ya wananchi

Pia nikiri wananchi wanatamani Sana mabadiliko kwenye maeneo mengi hata ikibidi chama kilichopo kiwekwe pembeni kwanza na waone

Lakini Naomba niandike kwa masikitiko makubwa kwamba Mfumo wa Chama kikuu Cha upinzani Chadema Hauna uwezo wa kubeba uongozi wa nchi na taifa kwa ujumla

Yako madhaifu mengi kwenye mfumo wa Chadema, Kwa Leo aomba nielezee udhaifu wa chadema kwenye

Demokrasia ya NDANI
Chadema inaonyesha udhaifu mkubwa haswa kwenye nafasi ya juu ya chama
MFumo wa Chadema unaruhusu nafasi ya juu ya uongozi, MTU mmoja kuweza kugombea mara nyingi atakavyo hata maisha

Hii inaonyesha hata wakipewa nchi wanaweza wakabadili Mfumo wa nchi kuwa hivyo na Pengine kuwa madikteta haswa,
maana kile wanachofanya Sasa ndo picha ya kile watachofanya wakipewa serikali

Pia hapa tuona tatizo kubwa lingine la Chadema kutegemea MTU badala ya Mfumo na Hili ni hatari Sana Kama tulivyoona kwa awamu Fulani waliacha kuimarisha Mifumo wakategemea Mtu ,
Nafikiri tuliona hatari yake pale yule mtu anapoondoka pasipo kutarajiwa
lazima Chadema kabla ya kupewa Serikali washughulikie hili.

Mbaya zaidi hili tatizo liko Hadi kwenye viongozi waandamizi wa juu kabisa wa Cdm kuamini MTU mmoja
Kwamba MTU Fulani akishachukua fomu ya nafasi Fulani Basi mwingine anakiri kutokuchukua hiyo fomu
Alafu mnataka mpewe nchi Muongoze kidemokrasia kweli

Pili Mfumo wa Chadema umeonyesha udhaifu mkubwa wa kubeba watu smart au maarufu wanajiunga na chama chao
Hiii inaweza kuchangiwa pia na udhaifu wa demokrasia ya Ndani

Tatu ni Mfumo wa Chadema kushindwa kubeba au kuhandle watu wenye mawazo tofauti na wale wanaokihama chama hicho

Neno usaliti limetumika kuwa kashifu na kuwatuhumu wale wanatofautiana na baadhi ya viongozi wa chama hicho au msimamo bila kujali hoja zao

Kama kuhama chama kwa kutofoutiana hoja au msimamo ni usaliti kwa chadema
Inakuwaje wanawapokea waliohama chama lingine kwa hoja zile zile na wengine wanakuja kwa kutaka kugombea tu nafasi Tena za Cdm

Je Cdm ikipewa serikali Leo itawachukuliaje wale wanaotofautiana na serikali yao ?
Kama watawachukulia Kama wasaliti Kama wanavyofanya kwa sasa
je wapinzani wao watakuwa salama ?

Hayo ni machache kwa Leo kwenye mfumo wa Chadema

Naamini bado Wana nafasi ya kufanya madabiliko ya mfumo wao kuweza kubeba dhamana ya juu zaidi katika nchi yetu na sio tu kuwa chama kikuu Cha upinzani

Wao ndo wataamua ni muda Gani kwa haraka au miaka kumi na 15 nayoiona mimi baada ya kuingiza uongozi wenye fikra mpya au waliopo wakubali madhaifu wabadilishe

Hakuna Haja ya kubomoa nyumba ya nyasi Kama huna uhakika wa kujenga au kupata nyumba Bora zaidi ya tofali na mabati au zaidi ya hapo
Mfumo wa CCM kutawala unawezekana Tanzania pekee ambako tupo usingizini.
 
Back
Top Bottom