Nasumbuka sana wakuu mwenye kujua Tiba ya vidonda vya tumbo anijuze

Nasumbuka sana wakuu mwenye kujua Tiba ya vidonda vya tumbo anijuze

Nitangulize salam kwanza kwa ndugu wote wana jamii forum, kama kichwa cha Habari hapo juu kinavoeleza, ninasumbuliwa na vidonda vya tumbo huu mwaka wa 6 naomba kwa yoyote anayefaham dawa au ameshatumia dawa amepona anifahamishe na mimi niondokane na hiii karaha, , nipo mwanza, natanguliza shukran kwa yeyote atakayenijuza

Pole kwa kuumwa.

Mchango wangu kwenye hili ni:

1: Kutaka kujua uligundua vipi kuwa una shida ya vidonda vya tumbo. Hii ni kwa vipimo vilivyofanyika?
Ni vipimo gani ulifanya, hata kwa maelezo ya jumla tu kilivyofanyika?

2: Tiba na taratibu mbalimbali ulizopitia kwa wataalamu wa afya ili kutatua tatizo lako na ulifanyia kazi kwa kiasi gani?

Wakati mwingine magonjwa yamekuwa na mfanano katika kujitokeza kwake, mfano: unaweza kuwa na vijiwe kwenye mfuko wa nyongo na dalili zikawa kama za vidonda vya tumbo au ukawa na tatizo la Reflux ambalo tiba na suluhisho hywa tofauti kidogo.

3: Ulielekezwa nini cha kufanya kwenye mwenendo wa jumla wa kimaisha kuhusiana na lishe ili kutatua tatizo lako na umetekeleza/ ulifanyia kazi kwa kiasi gani?
 
Mtoa mada utapoteza pesa zako bureee kwanza kapime wingi wa gesi lakini anza na dozi ya bamia nakuhakikishia ndani ya miezi 6 utakua umepona kabisa fungu la bamia ni sh 500 tu
 
Chukua mapeke ya maparachichi,
licharange, anika kwenye jua lisilo kali, baada ya siku mbili limekauka, twanga au blend, chekecha, unga wake

chukua kijiko kidogo kimoja changanya na asali, lamba kutwa mara tatu, in seven days utakuwa sawa.

Hukuelewa ni check for more clarifications.

Upone haraka.
Samahani mkuu mapeke ya parachichi ndio nini
 
Huu ugonjwa unatutesa Jamani.

Mimi nitaanza Kugawa Dawa Baada ya kupona vizuri.
 
hUu ugonjwa umekuwa changamoto sana sana, ukiangalia kuanzia kwenye vyakula vya kutumia mpaka tiba yaani akili inawaza mpaka inachoka kabisa
 
Mtoa mada utapoteza pesa zako bureee kwanza kapime wingi wa gesi lakini anza na dozi ya bamia nakuhakikishia ndani ya miezi 6 utakua umepona kabisa fungu la bamia ni sh 500 tu
Asante sana , matumizi yake yakoje ?
 
NI TEXT INBOX NAMBA YAKO KISHA NITAKUTAFUTA TUONGEE NITAKUSAIDIA KUWEZA KULIFAHAMU TATIZO LAKO VIZURI..MIMI SIUZI DAWA WALA SITAKUTOZA HELA YOYOTE NITAKUHOJI NIJUE NAMNA UNAWEZA KUJITIBU..
FAIDA KWA WENGINE VIDONDA VYA TUMBO VINAWEZA KUSABABISHWA NA VITU MBALIMBALI SANASANA BAKTERIA AU ASIDI TUMBONI SASA TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO INATEGEMEA KITU KINACHOKUSABABISHIA NDIO TUNACHOTIBU NA HATIMAYE VIDONDA KUPOWA
 
Mkuu ni kweli mimi pia nna shida ya gesi nyingi sana tumboni. Vp ushauri wako nitumie dawa gani kukabiliana nayo?
Akhsante
Karibu better health 0699254400
IMG-20230525-WA0030.jpg
 
Kama upo Dar, nitakuunganisha na kijana wangu, akupeleke kwa mzee ambae yupo kibamba.

Anai amewapeleka watu, wamepona sasa wanakula maharage na Dagaa kama zamani, garama za dawa ni 50,000.
kaka kwema,naomba unisaidie namba tuwasiliane nina tatizo
 
Back
Top Bottom