Nasikitishwa na uhusiano wetu na Kenya, unaumiza wakulima na wafanyabiashara

Mleta mada hujielewi bunge la kenya limegoma kusaini mkataba kati ya uungereza na Kenya wa kuuza bidhaa za kilimo uingerez unaojulikana kama EPA sababu ni wa kinyonyaji unaumiza wakulima wa kenya.Bunge la uingereza lilisaini lakini kulikwa na kipengele cha kusema bunge la kenya halitakuwa na mamlaka ya kubadilisha huo mkataba au kuridhia

Tanzania huo mkataba wa EPA bunge letu liligoma na nyie michadema kwa ujinga wenu mkatukana sana humu sasa Bunge la kenya limegoma kuridhia


Ni sahihi chadema kuwa mlipigwa chini sio wazalendo kabisa.Bunge la kenya wabunge wa chama tawala na upinzani wamesimama kama kitu kimoja kukataa mkataba Wa EPA wa kibiashara kati ya Kenya na Uingereza wakati sisi mivyama koko kama Chadema haikusimama na wabunge wa CCM kupinga!!!
 
Sasa wewe mbona unakuwa mjinga sana?

Kwani huli suala kosa ni la viongozi wa wapi?

Umesikia selikali ya tz au Uganda ikizuia mtu kupeleka mahindi kenya?
 
Kosa la Magufuli kwenye hili ni nini?

Kwamba uhusiano na Kenya siyo mzuri?
Crimea!!! Hata hilo linakupa shaka? Hamkuchoma kuku wao? Mbona before Magufuli haya mambo ya ajabu ajabu hatukuyaona?
 
Crimea!!! Hata hilo linakupa shaka? Hamkuchoma kuku wao? Mbona before Magufuli haya mambo ya ajabu ajabu hatukuyaona?
Wewe, kabla ya Magu wakenya walikuwa wanawatia vidole mnakaa kimya, Magu kasema hapana ndio maana unaona wanavyorusha rusha miguu.
 
Ninachokiona mm Kuna gepu sehemu wazalishaji malighafi, kisha wasomi, kisha wafanyabiashara, kisha serikali inafunga mwisho Sasa kwenye nchi za Africa wasomi ni Kama gepu lakuto kukamilishaa dhumuni. Watu mnajifanya Kama kuwaonea huruma wakulima Kama kigezo cha kuilaumu serikali je serikali inamakosa ? Je wewe kama msomi wa humu jf unamsaidiaje huyu mkulima ukiachana hii kazi ya kutoa report ambayo nikazi ya mfanyabiashara ndo inabidi azitoe kwa serikali.
 
Tz ni hatari sana, waweza kuta wew ni graduate
 
nyie mnaoshabikia kila UJINGA wa viongozi wanapoboronga mnatia hasira sana!.

Anyway, ukishaolewa ukaacha utegemezi...akili itakukaa sawa!.
Utegemezi hawezi acha mana atakuwa anamtegemea mume wake
 


Lakini mbegu za kienyeji hutoa mazao hafifu balaa
 
We unaeandika utumbo huu ni mkulima au umejiskia tuu uandike!!?
Unajua shida tunayoipata sisi mipaka ikifungwa mbeha wewe!!?

Alafu nmekumind kishenzi yaan.

Kwa sababu ya watu kama hao pengine ndio maana nchi yetu ni masikini miaka nenda rudi

Usishangae hapo ni mtumishi wa serikali hana uchungu kabisa na ujasiriamali
 
Labda nikukumbushe tu mwandishi wa hii habari kwamba,''Kenya haijawahi kuwa rafiki wa kweli wa Tanzania,toka enzi na enzi''.Wakati Tanzania ikisadiana na nchi za kusini mwa Africa ,kwenye vita vya ukombozi,Kenya ilikuwa ikifanya biashara na Makaburu wa Afrika Kusini.Makaburu walikuwa ni adui yetu namba moja huko kusini mwa Afrika.Kuna makaburi mengi sana ya ndugu zetu huko Msumbiji na Angola.Ukiondoa ujirani wa mipaka,Tanzania na Kenya ,ni paka na panya.Labda Tanzania na yenyewe ilipe kisasi kwa Kenya kuacha kununua mahindi,sisi nasi tuache kununua bidhaa za wakenya.Sasa hivi ulimwengu ni kama kijiji tunaweza agiza bidhaa nchi za Asia,na tukaachana na hizi za majirani zetu.Kama Mbwai iwe mbwai!
 

Mtu anaefikiria kujikwamua kwenye umasikini hawezi kufikiria kutanguliza chuki au ushabiki shabiki kazini

Kilimo ni kazi
 


Na biashara haina uhusiano na uadui

Japan na China ni maadui tangu na tangu ila kajifunze wanavyouziana vitu vya thamani ya mamia ya matrilioni
 
Uhusiano na Kenya ni mbaya enzi na enzi walishachukua mpaka ndege zetu wakati wa EAC ya mwanzo labda kama hujui historia yetu na Kenya. Saa hizi Kenya wanaumia sana baada ya kuwabana wizi wa madini yetu ya Tanzanite na Dhahabu pia kuwanyima ajira hapa nchini. Tutawanyoosha tu pamoja na nyinyi vibaraka wao mliokuwa mnafaidika na wizi huo hatutarudi nyuma.
 
Wataalam wetu wa kilimo/mifugo vjijijini hawana msaada kwa wakulima/wafugaji. Hawana mpango kazi,hawatusaidii wakulima/wafugaji kwa lolote. Afadhali hivyo vyeo vifutwe,, wengi wamefungua viduka vya pembejeo, lakini ni watumishi wa serikali,wanalipwa mishahara
 
Na biashara haina uhusiano na uadui

Japan na China ni maadui tangu na tangu ila kajifunze wanavyouziana vitu vya thamani ya mamia ya matrilioni
Kama biashara haina uadui mbona Nyerere alipiga marufuku bidhaa za Kenya kuingia Tanzania.Kama kuingia ziliingia kwa magendo?
 
Mtu anaefikiria kujikwamua kwenye umasikini hawezi kufikiria kutanguliza chuki au ushabiki shabiki kazini

Kilimo ni kazi
Kwa hiyo wewe unataka wakenya wafanye wanachotaka wao siyo?? Subiri tunapiga stop bidhaa zao zote kuja TZ tuone nani ataumia zaidi.
 
Wewe siyo mkulima kwenda zao huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…